Vyama vya upinzani haviaminiki kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,239
7,793
Hii inatokana na wimbi la wabunge na madiwani wa vyama vya upinzani kukimbia vyama vyao na kuhamia CCM.

Tumeshuhudia wabunge na madiwani wa CHADEMA, ACT, CUF wakihamia CCM kwa kasi kubwa. Hii inatoa picha kuwa vyama vya upinzani haviaminiki kwa wapiga kura wala wao kwa wao hawaaminiani.

Na hii inatoa picha kuwa kutakuwa na anguko kubwa sana la wabunge wa upinzani, sidhani kama kutakuwa na wabunge au madiwani wa upinzani.

Vyama vya upinzani inaonyesha vimeishiwa punzi kabisa, wakati huu ndio wenyewe wa kujipanga na kujizatiti lakini kwa haya yanayotokea si ajabu tukashuhudia hata wenye viti wa vyama na makatibu wakihamia CCM.

CCM oyeee!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe. Kama sio mbunge wa upinza bw. Sugu mngekua mnaendelea kugomewa maiti kwenye hospitali za serikali. Serikali ya CCM ilikua haitoi maiti kama gharama hazijalipwa. Sijawahi kuona serikali inayodai maiti madeni
 
Kuhamia ccm ni ujinga na tamaa tu ya matumbo yao kuliko Sela za vyama vyao wanazotupatia kila uchwao majukwaani,hawana pa kushika tena Wapinzani,kila walilokuwa wanalipgia kelele Magu kalifanya kama sio kuligusia,Leo wamebaki kusema Tanzania hakuna democrasia wakati wao wanaotaka hiyo Democrasia hawana Uzalendo.
 
Sasa kosa la upinzani nn kama kuna waliongia na wakaamua kuondoka.....

Kufanya siasa upinzani ni changamoto sana kwasababu ya huyu mwengine kutumia vyombo vya umma vibaya/ mfumo kufanya vyombo vya umma kutumika vibaya.....

Mfumo ulivyo CCM kikiwa chama cha upinzani basi nacho maisha yake lazima yawe magumu, ndio maana wanafanya uhuni wowote ule wasitoke waliposhikilia.
 
nakumbuka kauli ya Hayati Mwalimu Nyerere alisema" UPINZANI WA KWELI UTATOKANA NA CCM" SI vinginevyo , hadi sasa CCM inaonekana kuwa IMARA zaidi kuliko wakati mwengine......kwa kiwango kikubwa utendaji wa awamu ya tano umekibeba na kukiimarisha zaidi chama.
si vibaya wala dhambi CCM ikashinda kiti cha urais, ubunge na udiwani wa asilimia 99%.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kosa la upinzani nn kama kuna waliongia na wakaamua kuondoka.....

Kufanya siasa upinzani ni changamoto sana kwasababu ya huyu mwengine kutumia vyombo vya umma vibaya/ mfumo kufanya vyombo vya umma kutumika vibaya.....

Mfumo ulivyo CCM kikiwa chama cha upinzani basi nacho maisha yake lazima yawe magumu, ndio maana wanafanya uhuni wowote ule wasitoke waliposhikilia.
kuhama kiongozi mmoja au wawili sio tatizo lkn ukiona kundi kubwa la viongozi linahama...lazima ushituke....chama sio imara...wapinzani wa Tanzania bado wepesi mno! nilidhani kuna chama cha upinzani chenye nguvu zaidi kingezaliwa mwaka jana 2019 lkn hakuna, vilivyopo hadi sasa ni dhaifu sana....tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu octb 2020 tukiwa na vyama dhaifu kabisaa.....ccm imejipanga kikamilifu.

2015 wengi walitoka ccm kwenda upinzani.... ccm wamepoteza majimbo mengi 2015 than ever, hivyo mkakati wao ni kuyarudisha majimbo hayo.... njia kubwa waliyoitumia ni kuweka mazingira magumu ya waliochaguliwa kufanya mikutano ya hadhara... njia hii ccm wanaijua vizuri ndio iliyowaangusha. Kuondoa bunge live... wanafahamu bunge live lilikuwa linawaweka kwenye wakati mgumu kutokaba na hoja za ufisadi na Serikali ilikuwa inachambuliwa kwa hoja nzito. Kumtuliza Tundu Lissu... huyu jamaa zile njia alizokuwa anazitumia ndio ambazo serikali zimefanya serikali kufuta bunge live.... zile press za Lissu, zilikuwa zinawachukiza wale waliopiga vita bunge live na walikuwa hawana uwezo wa kumzuia kwa vile ni haki ya kila raia kuita press kama ana jambo la kuzungumza ili mradi asivunje sheria za nchi.

Huu ni mkakati wa ccm ili warudishe majimbo waliyopoteza na kufanya majimbo yote kuwa chini ya CCM.... ili watafune vizuri rasilimali za nchi kimya kimya.

CCM OYEEEE!!
 
Suala la mtu kuhama chama Ni Jambo la kawaida,,ningekua mbowe ningehimiza wanachadema wengi kuhamia ccm wakapate ubunge,uongozi wa juu etc
 
Kuhamia ccm ni ujinga na tamaa tu ya matumbo yao kuliko Sela za vyama vyao wanazotupatia kila uchwao majukwaani,hawana pa kushika tena Wapinzani,kila walilokuwa wanalipgia kelele Magu kalifanya kama sio kuligusia,Leo wamebaki kusema Tanzania hakuna democrasia wakati wao wanaotaka hiyo Democrasia hawana Uzalendo.
Sasa magu amefanya nn kama sio kuharibu uchumi wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sometimes huwezi jua kama wanahamia kuko kiroho safi au kinafiki tu, kama mamvi & Mr zero walivyohamia upinzani kinafiki.

Bora uhai tu mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wala usihofu. Subiri mwezi wa nane utapata majibu na majawabu yote kwa pamoja. Watakapoitwa ng'ombe tena aliyekatwa mkia ndipo wataijua vizuri ccm.
 
Back
Top Bottom