inaonekana kali sana. Sisikii yale makelele ya kina Ray et al, yanayofuatiwaga na midundo ya kushtusha. Bongo tukiwa na quality hii tutafika mbali sana.
Imegharimu dola 200,000 sawa na zaidi ya Tsh 400,000,000 na imechukua miaka minne kuikamilisha.
Vita Nikuvute Imeshinda tuzo tatu kimataifa za kule Seattle USA, Burkina Faso 🇧🇫 na Rwanda.
Imeleta mapinduzi katika sekta ya filamu za Bongo Tanzania na kimataifa
Bajeti ya sinema hii imechangiwa na wafadhili mbalimbali wa kimataifa. Adam Shafi mtunzi wa kitabu Kuli ndiyo aliyewavutia waandaaji wa sinema hii kwani uandishi wake umerahishisha kazi kwa kuwa kitabu cha Kulu ni kama simulizi ya movie. Pia shukrani zimeenda kwa Mkuki na Nyota wachapishaji wenye hati miliki ya kitabu Kuli ambao hawakusita kutoa ushirikiano kama wadau.