Vyama vya upinzani, unafiki na tamaa ya pesa

Vyama vya upinzani, unafiki na tamaa ya pesa

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
14,696
Reaction score
32,273
Mwaka 2020 asilimia 95 ya wapinzani hasa wa Chadema na ACT wanajua kuwa hawatapata nafasi za Ubunge na Udiwani. WANAJUA KABISA HILI PASINA SHAKA.

Ni hawa hawa wapinzani wanaosema kuwa TUME YA UCHAGUZI SI HURU. Sasa swali linakuja wanaenda shiriki uchaguzi wakitegemea nini? Kuwa utatokea muujiza ghafla Tume wakati wa kutangaza matokeo itakuwa huru?

Haya ni mambo yanayofikirisha sana; ni either wapinzani hawajiamini ndo maaana wanasingizia tume ili wakishindwa waje waseme "tuliwaambia" au ni kwa sababu wanataka wapate nafasi ya kutumia pesa za vyama kwa maslahi yao binafsi wakati wa kampeni.

Ni mwendawazimu tu ambaye anaenda kushiriki uchaguzi akijua kuwa hatoshinda, why sasa ashiriki? Miaka zaidi ya 25 wapinzani wanapiga kelele kuwa Tume ya Uchaguzi si huru na Katiba si rafiki kwa uchaguzi huru, but still wanashiriki.

"Wendawazimu ni kufanya jambo lile lile kwa njia ile ile na kutegemea matokeo tofauti"

Unajiuliza mwaka 1995, 2000, 2005, 2010, 2015 miaka yote hiyo wanalalamikia tume ya uchaguzi. Wanalalamikia katiba kuwa ni mbovu kwao. Lakini unawaona wanashiriki kupiga kampeni na kugombea nafasi mbalimbali. Unajiuliza kwa lengo gani?

TUFIKIE HATUA TUWE WAKWELI MAMBO YA KUFANYANA WATOTO SI MAZURI.
 
Kwahyo wewe unakubali kuwa tume sio huru. Na hivyo basi hakna haja ya vyama tajwa kushirk uchaguzi sio? Wewe kwa kutokuwa na Tume huru kunakupa furaha sio?

Kwa kusoma historia ya nchi hii unakubali kuwa baba au babu yako ama wewe mwenyewe hukushirk kwenye mchakato wa mstakabali wa katiba hii ilyopo sio?

Je, ndugu yako ama jirani yako alishiriki? Unakubali kuwa toka katiba hii imeundwa kuna mabadiliko mengi ya nyakat na mambo ya kiteknolojia, elimu nk? Kama ndvo unadhani katiba ile inafit?

Kwanini tushangilie kitu kilichowazi wakati tunauujua ukweli? Nini kinatufanya tujitoe ufahamu?je ni kwasabb tunafaidika na katiba?
 
Wewe ndiyo hufai. Wamesusia baadhi ya chaguzi matokeo ni yapi ?! 2016 Zanzibar walisusia kilichotokea ni kuwepo kwa wapinzani waigizaji walioishia kupewa uwaziri .

2019 Baada ya figisu nyingi CHADEMA walisusia uchaguzi wa serikali za mitaa. Kilichotokea ni nini ?! Ni Ccm kudai kushinda kwa kishindo na hivyo Cdm kupoteza vijiji, mitaa, na vitongoji vyote walivyokuwa wanaviongoza. Sasa hasara ni ya Nani ?!.

Tanzania, wananchi wangekuwa na silka na hulka za vurugu . Hayo mambo ya katiba na Tume huru vingeshapatikana. Wanaotawala wametumia mwanya wa wananchi kuwa wastaarabu kuwanyima stahili yao.
 
Na bado katiba inataka kutengenezwa vizuri kuzuia baadhi ya viongozi kuwa na kinga kutoshtakiwa.

Inamaana ukiambiwa una saratani au ukimwi usichukue tahadhari zozote au kufanya jitihada za matibabu kwa vile utakufa?
 
Wewe ndiyo hufai. Wamesusia baadhi ya chaguzi matokeo ni yapi ?! 2016 Zanzibar walisusia kilichotokea ni kuwepo kwa wapinzani waigizaji walioishia kupewa uwaziri .

2019 Baada ya figisu nyingi CHADEMA walisusia uchaguzi wa serikali za mitaa. Kilichotokea ni nini ?! Ni Ccm kudai kushinda kwa kishindo na hivyo Cdm kupoteza vijiji, mitaa, na vitongoji vyote walivyokuwa wanaviongoza. Sasa hasara ni ya Nani ?!.

Tanzania, wananchi wangekuwa na silka na hulka za vurugu . Hayo mambo ya katiba na Tume huru vingeshapatikana. Wanaotawala wametumia mwanya wa wananchi kuwa wastaarabu kuwanyima stahili yao.

Kule vyama au chama kususia uchaguzi ni suicidal, self distraction na kutokuwa na vision. 2015 ulikuwa ni mwaka wa Wapinzani lakini walichezea shillingi chooooooni! 2020 CUF, ACT-Wazalendo hawatapata mbunge hata mmoja Tanzania Bara, pia CUF haitapata mwalikishi kule Zenj!
 
Unasema nini na unatetea nini ?!. Kama play ground ingekuwa neutral usingesema hayo. Nashangaa mtu kutamba kwenye uchaguzi uliojaa hila.
 
Ulipaswa upiganie tume huru ya uchaguzi sio kuwalaumu wapinzani manake tume huru ni kwa faida yako pia. Siku moja nina uhakika mtalia kwa sababu ya udikteta lakini kumbe nyie wenyewe ndio mmeusababisha.
 
Huwezi kuacha kushiriki uchaguzi hata kama tume si huru nchi nyingi haki haiombwi lakini hutolewa kwa nguvu na njia moja ni kushiriku uchaguzi
 
So unashiriki uchaguzi ili iweje? Ukishindwa uje useme tume si huru wakati ulijipima ukajua utashindwa?

Huwezi kuacha kushiriki uchaguzi hata kama tume si huru nchi nyingi haki haiombwi lakini hutolewa kwa nguvu na njia moja ni kushiriku uchaguzi
 
Back
Top Bottom