Vyeti vya kugushi- Aibu kwa watawala

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
16,952
10,500
habari ndio hiyo | Tarishi Hauwawi
Sakata la vyeti feki launguruma kila mahali Tanzania!

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 10:44 pm
Naomba ieleweke kuwa kuna makundi mawili hapa tunayoyaongelea: La kwanza ni kundi la akina Mzindakaya, JK , Karume, Rwakatare n.k. Hawa wana shahada za heshima tu (honoris causa) siyo za kusomea! Chuo chochote kinaweza mtunukia mtu shahada hiyo ya heshima kwa kutambua mchango wake katika jambo fulani. Siku za nyuma hata baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Spika Adam Sapi,
Salim Ahmed Salim, Kaunda na Obote walipewa heshima hiyo na vyuo mbalimbali duniani. Kundi lenye matatizo ni lile lenye shahada feki na linadai kuzisomea shahada hizo! Kundi hili ni hatari sana maana linaharibu kabisa heshima, sifa na viwango vya elimu nchini.
Wafuatao wana vyeti feki vinavyoitia aibu Serikali na nchi kwa ujumla:
(1) Salmin Amour – Ph.D yake ni feki, ya kisiasa. Aliipata Ujerumani Mashariki enzi hizo kwa miezi mitatu tu huku akiwa na cheti cha form four tu!
(2) Pius Ng’wandu – Ph.D yake ni feki. Chuo anachodai kusoma cha Stanford, Marekani hakina kumbukumbu zake. Aliosoma nao huko Marekani, akina Prof. Baregu, wanajua kuwa ana Masters tu!
(3) Mary Nagu – Ph.D yaje ni ya kununua kwenye mtandao.
(4) Emmanuel Nchimbi – Ph.D yake ya uchumi ni ya kununua. Hana uelewa wowote wa economics kichwani mwake.
(5) Makongoro Mahanga – Ph..D yake ya ugavi ni ya kununua kama Nchimbi.
(6) Didas Masaburi – Ph.D yake ilinunuliwa pamoja na ya kaka yake Makongoro.
(7) Norman Sigallah – Ph.D yake ni ya kununua kwenye mtandao.
(8) Mafwenga – Ph.D yake sawa na ya Sigallah
(9) Nangale – Ph.D yake ni kutoka chuo kimoja bomu cha chini ya viwango, London .
(10) Mathayo David – Ph.D ya kujipachika.
(11) Mutamwega – Ph.D yake ni feki, ya kununua. Mhusika hawezi kuandika hata sentensi moja sahihi ya Kiingereza.
(12) Lukuvi – Masters yake ni feki. Kaipata akiwa na sifa za elimu ya darasa la saba na cheti cha ualimu, class C..
(13) Samuel Chitalilo – Vyeti vyake vya elimu ya juu toka Uganda vyote ni feki. Ana kesi ya kujibu mahakamani!
Nimepata taarifa mbalimbali kuhusu vyeti vya Wabunge wafuatao:
Sigonda,
Capt.Komba,
Omari Mzeru na Savelina Mwijage.
Nazifanyia kazi. Nitazianika hapa muda muafaka!
Ijabu Ijabu kanipa hamasa sana juu ya suala hili. Wote aliowaeleza kweli wana vyeti feki na hata ukiongea nao, ni vihiyo vihiyo wa kutupwa! Naomba niongeze majina mengine kwenye listi la Mhe. Diodorus Buberwa Kamala, Mbunge wa Mkenge na Waziri wa A. Mashariki. Huyu bwana kasoma Mzumbe kama Nchimbi ambako mtandao wa vyeti feki ulianzia na Mkuu wa Chuo hicho Bw. Warioba. Ph.D yake ni feki, ni ya kununua kama hizo za wenzake aliowataja Ijabu.
Hata kwenye Bunge la A. Mashariki tunaambiwa anapwaya ile mbaya. Naibu wake, Mohamed Aboud, yeye ndo balaa maana ni form four failure na CV yake inasema uongo kuwa ana diploma ya Uingereza! Wote ni Ze Komedi mbele ya Wakenya, Waganda, Warwanda na Warundi!
Yupo huyu mama wa Kibaha, Zaibab Gama. Anajiita Dk. wakati ana diploma ya radiology tu!
Kuhusu Mbunge Savelina Mwijage (Viti Maalum, Kagera), huyu ana matatizo makubwa maana anatumia jina la marehemu. Taarifa zote zilitoka gazetini, lakini analindwa. Hawezi hata kuandika jina lake, lakini ni Mbunge. Anayebisha aje na ushahidi maana huyu mama namfahamu miaka mingi akiwa mfanyakazi wa ndani wa Mhindi Bukoba.
Namfahamu sana Mbunge Sigonda. Ni mtu wa usalama wa Taifa aliyeishia darasa la nane. Leo naambiwa ni Dk.! Hebu tupe dataz Ijabu na wana JF wengine.
Capt. Komba yeye ni msanii na mwizi asiyestahili kujadiliwa hapa maana anawaibia hata wasanii wenzake dani ya TOT. Mzeru wa Morogoro yeye ni mafix moja kwa moja. Hana udaktari wowote! Alijipachika udaktari kuombea ubunge na unaibu waziri kwa JK ! Agustino Lyatonga Mrema – Pacific Western University , a diploma mill. Yeye alipoenda kuchukua hiyo “degree” alikwenda na matarumbeta kibao, vifijo na nderemo.
Mustafa Mkullo – Almeda University , a diploma mill. Kule youngafrican. com nakumbuka ilisema eti chuo chake kiliwahi kutoa associate degree kwa mbwa anayeitwa “Wally” mali ya mwandishi mmoja wa habari huko Marekani (In 2004 the CBS affiliate in Albany , New York , ran a report on Almeda that featured Peter Brancato, who had filled out an application for an associate degree on behalf of his dog, Wally.
Part of the “life experience” listed on the application was “Plays with the kids every day … teaches them to interact better with each other … Teaches them responsibilities like feeding the dog.” Almeda granted Wally an associate’s degree in childhood development with a course list including European culture, college algebra, American history, and public speaking.[13] In reply, Almeda claims Brancato perjured himself by creating a false identity using a fabricated name and date of birth.
They write, “He completed an application that included a background of the following: Eight-years tutoring pre-K children, curriculum design and development, teaching coping skills, and volunteer coaching.”” Almeda University – Wikipedia, the free encyclopedia Kama sijakosea waheshimiwa wengi sana wana degrees kutoka chuo cha Washington International –
I think even Sofia Simba anayo ya huko Yona Fares Maro Master of Science in Computer Science and Information Systems (MS) University of Michigan-Flint
Thank You
 
Mwalla angalia KUCHA ZAKO NA MENO.Haujatwambia ya Nape Nnauye maana huyu Form four alipata division Five,form six alisomea chuo cha ualimu:confused::confused::confused:
Sasa wewe unaejua unamuomba kwanini
Weka hapa
 
Hii habari ni ya lini? Capt. Komba na Dr. Pius Ng'wandu kweli wapo hai? Leteni thread zenye uhalisia kwa wakati huu badala ya ku copy and paste mada za zamani!
 
Utakua umekopy na kupaste toka kwenye blog ambayo now haifanyi kazi tena sababu habari ni za zamaniiiiiiiii
 
Huyu mleta mada kakaa bar akinywa bia mpaka akaanza kusinzia kwenye kiti, mhudumu kamkurupusha na alipoamka akatuma hii mada JF, anawasimanga watu eti vyeti vyao ni vya kununua wakati yeye akili zake za kawaida zinazidiwa maarifa na hao anaowataja. Wengine wameshatangulia mbele za haki, wala haoni kwamba hawatendei haki!.
 
Habari ya zamani sana ila inaweza kuwa Bado ina mashiko, kama hawakushugulikiwa wachunguzwe. Ila mkuu umeshaaga kwenu maana sio muda mahakama ya hakimu mkazi Kisutu itahitaji ushirikiano wako
 
Hii habari ni ya lini? Capt. Komba na Dr. Pius Ng'wandu kweli wapo hai? Leteni thread zenye uhalisia kwa wakati huu badala ya ku copy and paste mada za zamani!
Samahani hivi pius ng'wandu alishatangulia?lini...
 
Huyu mleta mada kakaa bar akinywa bia mpaka akaanza kusinzia kwenye kiti, mhudumu kamkurupusha na alipoamka akatuma hii mada JF, anawasimanga watu eti vyeti vyao ni vya kununua wakati yeye akili zake za kawaida zinazidiwa maarifa na hao anaowataja. Wengine wameshatangulia mbele za haki, wala haoni kwamba hawatendei haki!.
Hao walio hai kama anawasingizia si wamshitaki tu, kama Ni mzushi si wathibitishe
 
Back
Top Bottom