Ushauri: Vyama vya Upinzani vifutwe, kibaki CCM pekee kama chama dola

Ccm itaondoka au kufa pale tu tanzania itakaporidhia katiba ya wananchi au tume huru ila bila hayo yote ni ndoto.
 
Chadema imeimarika na kustawi zaidi baada ya ujio wa Lowasa hata kama Urais hatutaupata. Utitiri wa wabunge na madiwani tunaopata ktk uchaguzi na idadi ya kura za Urais zitaongeza ruzuku maradufu kwa kazi za chama. Na huu mtandao wa UKAWA Bungeni kuna uwezekano tukapata Spika na hata Waziri Mkuu. Ujio wa Lowasa Chadema na UKAWA umeleta manufa zaidi kuliko madhara.
 
Nikupe history kidogo mfumo wa vyama vingi hatukuupenda kabisa lakni wazungu wakatwambia kama hamtakuwa na vyama vingi hatuwapi misaada so that tukaogopa kukosa misaada ndo kisa cha kuwa na mfumo wa vyama vingi

nani kakwambia uwongo huo wakati vyama vilikuwepo hata kabla hatujapata uhuru. tafuta histori ya kipindi cha TANU ujue. ila mwl nyerere aliona mfumo wa vyama vingi kwa wakati kama ule ulikuwa haujengi umoja (hasa katika misingi ya kijamaa) ila pia alijua demokrasia nzuri ni pale watu wakaweza kuwa na uhuru wa kuchagua.

nakubaliana na mtoa maada kwanza kwasababu alizo zitoa pili naongezea kuwa kwa jinsi tume ya uchaguzi ilivyo haina haja ya kuwa na ushindani wala kupoteza fedha nyingi kwenye kampeni.
 
Vyama vya upinzani viko wapi? Lowassa unamwita mpinzani. Hamna akili kabisa nyie Chadema
 
Ukweli utabakia kweli hata kama utakuwa mchungu. Si rahisi kwa vyama vya upinzani kuchukua dola nchi hii kwa mfumo tulionao. Sasa hivi si rahisi kutofautisha chama tawala na dola, ni kama pete na chanda. CCM imejijenga na kujiimarisha zaidi kupitia watendaji wa serikali ambao kimsingi si wanasiasa, ila kwa kulipa fadhila ya aliyewateua. Unategemea nini kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, Wilaya, Mkurugenzi wa Wilaya, Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Polisi, Magereza, Usalama wa taifa, tume ya uchaguzi na Wateule wengine wa Taasisi za Umma na mashirika yake? Wote hao wako pale kujikomba kwa chama tawala ili maisha yao yaendelee. Hivyo utaona kuwa mfumo mzima unakilinda chama tawala na si rahisi kwa mtu aliye nje ya mfumo kujipenyeza ndani. Hivyo basi kitu pekee cha kupigania ni kupata katiba mpya kama ilivyopendekezwa na Jaji Joseph Warioba.
 
Hapana usikate tamaa siku yao itafika haitakuwepo tena,usikate tamaa na wala kuwakatisha tamaa wenzio
Pambana hakuna ubwete hivyo.
 
Ila sasa, kikiwepo ccm peke yake halafu wawe wanajichagulia rais kivyao vyao mtashuhudia vifo vya viongozi hadi mshangae, watachinjana haoooo, loh. Kwa tabia hii waliyojijengea! Kila mmoja atakuwa anawaza awe yeye na akiona kuna dalili ya upinzani shingo halali yake
 
Nyie kateni tamaa lkn mimi siwezi kurudi Misri nitapambana mpaka nifike nchi ya ahadi,siwezi kuwaacha wanangu jangwani ki-raisi namna hii. Na hata nisipofika sina shaka nitakapoishia hapatakuwa mbali na nchi ya ahadi, jambo ambalo litawafanya wasitembee mwendo mrefu. Mungu nisaidie

Hili ndiyo jibu halisi la mada husika.
Asane sana!
 
Ujio wa Lowassa ni ushindi wa Cuf zenji.... watawala waliwekeza sana bara na kwa uwoga mkubwa wakamtelekeza mwenzao zenji.... demokrasia kwa nchi za kiafrica ni process ndefu.... kumtoa mtawala mwenzako mlie oleana au wa rangi yako ni shida kuliko mkoloni... hapana sikubaliani na mtoa mada.... tuendelee kushinikiza kwa njia zetu na external forces bila mapanga wala mtutu wa bunduki.... siku moja ya zanzibar yatatokea huku.... ccm mnayo iona na uchovu wake, 2015 to 2020 haitakuwa the same.... watabadilika na hilo ndo tunalo taka, pia nasika JPM kagoma kuwa mwenyekiti wa ccm, anataka ccm ijiendeshe na kujijenga..... tusichoke wakuu... demokrasia kwa nchi zetu ni process ndefu...
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu siasa za Tanzania tangu miaka ya tisini. Baada ya uchaguzi wa mwaka huu,nimeamua kukubali kuwa CCM hakitakaa kiondoke madarakani kwa njia yoyote ile unayoijua wewe duniani kwa sasa, hata kama itafanya vibaya namna gani!

Mipango yote,mikakati yote ya kukiondoa chama hiki haiwezi kufanikiwa kwa kuwa ukweli unaonekana dhahiri kuwa kimewekeza sana katika kuhakikisha kinakuwa salama baada ya uchaguzi hata kama ni kwa gharama ya maisha ya watu wake.

Mikakati wanayoifanya CCM ni pamoja na kuhakikisha wanatumia inteligensia ya taifa,kuhakikisha kuwa hakuna chama kinachoweza kukua na kuwa tishio kwa ccm halafu kikabaki salama. Kwa watu wengine tulijua mapema jinsi cdm ilivyouwawa hata kabla ya kuingia katika uchaguzi huu. Naweza kusema hivi chadema ilivyo ni kwa sababu ya ubishi na uhodari wa Mbowe. Naamini wasingefika hata hapo walipo bila uthabiti wa viongozi wa juu akiwemo pia dr Slaa.

Kwa hali ilivyo, ninajaribu kuviona vyama vya upinzani kama vile vinatumika kuweka uhalali wa kuendelea kutawala kwa ccm mbele ya jamii ya kimataifa. Baadhi ya vyama vinavyoonekana kuanza kuwa tishio hukabiliana na misuko suko mikubwa na hata kwa baadhi ya wanachama wake kupoteza maisha kwa vile tu wao ni wapinzani. Sasa nadhani umefika wakati ili kuepusha watu wasio na hatia kuumia kwa vile tu ni wapinzani,vyama hivi vifutwe na kibaki chama kimoja kama zamani. Hakuna sababu ya ccm kutumia nguvu kubwa na rasilimali za taifa kwa kuandaa uchaguzi ambao wao wanajua wanataka kushinda kwa namna yoyote ile.

Nawaomba watanzania waniunge mkono katika hili, wale wabunge waliochaguliwa kupitia upinzani, mniunge mkono kwani mnaweza kugombea tena kupitia CCM pia. Sioni tumaini tena katika mfumo huu wa vyama vingi. Ni bora kuwe na mfumo wa mgombea binafsi au hata CCM wachaguane wenyewe kama wanavyopenda ili mradi watu wasiumie kwa sababu ya uadui wa kisiasa.

Umelogwa wewe.. si bure!
 
Kwa mambo mengi yanayojitokeza katika uchaguzi ulio katika mfumo wa Vyama Vingi tangu uanzishwe hapa kwetu TZ, ni maoni yangu kuwa tulazimika tu kuingia katika mfumo huu, hatukuwa tayari. Ushindani wa kweli ulikuwamo ndani ya chama kimoja kwani wagombea wote walikuwa ni wa baba na mama moja. Vinginevyo tuwarudie waliotushauri au kutuwekea mazingira ya kulazimika kuingia kwenye ushindani wa vyama vingi ili watueleze wao wanashindana vipi bila mabomu ya kutoa machozi, wanavumilia vipi matokeo yanapochelewa kutolewa, wameweka misingi gani inayokitenganisha chama kinachotawala na dola nyakati za uchaguzi ili wawe na mazingira sawa na vyama vingine, na nani anaisimamia dola wakati wa uchaguzi. Ni dhahiri kuna mengi ya kujifunza huko.

Mfano moja wa jambo la kujifunza: nilikuwa masomoni Uingereza wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010 uliomwingiza madarakani David Cameroon wa Conservatives, hakupata kura za kutosha kuunda serikali mwaka huo, akalazimika (kwa mujibu wa sheria zao) kushirikiana na Nick Cleg wa Liberal Democrats. Wakati wa kampeni, Tume ya Uchaguzi ndiyo iliyowapangia Midahalo Mitatu (3). Haikuwa hiari kuhudhuria kwa wagombea wa Uwaziri Mkuu, bali ilikuwa ni lazima. Tena midahalo hiyo ilipangwa kufanyika miji tofauti-tofauti. Ninakumbuka Mdahalo wa kwanza ulifanyika jijini London, wa pili ulifanyikajjiji la Bristol na wa tatu nimesahau mji lakini ni ndani ya Uskochi (Scotland). Kila mji wagombea walipewa mambo kama matatu hivi kueleza sera za vyma vyao zitayatekeleza vipi. Mambo haya kwetu hatuyaoni, midahalo ni hiari ya vyama au wagombea nk.

Ninadhani amani ya Tz itakuwa katika mikono salama zaidi tukirudi kwenye mfumo wetu wa chama kimoja, tukaboresha misingi ya ushindani ndani mwake - HAYA NI MAWAZO YANGU TU.
 
Mimi naunga mkono ushauri wako iwapo tu katiba iliyopo ndo itaendelea kuwepo hata kwenye chaguzi zinazoendelea,lakini kama katiba itabadilishwa mbona hawa wetu tena ni wepesi sana.
 
CCM kingesimama kama chama cha kiasa ungekuta kimekufa muda mrefu ila ccm kimesimama kama serikali, polisi, jeshi, usalama wa taifa n.k. Sasa nguvu zoote hivi huwez kushindana nazo

Kwa mwendo huu , Mwisho wa njia tutageuka Syria
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu siasa za Tanzania tangu miaka ya tisini. Baada ya uchaguzi wa mwaka huu,nimeamua kukubali kuwa CCM hakitakaa kiondoke madarakani kwa njia yoyote ile unayoijua wewe duniani kwa sasa, hata kama itafanya vibaya namna gani!

Mipango yote,mikakati yote ya kukiondoa chama hiki haiwezi kufanikiwa kwa kuwa ukweli unaonekana dhahiri kuwa kimewekeza sana katika kuhakikisha kinakuwa salama baada ya uchaguzi hata kama ni kwa gharama ya maisha ya watu wake.

Mikakati wanayoifanya CCM ni pamoja na kuhakikisha wanatumia inteligensia ya taifa,kuhakikisha kuwa hakuna chama kinachoweza kukua na kuwa tishio kwa ccm halafu kikabaki salama. Kwa watu wengine tulijua mapema jinsi cdm ilivyouwawa hata kabla ya kuingia katika uchaguzi huu. Naweza kusema hivi chadema ilivyo ni kwa sababu ya ubishi na uhodari wa Mbowe. Naamini wasingefika hata hapo walipo bila uthabiti wa viongozi wa juu akiwemo pia dr Slaa.

Kwa hali ilivyo, ninajaribu kuviona vyama vya upinzani kama vile vinatumika kuweka uhalali wa kuendelea kutawala kwa ccm mbele ya jamii ya kimataifa. Baadhi ya vyama vinavyoonekana kuanza kuwa tishio hukabiliana na misuko suko mikubwa na hata kwa baadhi ya wanachama wake kupoteza maisha kwa vile tu wao ni wapinzani. Sasa nadhani umefika wakati ili kuepusha watu wasio na hatia kuumia kwa vile tu ni wapinzani,vyama hivi vifutwe na kibaki chama kimoja kama zamani. Hakuna sababu ya ccm kutumia nguvu kubwa na rasilimali za taifa kwa kuandaa uchaguzi ambao wao wanajua wanataka kushinda kwa namna yoyote ile.

Nawaomba watanzania waniunge mkono katika hili, wale wabunge waliochaguliwa kupitia upinzani, mniunge mkono kwani mnaweza kugombea tena kupitia CCM pia. Sioni tumaini tena katika mfumo huu wa vyama vingi. Ni bora kuwe na mfumo wa mgombea binafsi au hata CCM wachaguane wenyewe kama wanavyopenda ili mradi watu wasiumie kwa sababu ya uadui wa kisiasa.

Hakuna mahali popote duniani ambapo mwenye shibe aliyetumika kumkomboa mwenye njaa; ni hadi vyama vya upinzani vitakapokuwa vinaongozwa na malofa ambao hawana cha kupoteza ila roho zao ndipo upinzani utakapokuwa wa kweli. Viongozi wote wanaoongoza vyama vya upinzani ni viongozi masilahi na hawafai. Cha pili ni wakati; wakati bado haujatimu vizuri yaani pale mtu anapokuwa hana njia nyingine yoyote ya kujipatia mkate wake ni ama afe ama mnyang'anyane. Kwa sasa njaa hazijakaba vizuri bado ipo fursa ya mtu kujipatia mkate wake kwa vijiharakati; bali sisiem itakapokaba kila mahali hadi kijimkate hakipatikani hata kwa harakati hapo ndio ukombozi utakuwa umeiva. Kwa maneno mengine ccm haijatawala vibaya vya kuchusha ndio maana bado inaponea
 
Back
Top Bottom