APA CHICAGO
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 259
- 292
Mwaka huu hapo October kutakuwa na uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani. Ninaimani mtasimamisha wagombea wa urais, wabunge na madiwani.
Nataka tusemezane jambo moja kubwa kwa kuwa wabunge na madiwani wa upinzani baada ya uchaguzi wanahamia CCM hatimaye taifa linaingia gharama za kurudia uchaguzi mwingine je? Kuna haja ya kuwachagua watu hao ambao huko mbele watahamia CCM?
Najua kuna watu watakuja hapa na hoja kuwa ooh wananunuliwa.
Yes kama wananunuliwa kumbe hawafai hata kidogo kuwa viongozi kwani wanapokea rushwa na kama wanapokea rushwa wanaweza pia kutoa rushwa hivyo hawafai kuwa viongozi. Lakini pia yote wanayokutana nayo ndiyo changamoto za kazi yao hivyo walipaswa wazikabili sio kuzikimbia.
Mfano Hayati mwalimu JK Nyerere angeogopa changamoto za kesi za uchochozi nakadhalika wakati wa kudai Uhuru wa nchi yetu pengine tungalikuwa hadi leo tuko chini ya UKOLONI wa watu weupe.
Mbaya zaidi kuna wabunge wa upinzani hatujawahi ona wanatoa michango ya maana bungeni lakini wanapotaka kuhamia CCM au Chama kingine ndo wanasikika hii sio sawa.
Tujiulize swali fikilishi hivi hao wabunge walichaguliwa ili Wakawasemee wananchi matatizo yao au Wakatangaze wanahama chama? Je, haya siyo matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi wa nchi hii?
Imagine hivi hawa wangeitisha mkutano wa waandishi wa habari wakasema hayo nje na bunge wangepungukiwa nini?
Tuna tatizo kubwa sana kwani kuna watu wanatumia kodi ya wananchi vibaya. Kwa mwenendo huu kama taifa
bado tunasafari ndefu sana kufika tunakotaka kufika.
Mtu hata asemeje Mimi bado nasema wanasiasa hama hama hawa ni tatizo kubwa kwenye nchi yetu maana wao matumbo yao ni bora kuliko kuwatumikia wananchi. Tujiulize kwani akina Zitto, Msigwa, Mdee Heche na wengine wengi wao hawajawahi shawishiwa wahame vyama vyao Lakini mbona hadi leo bado hawajahama vyama vyao.
Ushauri wa bure ni heri tuwapigie kura CCM washinde ili tuepuke gharama za kurudia uchaguzi na kupogezeana muda wa kupanga foleni.