Vyama vya upinzani Dodoma vyataka CDA iondoke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyama vya upinzani Dodoma vyataka CDA iondoke

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hKichaka, Apr 29, 2011.

 1. hKichaka

  hKichaka Senior Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thursday, 28 April 2011 21:04 Elizabeth Suleyman
  UMOJA wa vyama vya Upinzani Mkoa wa Dodoma, umemwandikia barua Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu( Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi ukitaka ujibiwe hoja yao ya kuondolewa kwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma(CDA) waliyodai waliitoa kwa maandishi.

  Wapinzani hao walidai CDA imewekwa kwa tamko la serikali na maslahi ya wachache, huku ikiwafanya wananchi wa mkoa huo kuishi kwa hofu ya kuporwa ardhi yao.

  Katika barua ya umoja wa wapinzani hayo kwenda kwa Lukuvi yenye kumbukumbu namba NCCR_ M/KM/DOM/05/011 ambayo alidai ilifikishwa ofisi ya Waziri jana hiyo jijini Dar es Salaam ilisema wanaomba kupata majibu ya hoja za kuondolewa kwa CDA.

  Ilisema CDA inaonekana kuwanyima uhuru na haki wananchi wa Dodoma kwa kuwa haifanyi kazi kwa ajili ya wananchi na badala yakena kwamba wananchi wanataka wahudumiwe na Manispaa yao kama ilivyo katika maeneo mengi nchini.

  Akizungumza jana na gazeti hili, Mwenyekiti wa Umoja unaovihusisha vyama vya CUF, TLP na UPDP, Kayumbo Kabutali alisema, lengo la kuandika barua hiyo ni kushinikiza, CDA iondolewe kwasababu haifanyi kazi kwa ajili ya maslahi ya wananchi bali ni ya CCM.

  "Lengo la kuandika barua hii, kwa Waziri ni kuomba CDA iondolewe haraka kwa mujibu wa sheria, kwasababu iko kwa ajili ya maslahi ya CCM na sio wananchi," alisema Kabutali na kuongeza:

  "Hivi sasa wananchi wameingiwa na hofu kubwa ya kutaka kuporwa ardhi yao kwa kuondolewa kwenye maeneo yao, kuvunjiwa nyumba bila kulipwa fidia kitendo ambacho kinawanyima haki zao kama binadamu,"alisema.

  Kabutali aliongeza kuwa, kazi zinazofanywa na Halmashauri ya Manispaa Dodoma hazina tofauti na za CDA, hivyo uwepo wake ni kutaka kuwanyonya wananchi ardhi yao yenye ekari zaidi ya 276, 910 kwa kudai kuwa wanataka kuupanua mji huo uwe mji mkuu.

  Alisema ukiangalia uwezo wa katiba ibara ya 64(5) inasema ...itakuwa nguvu ya kisheria katika Jamhuri nzima endapo sheria yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba, hivyo sheria ya kuanzisha Manispaa na CDA kwa mujibu wa katiba ya mwaka 1977, zinaonyesha kuwa zinafanya kazi zinazofanana zikijinadi zipo kisheria.

  "Kitendo cha kuwepo kwa CDA na halmashauri ni kusababisha usumbufu kwa wananchi wa Dodoma hususan masuala ya ardhi na kuwafanya kuishi maisha ya kubahatisha kwa kutofahamu ni kipi kinaendelea juu ya ardhi siku zijazo,"

  "Hivyo tunalazimika kuandika barua hii, ili kuutaarifu umma kwamba kurudi katika Katiba ya nchi ya 1977, ibara 64 (5), tutaona nani hayuko kisheria zaidi na anambana mwenzake na anafaa aondolewe,"alisisitiza.

  Alisema, baada ya kuwasilisha barua hiyo kama umoja uliamua kuazisha mtandao wa sauti ya wana wana Dodoma ambapo wamepanga kufanya maandamano Juni 16, mwaka huu baada ya kikao cha bajeti kuanza, ili kushinikiza CDA iondolewe.
   
 2. hKichaka

  hKichaka Senior Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HII ni uweli kabisa kazi za CDA haionekani..............lakini mashangingi kibao
   
 3. hKichaka

  hKichaka Senior Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani Tunamwomba CAG aende huko Dodoma akague ofisi zote za serikali nasikia ni aibu kwa ufisadi.
   
 4. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,362
  Likes Received: 3,195
  Trophy Points: 280
  Yaani mimi napendekeza hili CDA liondolewe haraka kabla hata ya kufuta vyeo vya wakuu wa mikoa na wilaya, ni kuongeza gharama za uendeshaji wakati tayari kuna manisipaa.
   
 5. N

  Nzogupata Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo CAG atasaidia nini? Ni wapi alikotumwa akaleta uozo? CAG nae ni walewale tu. Fuatilia uone mara ya mwisho alitumwa wapi na PM na akapata nini? Hata pale ambapo elimu ya uhasibu haihitajiki kwa maan ya receipt tu kutosha anakuambia hakuona ufisadi wowote. Ajabu na hata yeye anatakiwa apatikane wakum-CAG kwani naye ni tatizo tu. Atafika CDA atakutana na mkurugenzi anaishia hapo badala ya kuonana na waathirika wa mamlaka anaishia kunywa chai na lunch zao, ripoti inasema uchunguzi wetu haujabaini ubaya wowote.
   
 6. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii ni sahihi kabisa, CDA hakuna kazi wanayoifanya ikaonekana, wamejaa watu pale wengi sijui wanafanya kazi gani na magari mengi mpaka watu wa TAMISEMI wanakosa pa kupaki, vilevile kwa wanaomjua mkurugenzi wa CDA ni mtu jeuri sana na lina kiburi, kuna document zetu zipo kwake hajasign mpaka leo ukimuona ankuwa mkali na jeuri, sasa sijui yuko kwa manufaa ya nani pale...

  naunga mkono, hii mamlaka ing'olewe hakuna kazi wanayofanya
   
Loading...