Vyama vingi ni nguzo za maendeleo.


A

amakwa

Member
Joined
Jun 7, 2013
Messages
24
Likes
0
Points
0
A

amakwa

Member
Joined Jun 7, 2013
24 0 0
Wakati nakua kulikua na chama kimoja kiitwacho CCM, pale Kigoma mwaka 1994 nikiwa darasa la nne alifariki mbunge wangu aitwaye Mbano kasha jimbo hilo kuwa wazi na hapo ndipo nilipo anza kumfahamu Dr Walid Aman Kaburou. jamaa alipendwa kweli akigombea ubunge na Azim Dewji wa CCM,hapo ndipo nilipoanza kuona political movement za upinzani, kipindi hicho mji wa Kigoma ulikua na barabara za lami toka stesheni ya treni Kigoma mpaka Ujiji, njia panda Mwanga mpaka njia panda Mwandiga na lami mbovu toka stesheni mpaka TANESCO na zote hizo hazikuzidi kilometa 25 kwa ujumla wake. Lakini baada ya mkoa wa Kigoma kuanza kuonyesha upinzani hasa baada ya wabunge wengi wa mkoa huo kuwa wapinzani kwa mara ya kwanza katika maisha ya watu wa Kigoma barabara nzuri za lami toka Mwandiga mpaka Manyovu na kutoka njia panda Mwandiga mpaka Uvinza zote zina lami,kwa nini sasa sisi watu wa Kigoma tusiamini kuwa upinzani ni maendeleo ukizingatia pia kwamba kwa mara ya kwanza wananchi wa Kasulu na Kibondo wameuona umeme lupitia Machali na Mkosamali wote wa NCCR Mageuzi wakiwa pia ni wapinzani. Haya ni mawazo yangu tu jamani
 
Adharusi

Adharusi

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2012
Messages
13,157
Likes
4,642
Points
280
Adharusi

Adharusi

JF-Expert Member
Joined Jan 22, 2012
13,157 4,642 280
Haya tumekusoma
 

Forum statistics

Threads 1,274,218
Members 490,631
Posts 30,505,044