Vyakula vya misaada zamani na ufisadi nchini leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyakula vya misaada zamani na ufisadi nchini leo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mshiiri, Sep 4, 2008.

 1. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Misaada lazimishi
  Kipindi cha nyuma miaka ya sitini na sabini mababu zetu na baba zetu shuleni walikuwa wakila sana vyakula vya misaada kutoka Marekani. Vyakula hivyo vilikuwa vyaja kama misaada kwa ajili ya njaa ama nia ya Wamarekani na mataifa mengine hisani eti kuboresha elimu nchini. Wazazi wao walihoji na kujiuliza sana kulikoni na hofu yao ilikuwa ikiwa vyakula vile havina madhara "in the long run".

  Mgawanyo
  Si sehemu zote nchini walipata mgawanyo wa vyakula hivi mfano maeneo ya kina Mhe. Dr. Slaa nk. Maeneo mengine kama mkoa wa Kilimanjaro hivi sasa almost eneo lote walipata mgao huu.

  Viongozi fisadi
  Viongozi wote ambao ni mafisadi wasiojali maslahi ya nchi na wakiwa kama Carl Peters katika kutengeneza mikataba ya nchi na waliopindishwa fikra kutokana na kula vyakula hivi wamegeuka kuwa mafisadi wa kutupa. Ushahidi ni kuwa hata wakijiuliza wenyewe je nimekula vyakula hivi watapata jibu ni ndiyo. Akili zao zimefanywa kama mtu ajikatae nyama ya tako na kuila yaani kuila nyama yake mwenyewe au mtu aibaye fedha zake mwenyewe. Hii ndi side effects za kula vyakula vile miaka ya sitini na sabini. Hawa jamaa huwa na long term plan na sasa kila kitu kitakuwa rahisi kwao RE-COLONISATION of Africa in the new era ambayo watu wameeelimika na bado hawajui kulinda na kutambua mali zao na haki zao.

  Madhara
  Madahara ya vyakula hivyo yako wazi kwani viongozi wote fisadi kwa sasa walisoma kipindi hicho na walikula sana vyakula hivyo kwani familia zao zilikuwa masikini sana na pia uelewa wa familia kuhusu adhari zake ulikuwa finyu. Hawa ni wale waliosoma kuanzia middle school hadi primary miaka ya mwanzo kabisa sabini. Hii ndio cadre iliyoko madarakani hivi sasa. Uelewa wa hiki kizazi ni tofauti kabisa na hiki kinachomaliza vyuo vikuu hivi sasa has waliosoma hapa nchini UDSM, SUA nk. Bahati mbaya sana baada ya kula vyakula hivyo walipewa nafasi za kuangaliwa kama the dose was effective wakasomeshwa nje UK, Sweden, Marekani nk. They were confirmed to have taken effective dose. Ndiyo maan utaalaamu wao haukuisaidia nchi kwani kwa wahandisi hata madaraja hujengwa na wachina hadi leo nk. Mifano nim mingi lakini hiki kizazi ni bure kabisa.

  1. Kufanya solid decision kwa manufaa ya Taifa
  Inakuwa haiwezekani kwani hii vocabulary haipo after the brainwashing as a result of hivi vyakula.

  2. Ufisadi
  Ufisadi ni product ya brainwashing effect ya vyakula hivi, kwani humfanya mtu kuwa mbinafsi kuliko kawaida na kuondoa dhana kabisa ya Ujamaa akilini mwake. Ni kama tusikiavyo wala unga kuna wakati hujisikia yuko New York kumbe amejinyea na yuko pembeni ya barabara magari yakimkwepa.

  3. Kupoteza mapenzi na nchi
  Kwa kuwa dhana ni umimi basi usisi haupo. Hapa wadanganyika wako upande mmoja na wao wako upande mwingine wakinyonya kwa mrija damu za waTanzania. Mathalani vile vyakula vilikuwa na vinasaba (genes) za kikoloni. Kwa malengo kuwa kama hawangerudi kutawala Africa tena basi wachache wao wataokuwa wamekula vyakula hivyo watatawala wengine na kutuuzia kwa bei ya kutupa rasilimali zao anma kutuita tukazichukue.

  4. Ubunifu kwa maendeleo
  Ubunifu hauwezi kufanywa na sasa watu hawa ambao wametaahirishwa au kupumbazwa hivyo whatever centuries from where we left their dark continent they will stand still in terms of development or they will develop with very very slow pace since their creativity is diminished or washed away. Na ndio matokeo tuonayo miaka 47 tangu Uhuru lakini hata malaria imekuwa tabu kupunguzwa kasi lich ya kutokomezwa. Mfano hapa walijua DDT ikipulizwa juu ya bara la Africa itaondowa na kutokomeza kabisa malaria ingawa itakuwa na adhari kimazingira lakini haziwezi ku-outweigh adhari za malari in the long run. Wakaunda conventions za kizushi kuwa DDT isitumike na kwa kuwa waliokuwa katika mikutano hii na suti nyeusi na wameshakuwa brain washed wakakubali na matoke yake its a shame damn thing. Anyway vingi mtu ataweza sasa kufikiri why they are YES YES men when it comes to international thinking leave alone national thinking especially when comfronted with SMART WHITE GUYS coming with no dollars and leave with thousand of tonnes of dollar bills/notes.

  Kudhamini wazungu
  Kwa rika hili la viongozi hudhamini sana wazungu na vitu vyao, baa zao, club zao, hotel zao, magari yao, nyumba zao, utajiri wao, na hata wengine huthubutu kusema vitu vyote vizuri ni vya kizungu hata inzi wakubwa sana wa bluu ni wa kizungu, na hata kuku wakubwa weupe ni wa kizungu na awapo na mazungumzo na mzungu ndio hizo effect huwa zinajimanifest to the maximum kwani ni kwa kinasaba sasa. Induced genetic attractions na hivyo wafanyapo makubaliano ya mikataba hawa viongozi wetu na wazungu akilini huwaza mali ni za wazungu hivyo kuogopa kuwejka interest ya watanzania. This is shame but tunakula matunda ya umaskini wetu na kupenda dezo yaani vya bure.

  Ushahidi
  Wale viongozi wote na raia wote wenye mapenzi na nchi hii hawakula vyakula hivyo na fikra zao pia hazikuadhirika na matokeo yake ndio waliobaki kubwata kwa manufaa ya Watanzania wote na sio wadanganyika mfano Waheshimiwa: Dr. Slaa, Zito Kabwe, Samwel Sitta, Dr. Harrison Mwakyembe, Warioba, C. D. Msuya, Mark Bomani, J.K. Nyerere, M. R. Kawawa, E. M. Sokoine, na wanaofanana na hao katika utendaji wao. Mungu awaweke malali pema peponi waliotutangulia mbele ya haki. Hata madawa mengi yaletwayo nchini na vifaa viletwavyo au vyakula ni vile vilivyokwisha muda wake ama vimekaribia kuisha muda wake na kabla ya kuwa na vifaa vya kisasa kwa wachache waliokuwa hawajaathirika na vyakula hivyo kufanya shauri hilo watanzania wengi tumekula vitu visofaa kwa binadamu.
  To be updated.......
   
  Last edited by a moderator: Sep 18, 2008
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Sep 11, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Interesting!

  Mzee wangu, hata mimi nilikula chakula hicho unachokiongelea wakati nikiwa Middle School. Pale shuleni kwetu kilikuwa kikiitwa mabuluga, wala sijui neno hilo lilikuwa na maana gani ingawa huwa nadhani lilitokana na chakula hicho kuwa Vulgar, lakini mimi siyo fisadi kabisa mzee wangu.
   
 3. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2008
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,507
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  "Mzee yawezekana hujapata nafasi ya kufisadi" Joke
   
 4. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  This is important to base our argument why viongozi wetu ni mbumbumbu kiasi hiki
   
Loading...