Vurugu Bungeni-"Blessing in Disguise!"- "Ni Kitendo cha Kishujaa! Kinachostahili Kupongezwa!".

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,495
113,592
Wanabodi,

Kwa kuanzia, japo siungi mkono vurugu za aina yoyote, lakini naunga mkono kwa asilimia 100% kilichotokea bungeni!.
Zile fujo ni matokeo tuu na sio chanzo!. Nimewasikia baadhi wa wabunge na wachangiaji kadhaa, wakilaani matokeo ambayo ni vurugu, ila hawajiulizi chanzo!.

Kwa vile chanzo ni Naibu Spika, sababu ni "kupinga unyanywasaji na udhalilishwaji wa wazi kwa KUB", vurugu zilizofuatia ni matokeo tuu ya provocation "actions under provocation" ni defence muafaka hata mbele ya sheria!.
Mimi Pasco wa JF nasisitiza kuwa "Wapinzani, did the right thing!". Hiki ni kitendo cha kishujaa cha kustahili kupongezwa na sio kulaaniwa!.

Kitendo hicho mimi nakiita ni "Blessing in disguise!", japo kwa jicho la juu juu ni kitendo kibaya, kiovu na cha kulaaniwa!, ila ukikitazama "kwa jicho la tatu", ni kiashiria cha kwanza cha mwanzo mzuri wa a "United We Stand!" na mwisho wa "Divided we Fall!".

Tangu kuasisiwa kwa vyama vingi nchini, tukio la jana ndilo la kwanza ambapo, the "giants!" wameacha tofauti zao na kusimama pamoja against "oppressors" ambapo msimamo huu ukiendelea, na mshikamano huu, kuendelezwa hadi 2015, wakafanikiwa kumsimamisha mgombea mmoja strong!, 2015 for sure bila kumunyunga maneno wala kupepesa macho!, CCM inakwenda chini!, just like the fall of Goliath!.

Hivyo huu unaweza kabisa kuwa ndio mwanza wa kwanza wa kweli wamwisho wa CCM!.

Big Up Wapinzani!.

Pasco.
NB. Pasco wa jf, ni mwanachama wa chama cha siasa!, ila anaandika independently with objetivity, impartiality and balance, free from his political affiliation.
 
For sure.
Mimi siyo mfuatiliaji wa bunge lakini kwa hili nimejikuta nafatilia na ku conlude kuwa upinzani wanaonewa bure tena kwa vitu visivyokuwa na msingi.
 
Tatizo la watu humu ni jazba na mawazo yanayoelekezwa na hisia badala ya LOGIC. "KUB" inaweza kumaanisha Kubwa Jinga au Kiongozi wa Ujinga Bungeni. Mamlaka yapo kwa sababu bila mamlaka hakuna utawala. Kura zimepigwa za mdomo watu wameomba zihesabiwe, zimehesabiwa... watu wametupilia mbali hoja... Zamu ya Mrema kuongea, watu hawataki... Cheap theatrics to be honest.
 
Mbowe alisimama kabla ya Mrema, sheria inamruhusu kuongea. Muttonhead
 
Siku zingine Pasco unakuwa na akili lakini mwezi ukikaa vibaya basi unachafua hali ya hewa...unakuja na Lowassa wako!

Kwa hili nakuunga mkono kwani ndio njia pekeee iliyokuwa imebaki kuonyesha watanzania kuwa haki haitendeki ndani ya Bunge na katiba itakayotoka itakuwa ni ya CCM

....Pia Vyama vya upinzani vinatakiwa uchaguzi ujao waweke wabunge vijana wengi zaidi kule Bungeni wamsaidie Mheshimiwa Sugu kurudisha heshima na adabu ya mjengo kwa hawa wajinga wa CCM...ikitokea vita kama ya jana basi iwe vita kweli kwani ya jana naona ilikuwa ni trela tu,

Je ni kweli kuwa Bunge linaahirishwa leo kama muuaji Nchemba anavyodai kwenye thread yake?
 
Pongezi nyingi Pasco kwa kuliona hili....Wapinzani, watu wengi wako nyuma yenu,unganeni mfanye kitu!!
 
consequences of being "Minority" or ''Majority'' wakati mwingine ni vizuri kutafakari kwa undani zaidi kabla ya kuchukua maamuzi.. anyway watu wako kazini!!!!
 
Pasco mbona watakukoma safari hii!!! wape tu za uso,wamezidi uzandiki utadhani si Chama kikongwe barani Afrika.
 
Last edited by a moderator:
wamezidi kuwaonea upinzani hawa mbulula...
Vyama vyote vya upinzani safi sana endeleeni hivyo2 mpaka kieleweke
 
Tatizo la watu humu ni jazba na mawazo yanayoelekezwa na hisia badala ya LOGIC. "KUB" inaweza kumaanisha Kubwa Jinga au Kiongozi wa Ujinga Bungeni. Mamlaka yapo kwa sababu bila mamlaka hakuna utawala. Kura zimepigwa za mdomo watu wameomba zihesabiwe, zimehesabiwa... watu wametupilia mbali hoja... Zamu ya Mrema kuongea, watu hawataki... Cheap theatrics to be honest.

Huna haja ya kukashifu na kutukana.........toa hoja tu utaeleweka
 
Big up Pasco !

Kama wabunge tena waliochaguliwa na wananchi hawaheshimiwi wala kutendewa haki tena wakiwa bungeni?? Hivi itakuwaje kwa raia wa kawaida kama mimi huku mtaani??
 
Last edited by a moderator:
CCm na serikali yao wamewekwa kona mbaya, wanaamua kutumia dola ili kufanikisha matakwa yao. Hao jamaa hawakumbuki historia kwamba wakina chiluba walitunga katiba za kibaguzi akidhanib ataishi madarakani milele. Mwisho wake ileile katiba ikamrudi mwenyewe.
 
Tatizo la watu humu ni jazba na mawazo yanayoelekezwa na hisia badala ya LOGIC. "KUB" inaweza kumaanisha Kubwa Jinga au Kiongozi wa Ujinga Bungeni. Mamlaka yapo kwa sababu bila mamlaka hakuna utawala. Kura zimepigwa za mdomo watu wameomba zihesabiwe, zimehesabiwa... watu wametupilia mbali hoja... Zamu ya Mrema kuongea, watu hawataki... Cheap theatrics to be honest.
Chanzo sio wingi au uchache wa kura, chanzo ni kukataliwa mwongozo wa KUB, hadi sasa hatujui Mbowe alitaka kuomba nini? angesikilizwa tusingejua kama vyama vyote vya (isipokua Mrema na TLP) vingeungana, hapa pia nampongeza ndugai cause yeye ndio sababu ya kuufanya huo mungano. Safi sana ndugai.
 
Nimeshawishika kuwaambia waserikali na chama chake baada ya kukerwa na jinsi bunge linavyoendeshwa,

Nje ya bunge mmetumia polisi, mmewaua raia kwa makusudi tena kwa kutumia silaha, hamjaridhika na hilo, sasa mmehamia ndani ya Bunge, walikosheheni wawakili wa wananchi nako mmeanza kuwatumia polisi kupiga wawakilishi wa wananchi, mimi nawaambieni siku wahusika mliowanyanyasia wawakilishi wao wakisukumwa na dhamira ya kujitenga kutoka jamuhuri hii pendwa hakika hamtakumbuka mlipojikwaa, mtakimbilia oooh! wahaini, wasaliti.........
enyi wana ccm, dhibitini ukichaa wa ndugai, mwambieni vyeo huja na kupita "No condition is permanent"

ANAWEZA KUZALISHA:-
jamhuri ya watu wa bukoba
jamhuri ya watu wa mbeya
jamhuri ya watu wa kigoma
jamhuri ya watu wa Ntwara
jamhuri ya watu wa kilimanjaro.

"Kuna vitu vitatu viKkitokea nchi hutikisika, naam kwa vinne haiwezi kuvumilia
1) ......
2) ......
3) ......
4) mjinga (ndugai) ashibapo chakula!!!!!
 
Hakuna nchi inaongoza bunge kwa polisi....kama ni hivyo basi nchi ambazo mabunge yake yana mabishano makali na vijembe kama korea...philipines..us..uk...ukraine...wangeuana kabisa
 
Back
Top Bottom