Endeleaaa
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 1,485
- 738
utaifa ulioporwa ni utaifa gani?
baada ya kuporwa huo utaifa wako ulioasisiwa na wakoloni waliotwala Tanganyika, unajutia uhuru wako uliokukirimu utaifa mpya?
wewe huna utaifa?
unayo passport?
umeishawahi kusafiri nje na kuchanganyikana na watu wa mataifa mengine ukakosa kutambuliwa?
utaifa uliopachikwa na wakoloni wako ndio bora kuliko utaifa tunaouchukua vifuani mwetu na ulioasisiswa na watanzania wenzako wanamapinduzi?
Tuambie umuhimu wa huu Muungano na tusipokuwa kuwa na huo Muungano tunapoteza nini?
Unaona Tanganyika ni ukoloni? au utawala ndio ulikuwa wa kikoloni? kwani Zanzibaar kabla ya mapinduzi ilikuwa inaitwaje? mbona baada ya mapinduzi na hata muungano zanzibar imebaki kuitwa zanzibar? mataifa mangapi yamebadili majina ya utaifa wao eti kwa kisingizio kama hicho kuwa hayo majina yameletwa na wakoloni?
Mbona mipaka ya tanganika iliwekwa na wakoloni lakini baada ya uhuru hatujaibadilisha? au wewe kinachokukera ni jina tanganyika? Wewe unajua jina Tanzania mwalimu alilitoa wapi na lina maana gani?
Kama Muungano umekuwa ndio chanzo cha Zanzibar kudidimia kiuchumi kwanini waung'anga'anie the same kwa watanganyika.
Tueleze sababu za msingi za kwanini tuendelee kuamini kwenye Muungano huu wa vitu. maana ki uhalisia muungano huu sio wa watu bali wa vitu.