Vyama 12 upinzani vyajiunga na ccm v's cdm

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,952
Taarifa ya habari chanel Ten,sasa hivi viongozi wa vyama 12 vikiongozwa na paul kyara na lifa chipaka (Tadea).
wanalilia mgao wa ruzuku,na wanonekana kukumbwa na kiwewe cha vuguvugu la CDM la hivi karibuni.na wanaendeleza propaganda zilezile za CCM
Na wakati huo huo Wassira ameibukia mkutano wa madhehebu ya shia wimbo ukiwa ni uleule.
 
Taarifa ya habari chanel Ten,sasa hivi viongozi wa vyama 12 vikiongozwa na paul kyara na lifa chipaka (Tadea).
wanalilia mgao wa ruzuku,na wanonekana kukumbwa na kiwewe cha vuguvugu la CDM la hivi karibuni.na wanaendeleza propaganda zilezile za CCM
Na wakati huo huo Wassira ameibukia mkutano wa madhehebu ya shia wimbo ukiwa ni uleule.
Nikweli hata mie nimewaona na nikabaki na kicheko tu.....Hawa wote njaa zinawasumbua tu
 
commonmwananchi

Hao jamaa ni njaa tuuuuuuuuuu! Ukiwasikiliza wanasema huu sio wakati wa kuongea mambo ya Dowans na wanasema kwa kuwaCCM wameshinda basi waache watawale. Sijui dhana hii inatoka wapi? Endapo mtu ameshinda, AMESHINDA na kama jamii ya watanzania itaendeleza tabia hii ya kuwaacha viongozi kutawala pasipo kuwasimamia kutawala sawa na mikataba (social contract) ambayo vyama husika vimeingia na jamii, bila shaka viongozi watafanya madudu.... Mimi nadhani hao jamaa ni kwawapuuza kwa kuwa hawana jipya. But you know what, nadhani wanatumia mbinu iliyotumiwa na vyama vilivyoko bungeni baada ya kushindwa kuwa na wawakilishi kwenye serikali kivuli, vilisababisha mabadiliko ya kanuni. Bila shaka hii ndo janja yao
 
watanganyika wenzangu,walio na uchungu na taifa hili maneno hayo yawe chachu kwetu kusonga mbele kwani hii inadhihirisha ni kwa kiwango gani mishale imewaumiza adui.wakiwa bado wanatafuta dawa sisi tusonge mbele a kwa msaada wa bwana Tanganyika yetu tutaikomboa.
 
Njaa mbaya sana jamani
Narudia tena cdm wayapange matukio vizuri hawa wote watajirudi tu ila zile tetesi za hakuna upinzani tz na ni mapandikizi ya ccm ndo tunashuhudia ila nawalaumu na vyombo vyetu vya habari,kwanini wasiwa hoji vizuri hawa kuwa kwa maneno yao kweli wataitoa ccm madarakani while hilo ndo lengo namba moja la vyama? Yapo maswali mengi tu mazuri ili majibu yao yawaumbue wenyewe.okay waseme yote ila tunachotaka ni mabadiliko na ccm hawawezi kuyaleta na hiyo ni confermed maana mkuu amesema hawezi kumaliza matatizo yetu! Sina tatizo na reality ya statement hii ila kwa akili ndogo tu unaweza kuwaambia hivyo watoto wako hata kama ndo ni maskini wa kutupwa? National spirit inaweza kweli kuwa kubwa kwa statement kama hizi? Sh*t!
 
Wametumia good strategy ya kuombea ruzuku zaidi ya yote sijasikia jipya zaidi ya kujikomba kwa serikali ya ccm ili iwafanyie mpango wapate ruzuku. They are also bogas
 
kuna siku mbowe alisema kama kuna mbunge amepata ubunge akajua kazi imeisha basi amekosea kupata kwao ubunge ndiyo kwanza vita vimeanza na kwa mwendo huu, wanahakati,wanachadema tuwasapoti cdm kwa nguvu zote, maana tayari swala hili limefanywa la kidini....leo waislam wameongea mambo ya kutisha..sijui wakristu/serikali watakuja na tamko gani kujibu hoja/malalamiko ya waislamu
 
Tendwa afute hivyo vyama mara moja. Wanataka ruzuku ya nini? Waache kulalamika kama wale wa Arusha leo...
 
Tena nimeshangazwa na mahudhurio KIDUCHU ya vyama 12...,nimeona zaidi ni wabeba bendera za vyama vyao na labda hao wengine ni wapit njia waliosimama kushangaa kamera na Mzee Lifa(lofa)chipaka.
 
Taarifa ya habari chanel Ten,sasa hivi viongozi wa vyama 12 vikiongozwa na paul kyara na lifa chipaka (Tadea).
wanalilia mgao wa ruzuku,na wanonekana kukumbwa na kiwewe cha vuguvugu la CDM la hivi karibuni.na wanaendeleza propaganda zilezile za CCM
Na wakati huo huo Wassira ameibukia mkutano wa madhehebu ya shia wimbo ukiwa ni uleule.

CCM sasa imegeuka kuwa mwanaume limbukeni mwenye pesa anayedhani anaweza 'kula' kila mwanamke kwa kutumia pesa zake. ni wakati wa tadea, cuf, mende, nzi, nccr, tlp na panya wengine kuvizia mnuso ccm; na wataupata maana hali ni mbaya.
 
WanaJF,
CDM haishangai kwa kuwa hao hao ndio pia waliungana na kumwunga JK siku chache kabla ya uchaguzi. Mwenye macho haambiwi tazama.Watanzania wanawajua ni watu wa aina gani! Sioni kwanini tupoteze muda wa kuwajadili watu wasio na ajenda bali kuganga "njaa" na kutumika. Wananchi sasa wanajua kuchambua pumba na mchele.
 
Waache waendelee naona wamekubali kuwa chama tawala ni cdm vingine ni vya upinzani!
 
mwenyezi mungu awalaani vibaraka wakubwa hao wasaliti wa ukombozi asante dr slaa inabidi cdm mjenge ofisi kubwa yenye kumbi za midaharo kwa vijana itisheni harambee mtafanikiwa tu bavicha ipewe nguvu cdm ni tumaini la vijana wanyonge wasomi na waliokataa tamaa dhidi ya ufisadi mungu awape nguvu hakika mtashinda tu.
Vp kuhusu matamko ya masheikh arusha huo ndo udini wa jk na wenzake sijui anatupeleka wapi maana wakiongea cdm wachochezi sasaumetishiwa kifo wamebaki kimya na hao mawaziri vilaza pelekeni mahakamani mara moja viva cdm aluta continua
 
Kazi ya Tendwa imefail. Vyama vyote hivi ni sehemu ya sisiembe zilizosukwa kwa makusudi ya kudhoofisha upinzani. Sasa mission imefail, wananchi wamegundua janja ya C**, ndo matokeo yake kina lofa chipanya et al wanarudi nyumbani.
 
Inakatisha tamaa kujua hata uchaguzi uliopita walikuwepo kugawanya kura na kuleta picha bandia ya demokrasia.....CHADEMA songa mbele....nafikiri sasa wakati wa Mungu wa kuweka mambo wazi umefika na ndo maana tunaona ambayo hatukutegemea kuyaona...:smash:
 
watanganyika wenzangu,walio na uchungu na taifa hili maneno hayo yawe chachu kwetu kusonga mbele kwani hii inadhihirisha ni kwa kiwango gani mishale imewaumiza adui.wakiwa bado wanatafuta dawa sisi tusonge mbele a kwa msaada wa bwana Tanganyika yetu tutaikomboa.
Mama Josephine.
Nimependa hizo nilizoweka rangi nyekundu. Kila kamanda atumie huu msamiati bila ya kuuma maneno.
Wananchi wataelewa na wataunga mkono.
Tujitayarishe kusherehekea miaka 50 ya Tanganyika..tuwaache CCM waseme Tanzania bara au Tanzania.
Hata kwa hili jina la nchi CCM wanafanya usanii,kiini macho na mazingaombwe.
 
huyu Chipaka ndo boga kabisa...kutwa yuko kibarazani kwake pale sinza anapokea sh 50 /= za kuuza maji
 
Back
Top Bottom