Vurugu bungeni zasababisha Bunge kuahirishwa asubuhi hii

Kwa Hali iliyopo naona Sasa muda wa Mathias Chikawe kuondoka umefika
Maagizo waliyoyatoa kwa ma RPC kuwa Viongozi wapigwe sasa yanamgeuka waziri
 
Umesha hukumu kuwa ninaunga mkono kutojadiliwa! Nimesahihisha andiko kuwa amekataa kujadiliwa. Naamini angeruhusu kamati ya uongozi wa bunge ikae kuona uwezekano wa kujadliwa leo kusingetokea yaliyotokea. Tatizo la Makinda ni speed ndogo ya kufikiri.

kamati ikutane ili iweje???? hivi ile kanuni ya bunge ya 47 ilivyosomwa na mh. mbatia umeielewa kweli! Spika karizika ile ni hoja ya dharura kweli, na kanunu inamtaka kuhahirisha shughuli zote kwa muda huo kuruhu mjadala ,sasa yeye kafanya nini??? ebu fungueni hizi bongo zenu jamani ahaha! mnachosha
 
ni demokrasia nimeipenda hii, alichotendewa Lipumba ni utovu wa adabu lazima jambo lifanyike IGP anatakiwa kujipima. Lipumba ni kiongozi mkubwa chama chake kiko madarakani ndio kusema ni wa level nyingine, kumgusa tu walitakiwa wawaze mara mbili. lazima serikali itoa tamko imemchukulia hatua gani IGP au yule RPC au kiongozi aliyekuwepo kwenye tukio sio swala la mjadala.
apongezwe JK kwa kusimamia demokrasia Tz.

NB: hiki walichoonyesha wabunge ndiyo busara inayotakiwa sio kama walivyoboronga BMK
 
Baada ya Mbatia kuleta hoja ya dharura juu nguvu iliyotumiwa na polisi kwenye maandamano ya CUF jana tarehe 27 January ili ijadiliwe na wabunge kama hoja ya dharura, spika Makinda aliamuru serikali ilete majibu kesho ndio ijadiliwe.

Wabunge walisimama kushinikiza hoja ijadiliwe lakini Makinda aliendelea na msimamo wake wa hoja kujadiliwa kesho baada ya Serikali kuleta majibu, hapo ndipo sintofahamu ilipozidi na kuleta kutoelewana kati ya wabunge wa Upinzani na Spika. Ilibidi spika Anna Makinda kuahirisha bunge mpaka kesho lakini baadae akabadili na kusema saa kumi jioni leo hii.

Kwa habari zaidi, soma=>Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, January 28

Hili bunge lina matatizo kuanzia spika hadi wabunge wenyewe.Bunge lina agenda ambazo zilipangwa kujadiliwa.Sasa linatokea tukio mtaani wanaahirisha na kuacha ajenda kuhamia matukio ya barabarani.Waliokamatwa watapelekwa mbele ya vyombo vya sheria kutakakojulikana kama CUF walikosea au la.Bunge kiherehere chake cha nini? wanajadili nini wakati suala liko mikononi mwa vyombo vya sheria?

Bunge limekuwa linaanza kwenda na matukio badala ya ajenda zilizowapeleka pale.Hizi zote ni mbinu chafu za kutaka kuzidisha siku na kula posho zitokanazo na kodi za wananchi.

Hili bunge hovyo kabisa heri uchaguzi uje upesi wachaguliwe wabunge wengine wapya kuliko hawa wa sasa.LO.
 
Kwa Hali iliyopo naona Sasa muda wa Mathias Chikawe kuondoka umefika
Maagizo waliyoyatoa kwa ma RPC kuwa Viongozi wapigwe sasa yanamgeuka waziri
Chikawe na IGP Mangu wanapaswa kujua kuwa amani ya nchi hii haiwezi kusimamiwa kwa marungu na vitisho vya kuwafunga watu mahabusu!!
 
Katika maigizo yanayoendelea Bungeni inasikitisha sana Bunge kutojari muhimili mwingine na kujiona wao ni wao na hakuna mwingine.

Hivi inaingia akilini kuanzisha fujo Bungeni kisha eti hoja aliyoleta Mbatia ahijadiliwi leo na kusababisha shughuli za Bunge kusitishwa?. Chukuliwa kila upande uwe na msimamo na tuone utakao shindwa, mimi nimesema hoja itajadiliwa kesho na wewe unasema ijadiliwe leo, wakati huo mimi ndo nimeshikilia rungu itawezekana kweli wewe kushinda bila kutumia busara?.

Kinachosababisha upinzani kupata misukosuko ni kutotii sheria na kujitungia za kwao "Nguvu ya umma" na kusahau kama watakimbilia kule wanakokutukana na kuomba msaada.

Rejea maneno ya kanga anayoyatoa Dr. Slaa akiwa jukwaani juu ya Jeshi la Polisi utafikiri anawashambulia watoto wake na kujiona ananguvu nyingi kuliko wao. Ilifikia wakati anataka kujifanananisha na Nyerere eti mbona nimefika hapa polisi walikuwa wapi?. Vivyo hivyo na Lipumba, ahaiwezekani mkubaliane maandamano yasiwepo kisha ukaandamana kwa kisingizio cha Nguvu ya umma. Kuvunja sheria hakuangali Nguvu ya umma wote kwa pamoja lazima tutii sheria ili tuishi kwa amani.

Sasa Serikali imechoka kuona inazalaurika kila wakati tumeamua kufanya kazi, haiwezekani Bunge kujiona eti wao ndio muhimili Bora kuliko yote kisa eti walishinikiza sakata la Escrow kupitishwa kihovyohovyo na kusababisha hasara kubwa kwa Serikali bila faida yeyote sasa basi na lolote na liwe.

Ushauri kwa Upinzaji kama inawezekana adui lazima uishi nae vizuri ili umshawishi kirahisi akuamini na kukupa madaraka ya kumtawara ama kumuongoza bila kutumia nguvu nyingi. Tumie ujuzi aliotumia Nyerere hadi Wakoloni wakamwamini bila kutumia nguvu, kama mambo yataendelea hivi Watanzania hawatawaamini kwani watahisi harufu ya vita mbeleni, hivyo lazima umimi uwatoke kurudi kwenye sheria na kuteka Jeshi kimawazo.

Na mwisho lazima kutambua kuwa kwenye migogoro hiyo Serikali ina watu wake ili kupunguza ukali wa hoja zilizopo vichwani mwa watu.

Haya ni mawazo yangu tu kama tata mura.
 
Kwa Hali iliyopo naona Sasa muda wa Mathias Chikawe kuondoka umefika
Maagizo waliyoyatoa kwa ma RPC kuwa Viongozi wapigwe sasa yanamgeuka waziri
Hili swala linahusu hata huyu IGP haiwezekani mwenyekiti wa taifa CUF kudhalilisha na polisi wa ccm kwa kutumia ubabe huu uonevu ndo utakuwa umefikia mwisho sasa mbona kwenye maandamano ya ccm hatujawahi kusikia mabomu yamepigwa kila siku UPINZANI tuu kwa nini upinzani tuuu.
 
kamati ikutane ili iweje???? hivi ile kanuni ya bunge ya 47 ilivyosomwa na mh. mbatia umeielewa kweli! Spika karizika ile ni hoja ya dharura kweli, na kanunu inamtaka kuhahirisha shughuli zote kwa muda huo kuruhu mjadala ,sasa yeye kafanya nini??? ebu fungueni hizi bongo zenu jamani ahaha! mnachosha

Uko so judgemental!
 
Chikawe na IGP Mangu wanapaswa kujua kuwa amani ya nchi hii haiwezi kusimamiwa kwa marungu na vitisho vya kuwafunga watu mahabusu!!
pia lazima watambue hakuna AMANI BILA HAKI.
 
ni demokrasia nimeipenda hii, alichotendewa Lipumba ni utovu wa adabu lazima jambo lifanyike IGP anatakiwa kujipima. Lipumba ni kiongozi mkubwa chama chake kiko madarakani ndio kusema ni wa level nyingine, kumgusa tu walitakiwa wawaze mara mbili. lazima serikali itoa tamko imemchukulia hatua gani IGP au yule RPC au kiongozi aliyekuwepo kwenye tukio sio swala la mjadala.
apongezwe JK kwa kusimamia demokrasia Tz.

NB: hiki walichoonyesha wabunge ndiyo busara inayotakiwa sio kama walivyoboronga BMK
Hata hasingekuwa Lipumba, huuu ni ujinga wa kipumbavu uliyofanywa na polisi kwa mwanadamu mwenye utu wake
 
Hili bunge lina matatizo kuanzia spika hadi wabunge wenyewe.Bunge lina agenda ambazo zilipangwa kujadiliwa.Sasa linatokea tukio mtaani wanaahirisha na kuacha ajenda kuhamia matukio ya barabarani.Waliokamatwa watapelekwa mbele ya vyombo vya sheria kutakakojulikana kama CUF walikosea au la.Bunge kiherehere chake cha nini? wanajadili nini wakati suala liko mikononi mwa vyombo vya sheria?

Bunge limekuwa linaanza kwenda na matukio badala ya ajenda zilizowapeleka pale.Hizi zote ni mbinu chafu za kutaka kuzidisha siku na kula posho zitokanazo na kodi za wananchi.

Hili bunge hovyo kabisa heri uchaguzi uje upesi wachaguliwe wabunge wengine wapya kuliko hawa wa sasa.LO.

tatizo lako wewe huna shule( huna elimu kichwani) ndio maana huelewi mambo nadhani unaujua ushamiki tu bila kutumia akili.
Huwezi kujadili jambo usilo lijua maana lipo juu ya uwezo wako wa akili . Wewe saizi yako ni kuisifia mikutano ya kinana tu basi hayo mengine waachie wasomi huyawezi.
 
tatizo lako wewe huna shule( huna elimu
kichwani) ndio maana huelewi mambo
nadhani unaujua ushamiki tu bila
kutumia akili.
Huwezi kujadili jambo usilo lijua maana
lipo juu ya uwezo wako wa akili . Wewe saizi yako ni kuisifia mikutano ya kinana
tu basi hayo mengine waachie wasomi
huyawezi.
 
Back
Top Bottom