Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,842
- 31,076
Nianze kunukuu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 18 ambayo inasema kila mwananchi anayo haki ya kutoa habari na kupokea taarifa, bila kuingiliwa na chombo kingine chochote.
Nimelazimika kuanza bandiko langu kwa kunukuu Katiba yetu ili tuone kama njia ambayo watawala wetu wanataka tupite kama ipo sahihi.
Tumeshuhudia katika miezi michache iliyopita, magazeti kadhaa ya kila siku yanayoonekana yana mlengo wa "upinzani" yakiwemo Tanzania Daima, Mwanahalisi, Mawio na Raia Mwema yakifungiwa.
Tumeshuhudia pia majuzi vituo vya luninga vya Star TV, ITV, Azam TV, Channel 10, East African TV navyo vikipigwa faini kubwa, kwa madai ya kutoa taarifa wa kile ambacho TCRA inakiita UCHOCHEZI kwa kumnukuu Mkurugenzi wa kituo cha Haki za binadamu ambaye aliitisha Press Conference kuelezea namna kituo hicho kilivyoufanyia tathmini uchaguzi mdogo wa madiwani 43 nchini kote uliofanyika Novemba 26 mwaka Jana
Kwanza hizo ni habari za kutisha sana kwa vituo vya luninga karibu vyote vya binafsi kukumbwa na kadhia hiyo ya kuripoti taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa kituo cha haki za kibinadamu, Dr Helen Kijo-Bisimba, aliyesema kuwa uchaguzi mdogo wa kata 43 haukuwa huru na haki kwa kuwa ulikiuka misingi ya uchaguzi kwa kupokea vurugu sehemu mbalimbali na sehemu nyingine hata mawakala wa vyama vya upinzani walitolewa kwa nguvu vituoni.
Swali kubwa ninalojiuliza hivi vituo binafsi vya luninga vimefanya kosa gani hadi TCRA iwaone wana hatia hadi kuwapiga faini?
Hivi siyo kweli kuwa uchaguzi huo haukugubikwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu hadi baadhi ya watu kukatwa mapanga?
Nikajiuliza pia hivi hili neno uchochezi limebadillika tafsiri yake na kuwa kila anayeisema vibaya serikali hii ya awamu ya 5 ndiye anayeonekana MCHOCHEZI?
Tunavyofahamu ni kuwa mhimili wa vyombo vya habari ni mhimili wa 4 wa nchi (ingawa hauko rasmi) baada ya ile ya Utawala, Bunge na Mahakama ambayo ipo rasmi.
Kwa hiyo ni mhimili muhimu sana ambao unapaswa kutetewa kwa nguvu zote
Nitamke kuwa katika kipindi hiki cha utawala wa serikali ya awamu ya 5 wapinzani wanapitia katika kipindi kigumu kuliko wakati wowote, tokea mfumo wa vyama vingi urejeshwe nchini mwaka 1992.
Niungane na maoni yaliyowahi kutolewa na mkongwe wa wana habari hapa nchini, Jenerali Ulimwengu, kuwa kidemoktasia nchi yetu imerudi miaka 50 nyuma!
Kwa hiyo ni wajibu wa kila mtanzania kuipigania misingi ya nchi yetu isiteteteke na hili ni suala la DO or DIE
Kwa kuwa kama alivyowahi kutamka Tundu Lissu kuwa utawala huu hautamwacha yeyote salama, maana yake itaanza na kuwanyamazisha wapinzani na baadaye mtafuatwa waandishi wa habari.
Mungu ibariki Tanzania