Vyakula vyenye hadhi na mapishi yake

Vyakula vyenye hadhi na mapishi yake

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2015
Posts
28,532
Reaction score
44,760
Vyakula hupikwa ili viliwe, sio kula tu kwa kuwa una njaa na unataka ule. Kula ni kula tu sio kujaza tumbo ili ushibe. Kuna vyakula vyenye hadhi na heshima huandiliwa maalumu kwa watu maalum wanaostahili heshima. Mathalani, viongozi wakubwa, watu wenye hadhi na heshima katika jamii, nyumbani kunakuwa na chakula maalum kwa wageni na wenye hadhi katika familia. Wengine wote wataishia kula chakula kisicho na ubora wala hadhi mradi tu wajaze matumbo yao na waone wameshiba. Hebu shusheni orodha ya vyakula vyenye hadhi na heshima kwa watu maalumu wenye heshima na hadhi zao katika jamii, familia na kaya
 
Familia zingine unakuta baba anakula shatashata na watoto wanakula maji full tank
 
Vyakula vyote vina hadhi,inategemea mapishi yake,halafu kila mtu anapenda chakula fulani ambacho mwingine hakipendi.
 
Braza au sista ni msomi mambo ni mazuri ana hela akija likizo anachinjiwa kuku ale vizuri huku nyie wengine kajamba nani mtaishia kula dona bamia
 
Familia zingine unakuta baba anakula shatashata na watoto wanakula maji full tank
Haha ukipika makange ya nyama ya ng’ombe hayana michuzi. Baba atakula fresh na mboga za majani… watoto wadogo hawataweza bila mchuzi… kasheshe hapo… lazima ufanye adjustment from makange to roast..
 
Harusini ukumbi ni chini ya mti huku vijijini. Bi harusi na bwanaake wanatengewa kuku aliyeungwa vyema huko high table, nyie wengine changanyikeni mtaishia kugawiwa wali/pilau la ajabuajabu linalonuka moshi na finyango moja kama si kande au ugali kwa maharage
 
Inafuatana na ubaguzi wa wao kwa wao wa familia au taifa husika
 
Binafisi vyakula vya kigeni kama pizza na vingine havijawahi kunibamba kabisa....chukua pizza zako biriani nk mimi nipe nyama choma ya mbuzi tu basi
au mkuu wa meza hayo mavyakula yenu nitayaona takataka tu
 
Huwa napenda zile harusi/sherehe ambazo watu wote mnakula chakula kilichopikwa pamoja na kutengwa pamoja, mnapanga foleni wote kuanzia maharusi/viongozi wenye hadhi wote mnakula chakula chenye hadhi na ubora sawa. Sio wengine walishwe chakula kisicho na ubora wala heshima na maji ya kisima
 
80% ya wazazi wa kibongo wanapika vyakula ambavyo watoto wao hawavipendi ... Angalia watoto wanavyojidhalilisha kwenye shehere kisa chakula .

Hili watu waangalie sio unapika tu chakula .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom