Vurugu za Mbagala ni zaidi ya mnachokifahamu - Oh Tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vurugu za Mbagala ni zaidi ya mnachokifahamu - Oh Tanzania!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtaka Haki, Oct 15, 2012.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kitendo cha mtoto wa miaka 14 kukojolea kitabu cha kurani hakiwezi kuungwa mkono na mtu yeyote.

  Kila mmoja atatarajia KARIPIO na kemeo na hata ikibidi adhabu kwa mtoto huyo.

  Kama kitendo cha kiovu cha mtoto wa miaka 14 kinapaswa kukaripiwa kwa nguvu. Basi kitendo cha watu wazima wakiwemo viongozi wa dini kuhamasisha uovu na unajisi wa kuharibu na hata kuingia isivyo kwa halali na kuchoma madhabahu takatifu kinapaswa kikemewe na kukomeshwa kwa nguvu kubwa zaidi.

  Nitumie nafasi hii kuwashukuru sana viongozi wa dini ya Kikristo kwa kitendo chao cha uvumilivu na upole hata sasa. Huu ndio mfano wa kuigwa. Nimpongeze pia Sheikh mkuu wa Dar es salaam Alhaji Musa Salum kwa maneno ya busara na hekima katika kuzuia jazba. Anapaswa kuigwa kwa kuonyesha busara na hekima.

  Hata kama angekuwa ni Askofu aliyefanya kitendo hicho bado hekima inadai akamatwe Askofu huyo na kuulizwa kilichompelekea kufanya alichofanya. Kwa sababu ni wazi kuwa vurugu huzaa vurugu. Kwa wengine kuchomewa gari ni kitendo kinachouma kwao kuliko hata kuchomwa Biblia. Hivyo anaweza kushawishika bila kusukumwa na yeyote kulipiza kisasi.

  Matendo yanayotokea katika nchi hupima hekima na busara za watu mbalimbali. Ukweli ni kuwa waislamu walioingia katika makanisa na kuharibu kwa sababu iwayo yoyote wanapaswa kukemewa hasa na waislamu wenzao. Huu ndio wakati busara ya kila muislamu inapaswa kutumika badala ya kunyamaza kimya na hata kujaribu kukemea pande mbili ambazo kila mtu anajua wazi kuwa hazipo.

  Waislamu wenye busara wasipojitokeza kwa wingi kupinga VURUGU hizi kuna mbegu itakuwa inapandwa ambayo matokeo yake yatazaa uovu mbaya Tanzania.

  Kama ni halali kulipiza kisasi kwa nini haitarajiwi viongozi wakristo wahamasishe watu wao kubomoa misikiti? Hasa ukizingatia kweli kuwa wameharibu makanisa na kuchoma mali mbalimbali kama waislamu waliotokea msikitini, Je ni kweli wanaogopwa? Rais Ali Hassan Mwinyi aliwahi kuonya suala la kujibu mapigo kwa waliofanya bila busara. Alisema "Akitokea kichaa akachukua nguo zako ukioga, kisha ukamkimbiza uchi, ni nani atakayeonekana kichaa?" Kikundi cha wahuni hawa kinapandisha sifa ya dini ya kikristo na kuudhalilisha uislamu. Waislamu wa kweli wanapaswa wasinyamazie jambo hili.

  MAMBO YA MUHIMU NA YA KUZINGATIWA KWA HARAKA:

  Nimeongea na kiongozi mmoja wa dini na akasema yafuatayo:-

  Waislamu wachache wenye nia mbaya na wanaofadhiliwa na makundi fulani wanataka kuchafua jina la dini ya kiislamu ionekane hovyo na ya wasio na hekima, wasio na subira, wakatili nk.

  Aliniambia kuwa tukio hilo limepangwa na kikundi hicho. Wanapanga wachache halafu wanawaingiza wengine ili kutimiza makusudi yao. Anasema mtoto aliyekuwa anajibizana na mwenzake alitumwa na kundi hilo.

  Alitoa mifano mingi ya jinsi kundi hilo linalofadhiliwa na kikundi toka nje linavyojaribu kutengeneza matatizo Tanzania. Kijana aliyekuwa akifanya ubishi alitumwa amwambie huyo mtoto hivyo, huku kila mtu akijua matokeo yake na malengo yake.

  ANGALIENI MFANO WA ABUNUWASI USIWAPATE VIONGOZI:
  Kuna hadithi ya Abunuwasi alikutana na vijana, "Akawaambia nyie wakorofi nyie. Msije mkaenda nyumbani kwangu mkakuta ufunguo pale juu ya mlango, mkauchukua mkafungua mlango, mkala chakula kilichoko juu ya meza kisha mkafunika bakuli na kuondoka."

  WALE VIJANA WALIJUA WAMEAGIZWA LA KUFANYA
  Na ni kweli alikuwa akitaka wafanye hivyo. Alilenga kushtaki kuwa nzi wamekula chakula chake kwa kuwa alikiacha na amekuta nzi. Mfalme alipelekewa kesi ile na yeye bila kujua akampa mamlaka ya kuua nzi kokote atakakoonekana. Kumbe mlengwa alikuwa ni mfalme mwenyewe. Hatimaye alisubiri nzi aliyetuwa juu ya kichwa cha mfalme na kwa kutumia rungu ile ile aliyokabidhiwa na mfalme alimuua mfalme akidai anaua nzi. Waislamu wapenda amani na viongozi wa siasa hamtakuwa salama mambo haya yanayokusudiwa yakiachwa yaendelee.

  Kijana aliyejibizana na mwenzake aisaide polisi katika hili ninalolisema. Waliomtuma malengo yao yakitimia hata viongozi wa leo hamtakuwa salama.

  Kiongozi wa dini niliyeongea naye alinipa mifano ifuatayo juu ya kila njia wanayotafuta waislamu wachache ambao hata kuwaita waislamu ni kuutukana uislamu. Uislamu ni kuwa mtiifu kwa Mungu. Kiongozi huyo alisema wamekuwa wakienda makanisani kudai wameokoka na wanaomba vitu vya kichawi walivyokuwa wanatumia vichomwe. Kumbe wanaweka Kurani tukufu ndani yake. Kisa ikichomwa ionekane kuwa wakristo wamechoma. Waliovunja mabucha ya nguruwe walimtuma mtoto akanunue nyama ya nguruwe. Kisha wakaanza kuhimizana na kuanza vurugu walizokuwa wamepanga.

  Nchi za kiislamu zimekuwa zikivipiga vita vikundi hivi vya kihuni na kuvinyamazisha kwa sababu wanajua madhara yake. Bahati nzuri tuna raisi muislamu. Huu ni wakati muafaka wa kuwang'oa bila woga wowote. Nina hakika wanajulikana na hata wafadhili wao wanajulikana.

  Viongozi wa siasa msiposema haya leo kwa nguvu hata baadae itawashinda. Msiogope kusimamia ukweli ilio wazi. Waislamu walioko kwenye vyama vya siasa wakemee kwa nguvu zote. IGP ni muislamu kamanda wa kanda maalum ni muislamu.

  Taarifa hizi msipozifanyia kazi wakristo wanaweza kutokuwasikiliza viongozi wao na kuamua kulipiza kisasi. Kwa serikali isiyo na dini inapaswa kuona kuwa gari kwa wengine lina thamani kuliko Biblia au Kurani.

  Huu ndio wakati wa kutumia intelgensia ya kweli kubaini yanayosemwa hapa.

  Baba wa taifa Mwl. Nyerere alikuwa mkristo lakini alizima kwa nguvu zote na kwa haki chokochoko zenye kugawa taifa.

  Watu wasipojiridhisha kuwa haki inatendeka kuna siku watachukua sheria mikononi na wengi wataathirika wakiwemo wanaonyamazia maovu sasa.

  Namuomba raisi akemee bila kuwa na sababu ya kuongea kama kuna pande mbili katika jambo hili. IGP huu ndio wakati muafaka wa kutumia inteljensia ili waislamu wote waelewe kuwa wanapochochewa kinachotafutwa sio kutetea dini wala kitabu.

  Zanzibar walichoma makanisa hakuna aliyekuwa amewachokoza.

  Naomba wakristo wasichangie hoja hii. Wawepo waislamu wenye busara wachangie na kueleza mbinu za kuondoa chuki inayopandwa bila sababu ya msingi.

  Wahuni hawa wanawafanya viongozi wa Kikristo kupata sifa na mfano kwa jamii huku watu wengine wakiwabeza baadhi ya viongozi wa kiislamu juu ya matumizi ya jazba badala ya busara.

  Tuweke busara zetu hapa waaibike wanaodhania busara ni kidogo.
   
 2. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kidogo wewe nimekuelewa hujataka kumlaumu mtu,kikundi, au dini fulani bali unaonekana unania ya dhati katika kutafuta hitimisho sahihi la masuala kama haya...
   
 3. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante Mkuu
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Jichambueni, mtoe pumba katika mchele. Vinginevyo sifa ya uislamu itaharibika.
   
 5. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  udini udini udini whta is next...
   
 6. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukweli ni kwamba wakorofi ni wachache sana ila mbinu wanazotumia zinawaogopesha wenye busara kusema. Pia mbinu hizo zinawaingiza wasiojua lolote kwenye mtego na jazba.
   
 7. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwakweli haya mambo ya kulipuka lipuka hayana tija ni uhuni uliokithiri, wa TZ hatuko hivyo na hiki kichaa sijui tumekipata wapi?
  Inasikitisha mno kuona vitu kama hivyo. Jambo la kumuelimisha mtoto kuwa si busara kuchezea kitabu cha mungu sasa watu tunakuwa kama vichaa.

  Mungu apishe mbali kabisa ujinga huu.
   
 8. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Vyombo vya habari na waislam tayari wameshamuhukumu Dogo!! Dogo ni mtuhumiwa,pia dogo alishawishiwa na dogo wa kiislam. Dogo kwangu mimi ni HERO kama malala.
   
 9. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MADA HII moja ya malengo yake ni kuwaomba waislamu wafanye utafiti na kisha kutoa matamko.
   
 10. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kuna jamaa yangu huwa anasema uislamu ni dini ya amani lkn tangu jambo hilo litokee amekua mnyonge saaana hata chai haji kunywa nami hapa ofisini anakaa tu peke yake anatafakari nilipomfuata leo aliniambia najisikia aibu kwa kuwa na imani moja na wendawazimu walochoma makanisa sijui hata nifanye nini ila ameniambia jumapili ijayo nimpitie twende kanisani maana ndipo kwenye upendo na mungu mwenye sifa nzuri!!!
   
 11. m

  mamajack JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  wakati wa kuvuna kilichopandwa na kina mkama 2010.walidhani mbegu walizopanda hazikuota.hatia iko juu yao.
   
 12. M

  Mch Kasimbazi Member

  #12
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya ni maneno ya busara. Ingawa mimi ni mkristo nafikiri mleta mada anayo nia ya dhati ya kutafuta suluhisho. Wito kwa wakristo na viongozi wao tusikubali kuwa provoked au kuingiizwa katika mtego wa kundi hili.

  Mfano kuna mchungaji alinielelza binti mmoja aliyekwenda katika mkutano wake Bukoba na kutoka mbele ili kutubu na kumpokea Yesu. Baada ya hapo akamwambia mimi ni binti wa kiislamu nimeamua kuokoka ila nilikuwa na kitabu hiki (akamwonyesha Koran) je sasa nikifanyeje maana sikihitaji tena. Yule mchungaji akamwambia (baada ya kuona mtego) nadhani ukitunze utakuwa unalinganisha mafundisho tunayokupa toka Biblia na aya za Kurani ili ubaine tofauti iliyomo.

  Hii ilikuwa busara vinginevyo yangekuwa mengine!!
   
 13. t

  tlc trans Member

  #13
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bravo mleta mada, asante kwa mwongozo mzuri, naamini waislamu wanaona walichokifanya na matokeo yake pia watayaona!
   
 14. M

  MKUU WA KAYA JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 201
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimekukubali jamaa yangu una busara sana tena ulifaa kuwa kiongozi wa hiyo dini.Mimi nilisema jana huyo mtoto wa kiislamu aliyemshawishi mwenzekae lazima atakuwa ametumwa tu.Mazingira yote yanaonyesha hivyo
   
 15. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Bravo, bonge la uzi. Umeua zaidi na ule mfano wa Abunuasi. Ni kweli waislam wenye busara ndo wenye nguvu ya kurekebisha kuokoa hadhi ya uislam vinginevyo sisi Wafuasi wa Kristo hatuna uwezo wa kuwatenganisha zaidi tutaowajudge kuwa wote ni walewale wa kuogopwa.
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kwasasa chakufanya makanisa tuweke walinzi na tukimuona mtu ambaye haeleweki anakuja tena na mawe nikumfyatua kiuno tuuu, makanisa yalindwe kwa silaha tena kali!
   
 17. peri

  peri JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mkuu mimi ni muislam.
  Umejaribu kutoa ufafanuzi mpana, kusema kweli hakuna muislam anaependa kuona machafuko katika nchi yetu na suala la uchomaji wa makanisa ni kunyume kabisa na mafundisho ya uislam.

  Hao waliofanya hivyo vitendo ni wahuni na kamwe uislam haukuwatuma wala haukufundisha hivyo.

  Tusiwajumuishe waislam wote kwenye hau uhuni kama ambavyo hatupaswa kuwajumuisha wakristo wote kwenye kitendo cha kijinga alichokifanya yule mtoto.

  Kuhusu suala la kikundi cha wahuni kinacho fadhiliwa sitaki kuzipinga au kuzisadiki hizo habari.

  Nashauri wenye taarifa wazitoe kwenye vyombo vya dola vizifanyie kazi au wazitoe kwa vyombo vya habari ili wafanye uchunguzi.

  Tanzania ni yetu sote, tusikubali kupoteza amani na utulivu tulionao katika jamii yetu.
   
 18. MGANGA WA KIENYEJI

  MGANGA WA KIENYEJI JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  JINSI ULIVYO ANZA TU MAKALA YAKO, NI USHAHIDI KUA WEWE NI WAKALA WA SHETANI. Unataka kupandikiza hisia kua kuna watu wamebakwa na kunajisiwa. Kwa taarifa yako that is ANTI-ISLAMIC. WE MUSLIMS NEVER DO SUCH THINGS. LAKINI NI KAWAIDA YENU KUWACHOKOZA WAISILAMU HALAFU NA KUANZA KULIA LIA. MNAJAZWA CHUKI MAKANISANI KWENU MPAKA MNA WAHARIBU NA WATOTO WENU.

  HEBU NITAJIE, NI KIJANA GANI AU MUISLAMU GANI, ULIWAHI KUMSIKIA AKI MKASHIFU YESU AU KUCHANA KITABU CHA BIBLIA.

  WAISLAMU WANAJADILI KWA HOJA NA SIO KASHFA AU MATUSI AU UCHOKOZI.

  HAKUNA MWIZI ANAEPIGANA WAKATI AKIFUKUZWA KWA SABABU DHAMIRA INA MSUTA. NDIO MAANA MNAPO TUCHOKOZA, MNATAHAYARI NA KULIA LIA TU.

  HATA WAKIRSTO WENYE NIA NZURI, WAMEUNGANA NA SISI KULAANI KITENDO KILE.

  BADALA YA KUHUBIRI DINI KATIKA MAKANISA YENU MNAHUBIRI CHUKI NA IBADA ZA MASHETANI. SIKU HIZI WACHUNGAJI WOTE WAMEKUA WAGANGA.

  WAISLAMU HAWANA CHUKI NA WAKIRSTO AU WASIO KUA NA DINI WASIO WABUGUDHI WAISLAMU.


  ISLAM IS A RELIGION OF PEACE. BUT IT DEFENDS ITSELF WHEN IT IS ATTACKED. WE MUSLIMS, NEVER TURN THE OTHER CHICK. BE WARNED.
   
 19. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,749
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Mungu baba,mwana na roho Mtakatifu zidi kutujalia hekima!! hilo tu.
   
 20. m

  mr.sylvestre JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 253
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 80
  Kwa upande wangu mi siwezi kulaumu kwa walichokifanya hawa ndugu zetu waislam kwani dini yao inaruhusu kupigana na kupambana kwa namna yoyote ile pindi pale inapoonekana dini yao imechafuliwa.

  USHAURI:
  Ningependa kuwa shauri wakristo wote waendelee na moyo wao wa uvumilivu na unyenyekevu kama ilivyo kawaida yao na pia wawakanye watoto kuchezea imani za wengine.

  HITIMISHO:
  Tukio hili dalili tosha kabisa inayoashiria machafuko zaidi ya kidini huko mbele katika nchi yetu na hii inasababishwa na vuguvugu la chini chini lililopo hapa nchini dhidi ya wakristo. Ilianza MoU, OIC, KADHI, Sensa kwa kigezo cha dini na sasa uchomaji wa makanisa na mengi zaidi yanakuja ,Wakristo muwe wavumilivu.
   
Loading...