Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 1,132
- 2,675
Katika miaka ya hivi karibuni watawala wa nchi hii wamezidi kushusha hadhi ya jeshi letu pendwa lililojijengea heshima kubwa kwa miaka mingi
Kwa miaka niliyonayo nimekua na kuona namna JWTZ wanavyoheshimika mtaani na raia wa kawaida, jinsi wenye mamlaka ya kisiasa walivyokuwa wamejitenga mbali na makamanda hawa waliojenga heshima ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu
Ilikuwa nadra sana kuwaona wakilandalanda mitaani bila shughuli maalum
Ilikuwa nadra sana kuwaona kwenye vyombo vya habari isipokuwa kwenye shughuli maalumu za kitaifa
Ilikuwa vigumu kuona wanafanya "press" na waandishi wa habari
JWTZ ilizingatia misingi na nidhamu ya kulilinda Taifa bila kulazimika kuja hadharani kupiga watu "mikwara". Hii ni kwasababu walichokifanya walikifanya baada ya kujiridhisha kinatakiwa kufanywa na kikifanyika kinaleta heshima kwa nchi
Miaka yote katika maswala ya ulinzi na usalama wa nchi hawa watu ndio walikuwa tegemeo la mwisho kuleta heshima hiyo
Hata hivyo, siku hizi imekuwa tofauti sana
Wanasiasa wamewaleta hadharani sana kiasi kwamba wao wenyewe wanaanza kujiona wakawaida sana
Hali hii ikishazoeleka na raia nao watawaona wa kawaida sana na hapo ndipo shida itakapoanzia
Raia hawatawaheshimu na wao hawatakubali kutoheshimiwa. Wale wachache watakaokataa dharau wataweka magwanda yao chini na kufanya wanalolijua wao
Naiona hatari kubwa sana huko mbele watakaokuwepo watakuwa mashuhuda
Hatari ya kuchoka kukaa maporini badala ya kukaa kwenye ofisi za kifahari;
Hatari ya kuvaa magwanda muda wote badala ya kunyonga suti na tai;
Hatari ya kukataa kutembea msituni wakila biscuit na maji badala ya kula kwenye hoteli za nyota tano bila kutoka jasho jingi;
Hatari ya kutaka heshima badala ya wao kuendelea kuheshimu na kupiga saluti muda wote,
Htari ya kutaka umaarufu na kutajwa tajwa sana kwa kusifiwa kama ilivyo kwa wengine
Hizi hatari na nyinginezo ni sehemu ya ajali itakayokuwa imesababishwa na wanasiasa waliowalazimisha JWTZ kuja hadharani kuona wao wanavyoifilisi nchi bila huruma na bila kutoka jasho badala ya kuwaacha huko huko mafichoni wakiilinda nchi kwa siri
Katika ulimwengu huu ni nani asiyependa heshima? Ni nani asiyependa mali? Ni nani asiyependa kula vinono? Ni nani anayatamani kuona hawaachi watoto wake katika hali nzuri? Ni nani asiyependa maisha ya kifahari?
Hawa watu wamefundishwa uzalendo, kufa kwa wajili ya nchi, kufa wakitetea maslahi ya nchi yao, kufa wakilinda mali za nchi dhidi ya wageni.
Wanasiasa mmeamua kuwaleta waone mnavyoitafuna nchi hii.
Mmewaleta hadharani washuhudie namna mnavyokula pasipokutoka jasho. Namna mnavyoteketeza rasilimali za nchi kwa manufaa yenu na vizazi vyenu
Hivi mnauhakika wao hawayatamani hayo maisha yenu? Mnauhakika wao hawazitamani hizo mali mnazomiliki? Mnauhakika wao watakubali kuendelea kuwalindeni tu kila siku huku wakiona namna mnavyozidi kujilimbikizia mali kwa kuuza nchi?
Kwamba wao ni maroboti hawaoni yanayoendelea? Kwamba wao kwenye mtaala wa mafunzo yao walifundishwa kumiliki mali ni dhambi na wote wakaelewa?
Chondechonde wanasiasa, waacheni hawa watu wabaki na kazi yao ya msingi. Wabaki na viapo vyao, watumikie mafunzo yao. Msiwalazimishe kufanya kitu ambacho hakikuwa sehemu ya mtaala wao itakuja kuleta taharuki kubwa sana