Mtaka Haki
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 492
- 149
Kitendo cha mtoto wa miaka 14 kukojolea kitabu cha kurani hakiwezi kuungwa mkono na mtu yeyote.
Kila mmoja atatarajia KARIPIO na kemeo na hata ikibidi adhabu kwa mtoto huyo.
Kama kitendo cha kiovu cha mtoto wa miaka 14 kinapaswa kukaripiwa kwa nguvu. Basi kitendo cha watu wazima wakiwemo viongozi wa dini kuhamasisha uovu na unajisi wa kuharibu na hata kuingia isivyo kwa halali na kuchoma madhabahu takatifu kinapaswa kikemewe na kukomeshwa kwa nguvu kubwa zaidi.
Nitumie nafasi hii kuwashukuru sana viongozi wa dini ya Kikristo kwa kitendo chao cha uvumilivu na upole hata sasa. Huu ndio mfano wa kuigwa. Nimpongeze pia Sheikh mkuu wa Dar es salaam Alhaji Musa Salum kwa maneno ya busara na hekima katika kuzuia jazba. Anapaswa kuigwa kwa kuonyesha busara na hekima.
Hata kama angekuwa ni Askofu aliyefanya kitendo hicho bado hekima inadai akamatwe Askofu huyo na kuulizwa kilichompelekea kufanya alichofanya. Kwa sababu ni wazi kuwa vurugu huzaa vurugu. Kwa wengine kuchomewa gari ni kitendo kinachouma kwao kuliko hata kuchomwa Biblia. Hivyo anaweza kushawishika bila kusukumwa na yeyote kulipiza kisasi.
Matendo yanayotokea katika nchi hupima hekima na busara za watu mbalimbali. Ukweli ni kuwa waislamu walioingia katika makanisa na kuharibu kwa sababu iwayo yoyote wanapaswa kukemewa hasa na waislamu wenzao. Huu ndio wakati busara ya kila muislamu inapaswa kutumika badala ya kunyamaza kimya na hata kujaribu kukemea pande mbili ambazo kila mtu anajua wazi kuwa hazipo.
Waislamu wenye busara wasipojitokeza kwa wingi kupinga VURUGU hizi kuna mbegu itakuwa inapandwa ambayo matokeo yake yatazaa uovu mbaya Tanzania.
Kama ni halali kulipiza kisasi kwa nini haitarajiwi viongozi wakristo wahamasishe watu wao kubomoa misikiti? Hasa ukizingatia kweli kuwa wameharibu makanisa na kuchoma mali mbalimbali kama waislamu waliotokea msikitini, Je ni kweli wanaogopwa? Rais Ali Hassan Mwinyi aliwahi kuonya suala la kujibu mapigo kwa waliofanya bila busara. Alisema "Akitokea kichaa akachukua nguo zako ukioga, kisha ukamkimbiza uchi, ni nani atakayeonekana kichaa?" Kikundi cha wahuni hawa kinapandisha sifa ya dini ya kikristo na kuudhalilisha uislamu. Waislamu wa kweli wanapaswa wasinyamazie jambo hili.
MAMBO YA MUHIMU NA YA KUZINGATIWA KWA HARAKA:
Nimeongea na kiongozi mmoja wa dini na akasema yafuatayo:-
Waislamu wachache wenye nia mbaya na wanaofadhiliwa na makundi fulani wanataka kuchafua jina la dini ya kiislamu ionekane hovyo na ya wasio na hekima, wasio na subira, wakatili nk.
Aliniambia kuwa tukio hilo limepangwa na kikundi hicho. Wanapanga wachache halafu wanawaingiza wengine ili kutimiza makusudi yao. Anasema mtoto aliyekuwa anajibizana na mwenzake alitumwa na kundi hilo.
Alitoa mifano mingi ya jinsi kundi hilo linalofadhiliwa na kikundi toka nje linavyojaribu kutengeneza matatizo Tanzania. Kijana aliyekuwa akifanya ubishi alitumwa amwambie huyo mtoto hivyo, huku kila mtu akijua matokeo yake na malengo yake.
ANGALIENI MFANO WA ABUNUWASI USIWAPATE VIONGOZI:
Kuna hadithi ya Abunuwasi alikutana na vijana, "Akawaambia nyie wakorofi nyie. Msije mkaenda nyumbani kwangu mkakuta ufunguo pale juu ya mlango, mkauchukua mkafungua mlango, mkala chakula kilichoko juu ya meza kisha mkafunika bakuli na kuondoka."
WALE VIJANA WALIJUA WAMEAGIZWA LA KUFANYA
Na ni kweli alikuwa akitaka wafanye hivyo. Alilenga kushtaki kuwa nzi wamekula chakula chake kwa kuwa alikiacha na amekuta nzi. Mfalme alipelekewa kesi ile na yeye bila kujua akampa mamlaka ya kuua nzi kokote atakakoonekana. Kumbe mlengwa alikuwa ni mfalme mwenyewe. Hatimaye alisubiri nzi aliyetuwa juu ya kichwa cha mfalme na kwa kutumia rungu ile ile aliyokabidhiwa na mfalme alimuua mfalme akidai anaua nzi. Waislamu wapenda amani na viongozi wa siasa hamtakuwa salama mambo haya yanayokusudiwa yakiachwa yaendelee.
Kijana aliyejibizana na mwenzake aisaide polisi katika hili ninalolisema. Waliomtuma malengo yao yakitimia hata viongozi wa leo hamtakuwa salama.
Kiongozi wa dini niliyeongea naye alinipa mifano ifuatayo juu ya kila njia wanayotafuta waislamu wachache ambao hata kuwaita waislamu ni kuutukana uislamu. Uislamu ni kuwa mtiifu kwa Mungu. Kiongozi huyo alisema wamekuwa wakienda makanisani kudai wameokoka na wanaomba vitu vya kichawi walivyokuwa wanatumia vichomwe. Kumbe wanaweka Kurani tukufu ndani yake. Kisa ikichomwa ionekane kuwa wakristo wamechoma. Waliovunja mabucha ya nguruwe walimtuma mtoto akanunue nyama ya nguruwe. Kisha wakaanza kuhimizana na kuanza vurugu walizokuwa wamepanga.
Nchi za kiislamu zimekuwa zikivipiga vita vikundi hivi vya kihuni na kuvinyamazisha kwa sababu wanajua madhara yake. Bahati nzuri tuna raisi muislamu. Huu ni wakati muafaka wa kuwang'oa bila woga wowote. Nina hakika wanajulikana na hata wafadhili wao wanajulikana.
Viongozi wa siasa msiposema haya leo kwa nguvu hata baadae itawashinda. Msiogope kusimamia ukweli ilio wazi. Waislamu walioko kwenye vyama vya siasa wakemee kwa nguvu zote. IGP ni muislamu kamanda wa kanda maalum ni muislamu.
Taarifa hizi msipozifanyia kazi wakristo wanaweza kutokuwasikiliza viongozi wao na kuamua kulipiza kisasi. Kwa serikali isiyo na dini inapaswa kuona kuwa gari kwa wengine lina thamani kuliko Biblia au Kurani.
Huu ndio wakati wa kutumia intelgensia ya kweli kubaini yanayosemwa hapa.
Baba wa taifa Mwl. Nyerere alikuwa mkristo lakini alizima kwa nguvu zote na kwa haki chokochoko zenye kugawa taifa.
Watu wasipojiridhisha kuwa haki inatendeka kuna siku watachukua sheria mikononi na wengi wataathirika wakiwemo wanaonyamazia maovu sasa.
Namuomba raisi akemee bila kuwa na sababu ya kuongea kama kuna pande mbili katika jambo hili. IGP huu ndio wakati muafaka wa kutumia inteljensia ili waislamu wote waelewe kuwa wanapochochewa kinachotafutwa sio kutetea dini wala kitabu.
Zanzibar walichoma makanisa hakuna aliyekuwa amewachokoza.
Naomba wakristo wasichangie hoja hii. Wawepo waislamu wenye busara wachangie na kueleza mbinu za kuondoa chuki inayopandwa bila sababu ya msingi.
Wahuni hawa wanawafanya viongozi wa Kikristo kupata sifa na mfano kwa jamii huku watu wengine wakiwabeza baadhi ya viongozi wa kiislamu juu ya matumizi ya jazba badala ya busara.
Tuweke busara zetu hapa waaibike wanaodhania busara ni kidogo.