Chinga One
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 11,471
- 12,373
Wadau kuna habari zinasambaa kwa kasi sana mitandaoni kwamba sukari imeanza kupanda bei kutoka 2000 mpaka 2500...huku niliko sasa hivi inauzwa 2300 kutoka 2100.
Habarini za asb ndugu zangu. Natumai kwa uweza wa Mungu mmeamshwa salama. Nasi huku hatujambo.
Niombe kuwasisitiza ndugu zangu tununue sukari tuweke akiba. Maana kuna uwezekano sukari ikaadimika madukani mpaka mwezi wa sita au wa saba. Tangu Ijumaa Kiwanda wa Sukari cha TPC kimesitisha uzalishaji. Na sukari imeshaanza kupanda bei. Nimewasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Moshi akanimbia hali ya Upatikanaji wa sukari hautakuwa mzuri. Ni mpaka miezi hiyo niliyotaja. Ila wanapambana kuwajua watu wanaochochea upandaji wa Bei.
Ni hilo tu. Siku njema"""""
HII NI MOJA YA MESEJI ILIYONUKULIWA KUTOKA MAHALI FULANI,MTUMAJI WA HIYO TAARIFA TUNA MUHIFADHI KWA SASA.
tunaomba wajuzi wa mambo ya sukari mtupe taarifa kamili maana hali hii inataleta sintofahamu kwa wananchi.kama nikweli basi pia tunaomba serikali iingilie kati swala hili ili maisha yasizidi kua magumu na ukizingatia mwezi mtukufu wa ramadhani uko karibu.
=====
Dar/Mikoani. Bei za vyakula katika baadhi ya masoko nchini zimepanda na kusababisha hali ya maisha kuwa ngumu.
Uchunguzi uliofanywa kwenye baadhi ya masoko jana na juzi umebaini kuwa bidhaa mbalimbali zimepanda bei yakiwamo maharage ambayo yamepanda kutoka Sh 1800 hadi 2700 na 3000 kwa kilo.
Pia Sukari imepanda kutoka bei elekezi iliyotolewa na Serikali ya Sh1800 hadi Sh 2500, Mchele kutoka Sh 1200 hadi 2600 kwa kilo.
Unga wa sembe nao umepanda kutoka Sh1200 hadi Sh 2000. Bidhaa nyingine zilizopanda ni mboga za majani ambapo fungu la mchicha, chainizi, tembele limepanda kutoka Sh200 hadi Sh400 na Sh 500.
Nyanya ambazo mwaka jana, ziliuzwa kwa bei nafuu hadi kufikia Sh 1500 kwa sadolini, msimu huu zimepanda ambapo nyanya moja inauzwa kwa Sh 200 hadi 300 kutoka Sh200 nyanya tatu au nne.
Akizungumzia bei za vyakula kupanda, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema suala hilo liko kisayansi linalohitaji taarifa sahihi na hivyo asingeweza kutoa majibu bila kukusanya taarifa hizo.
Chanzo: Mwananchi