MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,976
Mtoa mada Unaumwa au umetumwa!! Hakuna jingine kati ya hayo.
Wagonjwa wa akili si lazima wawe Mirembe tu..... Source: mimi mwenyewe babu Asprin a.k.a ODM.
vyama gani vimeshindwa???? kwenye chaguzi zipi?????
Ukweli husemwa:
Tumekuwa na chaguzi kuu tatu na chaguzi ndogo nyingi tu ambazo pamoja na CCM kuchoka kuongoza lakini bado wananchi wanaipa kura. Kosa siyo wananchi kuipa CCM kura, Kosa ni viongozi wa vyama vya upinzani kushindwa kufanya kazi yao vizuri ili wananchi wawaamini na kuwapa uongozi wa nchi.
Mtoa mada Unaumwa au umetumwa!! Hakuna jingine kati ya hayo.
Baada ya maelezo yako yoote hayo ambayo sikuwa nayahitaji, sasa unaweza kujibu swali langu tafadhali?
Niliuliza hivi:
Vyama gani vimeshindwa ??????? Kwenye chaguzi zipi?????
Inatakiwa ufuatilie kwa ukaribu CCM imeshinda vipi, wewe ulitaka na vyama vya upinzani vinunue shahada za wapiga kura, kuna baadhi ya majina ya vijana hayajaonekana kwenye daftari la kura ulitaka viongozi wafanyeje ili hao vijana wapige kura.Ukweli husemwa:
Tumekuwa na chaguzi kuu tatu na chaguzi ndogo nyingi tu ambazo pamoja na CCM kuchoka kuongoza lakini bado wananchi wanaipa kura. Kosa siyo wananchi kuipa CCM kura, Kosa ni viongozi wa vyama vya upinzani kushindwa kufanya kazi yao vizuri ili wananchi wawaamini na kuwapa uongozi wa nchi.
Ukweli husemwa:
Mkuu, Mbona nilikujibu.
Chaguzi kuu tatu, CCM bado iko madarakani.
MsemajiUkweli
Ukweli ambao hujausema ni huu.
Kuwa CCM bado iko madarakani baada ya chaguzi(chafuzi) kuu tatu kwa sababu hata wenyewe wanasema kuwa wanashinda kwa ushindi wa kishindo na sio kwa kura.
Kishindo hapa unaweza kukitafsiri:
-Kubebwa na Katiba ambayo hakuna ambaye hajui kuwa katiba iliyopo ni kwa ajili ya kuibeba/kuibakisha madarakani CCM.
-Vyombo vya dola, polisi, usalama wa taifa, mahakama hazitekelezi majukumu yake kama vyombo vya taifa badala yake vinafanya kazi kama matawi ya CCM. Lengo ni kuibeba/kuibakisha CCM madarakani.
Lakini nakubaliana na wewe kuwa viongozi wa vyama vya upinzani wanapaswa kuwajibika.
Bado baada ya chaguzi(Chafuzi) kuu tatu hawajaona umuhimu wa kupigania kuwepo kwa tume ya uchaguzi uliyo huru.
Bado hawahakikishi vyombo vya dola vinafanya kazi kama vyombo vya nchi na sio kama vyombo vya chama.
Bado wanashiriki kwenye chaguzi (chafuzi) hizo.
Lakini wa kuwajibika hasa ni CCM na viongozi wa CCM(hata serikali wanasema ni serikali za CCM). Uvumilivu wa watanzania utafikia kikomo na hapo "amani ,mshikamano na utulivu" ambao CCM na serikali zake zinauchezea kama mwanaserere na wakisema kama asemavyo Pinda."Liwalo na Liwe" hatutazungumzia tena "kisiwa cha amani".
Mifano ya nchi jirani kama haitoshi kuwa fundisho kwetu; madhara yake, makovu yake huhitaji miaka kadha, miongo kadhaa kufutika. Katika CCM kama bado wamebaki walio weledi na wenye upeo wa kuona mbali walione hili na watuepushe kufika huko.
Ukweli husemwa:
Tanzania imeingia miaka ishirini (20) toka mageuzi makubwa ya kisiasa yalipoanziswa. Tumeshuhudia kufanyika chaguzi kuu tatu zikiambatana na chaguzi ndogo nyingi mbalimbali, na katika chaguzi zote, CCM imekuwa ikishinda kwa kura nyingi.
Nchi nyingi za demokrasia duniani, pamoja na kwamba chaguzi ndogo huwa siyo kipimo mahsusi cha hali ya kisiasa katika chaguzi kuu nchini, lakini ni kipindi ambacho mara nyingi vyama vilivyoko madarakani huwa vinakuwa vimepunguza umaarufu kwa muda katika jamii kutokana na matatizo ya utendaji serikalini au mchakato katika utekelezaji wa ilani zake za uchaguzi. Hapa nchini imekuwa ni tofauti kwa sababu hata katika chaguzi ndogo, CCM ilikuwa ikafanya vizuri.
Wiki hii tutashuhudia chaguzi ndogo zingine ambazo Wananchi wengi na wadadisi wa mambo ya kisiasa wanatumaini matokeo yatakuwa ni tofauti na miaka ya nyuma. Vyombo vingi vya habari na wananchi wengi wanatabiri vyama vya upinzani kushinda kwa kiwango cha juu katika kata nyingi nchini. Kama nilivyobainisha hapo juu, hakuna sababu kwa nini visishinde kwa kiwango hicho cha juu ukichukulia kuwa viongozi na wanachama wa CCM hawakujihusisha ipasavyo katika kampeni nyingi kutokana na kuwepo kwa chaguzi za viongozi wao ndani ya chama. Kampeni za udiwani hazikupewa kipaumbele.
Kwa wapenda demokrasia ya kweli, haikubaliki hata kidogo kwa vyama vya upinzani kuendelea kufanya vibaya hata kwenye chaguzi ndogo wakati historia inabainisha kuwa ni lazima vifanye vizuri. Ninafikiri ni vizuri kwa viongozi wa vyama vyetu vya upinzani kutafakari na kuchukua maamuzi ya kuwajibika kwa kujiuzuru ili kuwapisha wanachama wengine kuviongoza vyama kama matokeo katika chaguzi hizi ndogo yataendelea kuipa CCM ushindi zaidi.
Viongozi wetu wa kisiasa lazima waondoe hii dhana ya kuwa chama ni Baba na Mama yao na pia ni sehemu ya kuvuna tu mapato badala ya kuvuna wananchi na kukijenga chama kwa ufanisi. Hatuwezi kuendelea kujivuna kama tuna demokrasia nchini wakati vyama vya kisiasa haviendeshwi kwa demokrasia ya uwajibikaji.
Nawasilisha...
Kwanini hao VIONGOZI wakishindwa WAWAJIBISHWE? Kwenye kila chamakinachokwenda kwenye UCHGUZI huwa inachagua PLATFORM zao; sasa ni kumaanish platform zilikuwa introduced hazikuneemesha CHAMA well kun njia zipasavyo kuondoa VIONGOZI; Sababu HOJA zinaweza zikawa nzuri kweli, ukaopewa Wewe Mwakilishi Ukashindwa kupanua HEKIMA zako kuonekana kama vile YOU OWN and SUCH STRATURGIES or we now leaders we dont understand act of POLITICS just tht arc to the act of siphonic the weath of mother nature.
Our leaders shines like flowers some with Education and some with no education but wealth to dream for...
So, Who will ever strict politicoi? Until U become part of them..."Revolution is not a dinner party, not an essay, nor a painting, nor a piece of embroidery; it cannot be advanced softly, gradually, carefully, considerately, respectfully, politely, plainly, and modestly." Just hold your heads Up with PRIDE
,
Ukweli husemwa:
Tanzania imeingia miaka ishirini (20) toka mageuzi makubwa ya kisiasa yalipoanziswa. Tumeshuhudia kufanyika chaguzi kuu tatu zikiambatana na chaguzi ndogo nyingi mbalimbali, na katika chaguzi zote, CCM imekuwa ikishinda kwa kura nyingi.
Nchi nyingi za kidemokrasia duniani, pamoja na kwamba chaguzi ndogo huwa siyo kipimo mahsusi cha hali ya kisiasa, lakini ni kipindi ambacho mara nyingi vyama vilivyoko madarakani huwa vinakuwa vimepunguza umaarufu kwa muda katika jamii kutokana na matatizo ya utendaji serikalini au mchakato katika utekelezaji wa ilani zake za uchaguzi. Kutokana na hili, mara nyingi huwa vinashindwa kwenye chaguzi ndogo. Hapa nchini imekuwa ni tofauti kwa sababu hata katika chaguzi ndogo, CCM imekuwa ikifanya vizuri.
Wiki hii tutashuhudia chaguzi ndogo zingine ambazo Wananchi wengi na wadadisi wa mambo ya kisiasa wanatumaini matokeo yatakuwa ni tofauti na miaka ya nyuma. Vyombo vingi vya habari na wananchi wengi wanatabiri vyama vya upinzani kushinda kwa kiwango cha juu katika kata nyingi nchini. Kama nilivyobainisha hapo juu, hakuna sababu kwa nini visishinde kwa kiwango hicho cha juu ikizingatiwa kuwa viongozi wengi na wanachama wa CCM hawakujihusisha ipasavyo katika kampeni nyingi kutokana na kuwepo kwa chaguzi za viongozi wao ndani ya chama. Kampeni za udiwani hazikupewa kipaumbele ndani ya CCM mwaka huu.
Kwa wapenda demokrasia ya kweli, haikubaliki hata kidogo kwa vyama vya upinzani kuendelea kufanya vibaya hata kwenye chaguzi ndogo wakati historia inabainisha kuwa ni lazima vifanye vizuri. Ninafikiri ni vizuri kwa viongozi wa vyama vyetu vya upinzani kutafakari na kuchukua maamuzi ya kuwajibika kwa kujiuzuru au kuwajibishwa ili kuwapisha wanachama wengine kuviongoza vyama kama matokeo katika chaguzi hizi ndogo yataendelea kuipa CCM ushindi zaidi.
Viongozi wetu wa kisiasa lazima waondoe hii dhana ya kuwa chama ni Baba na Mama yao na pia ni sehemu ya kuvuna tu mapato badala ya kuvuna wananchi na kukijenga chama kwa ufanisi. Hatuwezi kuendelea kujivuna kama tuna demokrasia nchini wakati vyama vya kisiasa haviendeshwi kwa demokrasia ya uwajibikaji na vingine vikizidi kudidimia huku viongozi wake wakijitajirisha na malipo kutoka kodi ya wananchi.
Nawasilisha...
UPDATES
Matokeo ya chaguzi ndogo zilizofanyika tarehe 28/10/2012
Viti vilivyokuwa wazi ni katika kata 29
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda kata 23 ni sawa na 79.3%
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda kata 5 ni sawa na 17.2%
Tanzania Labour Party kimeshinda kata 1 ni sawa na 3.4%
angalizo:
Kwa sasa ni kipindi cha viongozi wa kisiasa wa vyama vya upinzani kutafakari na kupisha nguvu mpya ili ilisukume gurudumu la mabadiliko ya kisiasa kwa nguvu na mbinu mpya, kutokufanya hivyo ni kutowatendea haki wananchi wanaowaongoza.