Vurugu mechi ya Stand United na JKT Kanembo

Pukudu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
3,148
2,219
Leo kwenye uwanja Wa Kambarage kulikuwa na mechi ya Daraja la kwanza kati ya Stand Utd ya Shinyanga inayoongoza kundi kwa point 13 dhidi ya Kanembo Jkt ya Kigoma yenye point 12. Vurugu zimetokeoa baada ya refa kutoa penalt dakika za mwisho baada ya mabeki wa Kanembo Jkt kunawa mpira. Baada ya kuzongwa na wachezaji wa Jkt Refa alianza kurusha masumbwi kwa wachezaji kitendo kilichosababisha vurugu, na mpira kuishia happ
 
Polisi ndo wamefika kuwatoa JKT kanembi hizi timu za majeshi vurugu tupu na polisi Mara waliwafanyia Stand Utd vurugu TFF ichukue hatua
 
Vurugu sio mpaka jeshi, miaka ya nyuma kuna wanaume walimgonga refa hapo Taifa. Ila sio uungwana...
 
stand utd lazima ipande ligi kuu hii mi timu ya majeshi hovyo tu tumeipa nafasi miaka mingi hakuna inayofanya
 
Polisi ndo wamefika kuwatoa JKT kanembi hizi timu za majeshi vurugu tupu na polisi Mara waliwafanyia Stand Utd vurugu TFF ichukue hatua

Malinzi kasema ole wao wanaofanya vurugu viwanjani, ame-cite vurugu za Mbeya na Dar, amesema adhabu kali zitatolewa bila upendeleo wala uonevu na bila kuogopa chochote hata kama ni bastola (asomaye na afahamu).
 
Kwa hiyo adhabu ya kumpiga refa itapitiwa upya?
 
stand utd lazima ipande ligi kuu hii mi timu ya majeshi hovyo tu tumeipa nafasi miaka mingi hakuna inayofanya

Mwakani Ligi kuu lazima Shinyanga hivyo hivyo kidogo kidogo tunachangishana ila tutafika, Sio ka Mwadui walipewa milioni 100 wakashindwa kupanda
 
Malinzi kasema ole wao wanaofanya vurugu viwanjani, ame-cite vurugu za Mbeya na Dar, amesema adhabu kali zitatolewa bila upendeleo wala uonevu na bila kuogopa chochote hata kama ni bastola (asomaye na afahamu).

Na leo kuna mechi kati ya Mwadui FC na Polisi Dodoma na tulikuwa na baadhi ya Wachezaji wa Polisi wanadai wakizidiwa watavunja mechi ili mechi irudiwe neutral ground...... hata baada ya tukio la jana Jkt Kanembwa wanasema tutakutana Tabora means mechi itarudiwa neutral ground ila sijui hili lina ukweli kiasi gani
 
Kwa hiyo adhabu ya kumpiga refa itapitiwa upya?

Adhabu ya kumpiga Israel Nkongo (I presume) ilishatolewa na Yanga waliathirika sana hadi kukosa ubingwa mwaka huo, kama unataka ipitiwe pengine ufafanue ni wapi haki haikutendeka. Yanga na refa huyo hakuna bifu wala nini kwani mwenyewe umeshuhudia juzi juzi kachezesha na kujipatia zawadi kwa uchezeshaji safi. Sasa ni zamu ya Simba kupigwa rungu la TFF, Julio sijui kama hatafungiwa maana ndiye aliyehamasisha vurugu pale Taifa.
 
Mbona mnatafsiri mpendavyo tu? Mtoa mada ameeleza kuwa Kanembo walilalamikia penalti. Hilo ni la kawaida mpirani. Baadaye refa akaanza kurusha ngumi. Hilo si la kawaida. Alipaswa kuonyesha kadi au hata kumaliza mchezo baada ya muda. Lakini sio kuanza kurusha yeye ngumi. Ni kosa la kadi nyekundu. Nani angemwonyesha?
 
Hata mi ndo nauliza hivyo je kama kosa ni la refa itakuwaje?? Je tutabaki na hiyo point moja? Coz penalty haikupigwa, je mechi itarudiwa coz haikuisha au tutapewa point za mezani?..... Ingawa timu za majeshi ni korofi na ni kama vile zinajiona zina haki ya kupanda ubabe mwingi kiwango hakuna. Hizo point tatu ni muhimu kwa Timu yetu ya Stand Utd ili tuongoze kundi kwa tofauti ya point 4. Baada ya kumaliza first round
 
Vurugu sio mpaka jeshi, miaka ya nyuma kuna wanaume walimgonga refa hapo Taifa. Ila sio uungwana...

Wanaume wengine walienda pale Unyanyembe Tabora baada ya kuzidiwa maujanja na katimu ka Milambo walitembeza mikono si kawaida, pale ilikuwa man to man kati ya hiyo timu ngeni na timu mwenyeji. Timu ngeni inatokea katika mtaa mmoja jijini Dar es Salaam, pale kwenye jengo chafu kuliko majengo yote, juu yake kuna kijibendera chenye rangi kama zile rangi za Vodacom.
 
Ile mechi Kati ya Stand utd na Jkt Kanembwa ambayo kamati ya mashindano iliamua irudiwe Tabora sasa itachezwa kesho ktk Uwanja wa Kambarage hii ni kufuatia Stand Utd kushinda rufaa Yao
 
Ile mechi Kati ya Stand utd na Jkt Kanembwa ambayo kamati ya mashindano iliamua irudiwe Tabora sasa itachezwa kesho ktk Uwanja wa Kambarage hii ni kufuatia Stand Utd kushinda rufaa Yao

hiyo mechi haitachezwa,imeahirishwa until further notice.
 
hiyo mechi haitachezwa,imeahirishwa until further notice.

Aaah kwa nini?? Au ni Kweli mnataka kuibeba Jkt Kanembwa Sisi tunaongoza kundi wao wanafata!!! Penalty atoe refa, vurugu aanzishe refa, adhabu tupewe Sisi.... Mzee hatukuelewi Stand utd tumeibeba kwa michango yetu haiendeshwi na ruzuku ka Mwadui na Kanembwa afu mnataka kutudhulumu asee ... Poa bhana waliosema Ng'ombe wa maskini hazai hakukosea.... Haya wabebeni Jkt au mnataka timu toka Mwanza ndo ipande
 
Kwa hiyo hili mlilipanga mapema mh. Jamal Malinzi, maana tangia kuvunjika kwa mechi hao mJkt walisema tutakutana TBR na mkaamua hivyo, hii mechi ni haki yetu na hatutaki ushindi wa mezani.. lkn TBR hatuendi.... Hata mkibana kupanda tutapanda tu hata kwa ngazi ya miba... Premier league ni ya Tz nzima si ya baadhi ya mikoa, tumechoka Khaa kila siku nyie tu
 
Hivi upuuzi wa namna hii África utaisha lini? Mechi inaghairishwa kwa vurugu za uwanjani zilizo sababishwa na Refa?
 
Back
Top Bottom