Vunjeni Muungano lkn mimi nitabaki Mtanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vunjeni Muungano lkn mimi nitabaki Mtanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwanaone, Apr 24, 2011.

 1. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
  Najua wengi wenu mtahisi au mtaniona kama mropokaji lkn kamwe damu ya kitanzania na kamwe haitakuwa ya tanganyika wala ya kizanzibari. kwangu hupatwa na mfadhaiko nikimsikia mtu anajitambulisha yy ni mzanzibari au yy ni mtanganyika. uchezeeni muungano leo lkn kesho mutajuta. tunachotakiwa ni kuurekebisha mfumo wa muungano wa si kutengana haswa ktk wakati huu ambao tuhitaji kuujenga uchumi wetu. lkn mkiamua kamwe sitokuwa mtanganyika wala mzanzibari.
   
 2. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Utakuwa nani sasa? Tanzania ni muungano wa Zanzibar na Tanganyika.

  Zanzibar ipo na itakuwepo, Tanganyika mliiua wenyewe.

  Zanzibar inaweza kuwepo bila Tanzania lakini hakuna Tanzania bila Zanzibar.

  Kwa tunavyokwenda hapana muda ukajikuta unakuwa Mkenya au Mganda au........

  Huu mnaouita nyinyi muungano, si muungano ni uvamizi na haurekebishiki tena, ni kuvunjika tu.
   
 3. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Kwani wanaotaka muungano uvunjwe umesikia wanakuambia ubadilishe jina la huku bara? wewe baki na tanzania wao watachukua Zanzibar kwani zanzibari ina bendera yake, ina wimbo wake wa taifa,ina nembo yake, ina bunge lake na vyote hivyo vinatambulika kimataifa.
   
 4. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Naomba unipe FAIDA Kumi (10) tu za Muungano ili tujiridhishe nasi tukuunge mkono kutouvunja.
   
 5. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
  ni kujidanganya kusema zanzibar itakuwepo baada ya kuuvunja muungano. kama mnakumbuka mii ya hivi ya karibuni kuna wazee wa kipemba walikwenda ofisi za umoja wa mataifa kutaka kuwasilisha malalamiko yao ya kutaka pemba na unguja zitenganishwe kwani unguja imekuwa inainyima pemba fursa za kupata maendeleo. ndugu nawaambia muungano una umuhimu sana kwetu sisi lkn kama mnahisi hauna maana jaribuni kuuvunja na muuone matokeo yake. MUNGU UJAALIE MUUNGANO WETU UDUMU, MUNGU TUJAALIE TUZIREKEBISHE KASORO ZA MUUNGANO WETU SALAMA. MUNGU NIJAALIE NIWE MTANZANIA DAIMA. MUNGU IBARIKI TANZANIA. MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU TUUPUSHIE MBALI WALE WOTE WASIOTUTAKIA MEMA KTK MUUNGANO WETU.
   
 6. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Tanzania haiwezi kukwepa historia! Miungano yote ya kulazimisha inapata kifo cha asili. Iangalie USSR Kuanzia vita vikuu vya 2 Hadi 1990 au Yugoslavia chink ya Tito iliyogeuka kuwa nchi Saba za eneo la Baltic. Kwa hapa Africa angalia iliyokuwa Senegambia sasa hivi kuna Senegal na Gambia. Mambo ya muungano hayapaswi kulazimishwa bali watu waingie kwanhiari baada ya referandum.

  USA ina muungano wa tofauti ambapo zile states ziliunganishwa kwenye umoja kwa civil wars zilizodumu kuanzia 1776 mpaka mwamzoni mwankarne ya 18. Lakini zile states Zina autonomy kubwa kisiasa na kiuchumi. Status ya Gavana wa California Schwazznegger yaweza kuwa kubwa kuliko hata PM wa Uingereza
   
 7. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Nipe basi FAIDA KUMI za Muungano ili nijiunge nawe kuuimarisha Mkuu!!
   
 8. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
  kuna fursa nyingiu wanazopata wazanzibari au watanganyika ktk muungano
  japo sikatai kama kuna matatizao ktk muungano wetu kutokana na viongozi wetu ama muundo wa muungano;
  hivi sasa wazanzibari wana fursa sawa za kujiunga na vyuo ambavyo vipo tanganyika kama ilivyo kwa watanganyika kwa vyuo ambavyo vipo zanzibar. pia wazanzibar hawana kikwazo chochote cha kufanya kazi au biashara zanzibar kama ilivyo kwa watanganyika kwa upande wa zanznibar. na zipo fursa nyingi amabazo sisi wananchi wa pande zote mbili kwa namna moja ama nyingine tunafaidika kutokana na muungano wetu. lkn nahisi wanaosema huu muunganop hauna faida nio bora uvunjike watupe ni hasara zipi wanazipata kutokana huu muungano na kwanini tusioboreshe muungano na kuundoa hizo kasoro zake badala yakje tuuvunje?
   
 9. Bangusilo

  Bangusilo Senior Member

  #9
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi ni mtanganyika orijinali na pata huo mfadhaiko mpaka ulowe ukimaliza .
  Nipe faida kuu 5 za muungano na sizewe za kufikirika!.
  Kama wewe ni mwanafamilia wa wanasihasa njaa wanaofadika na muungano lazima utautetea tu.
   
 10. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ingekuwa BORA ukatupa wewe hizo FAIDA KUMI za Muungano na HASARA japo KUMI za Muungano kuvunjika.
   
 11. T

  Taso JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Hatuwezi kujuta, muungano sio lazima, viinchi vingapi vidogo kama karanga vina nguvu kuliko Tanzania na li muungano lake?

  Swaziland, Lesotho, Botswana, wameungana na nani?


  Hatujaenda Ulaya, viinchi kama Belgium, Luxembourg, Uswizi wameungana na nani?

  Kill the Muungano!
   
 12. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Yaani we ndo umempunguzia mpaka FAIDA TANO duh!!
   
 13. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
  naombeni wale wote ambao wanasema muungano uvunjike wataje hasara mbili 2. mimi nimeshataja faida ninazoziona
  1: elimu - wazanzibari wanfaidaka ktk elimu ya juu wakija kusoma tanganyika wankopeshwa sawa na wanalip[a ada sawa kama watanganyika na watanganyika wakienda zanzibar hivyohivyo wanapata fursa hiyo.
  2; kuna free trade btn zanzibar na tanganyika. mzanzibar hapati aina yyte ya kikwazo akitaka kufanya biashara tanganyika kwa sababu ya uzanzibar wake na mtanganyika hivyohivyo hapati vikwazo akitaka kufanya biashara zanzibar.

  sasa nyinyi munaouona hauna faida tajeni hasara mbili mnazozipta kwa ajili ya huu muungano wetu.
  MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU UBARIKI MUUNGANO WETU.
   
 14. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mueleweshe bado hajajua tu. Anafurahia Tanganyika yetu kuuawa, tunaitaka TANGANYIKA ebo!!
   
 15. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,229
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Kama Muungano ungekuwa muhimu kiasi hicho basi ungekuta leo hii dunia ni moja na hakuna mipaka ya ki nchi. lakini lazima ujue kila mipaka ina maana na umuhimu wake, hao waliotuwekea hii mipaka ya ki nchi walifikiri na kutizama mbali sana. Na ndio maana kila ukivuka mpaka wa taifa moja kwenda jingine hukutana na watu wa tofauti kabisa na wale wa taifa ulilotoka.

  Bila Muungano wa kitaifa bado maisha yanawezekana maana cha muhimu si muungano bali ushirikiano. Taifa moja laweza kushirikiana na taifa jingine katika mambo flani flani bila kuungana na mifano tunayo Sadec.

  Tanganika na Zanzibar zaweza kuwa na ushirikano kwa mambo hayo tunayoyaita ya Muungano lakini Kila taifa likawa huru hivyo kusiwe na Rais wa Muungano. iwepo tu kamitii ya shirikisho itakayoratibu na kusimamia hayo mambo ya shirikisho thats it.

  Pemba kuwa na serikali yake na Unguja kuwa na yake bado si tatizo kama uwepo wake utakuwa ndio maedeleo kwa wapemba na waunguja.

  Kwa jinsi serikali moja inaposimamia eneo kubwa ndivyo inavyokuwa taabu kwa serikali hiyo kuhudumia watu wa eneo hilo.

  Kama inabidi hata hiyo tunayoitaka iwe tanganyika inabidi iwe na sub governments ambazo zitachaguliwa na wananchi wa eneo husika.

  Mwisho. Muungano ni mzuri lakini ni pale tu unapokuwa kwa faida ya wote na si wachache tu.
   
 16. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye BOLD tolea ufafanuzi tena kwa ushahidi, maana mimi nimefanya biashara ya nafaka mwaka 2008 kwenda unguja adha niliyokutana nayo Mungu ndo anajua. Nilikuwa napitisha mazao kupitia bandari ndogo ya Mkwaja kwenda Mkokotoni, nalipa ushuru wote na bado nasumbuliwa na masheha. Unajua lakini unachokisema?
   
 17. J

  Joshua Bukuru Member

  #17
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 25
  Nikujibu ndugu,
  Hakuna mtanzania yeyote anapenda kuona muungano uvunjike lakini muundo wa muungano uliopo hauvumiliki kwa watanganyika na wazanzibar. Linalotakiwa ni kuwauliza watanzania ni aina gani ya muungano wanapenda au wanapendelea. Jibu la wengi ni kuwa na serikali tatu ingawa mwalimu Nyerere alitahadhalisha gharama ya kuendesha serikali tatu hatuwezi na mzigo mkubwa utaiangukia Tanganyika, kuwa na serikali moja kamwe visiwani hawatokubali. Kama itatokea tusielewane ni heri tuachane salama kila upande uwe na serikali yake ili tujenge nchi zetu. Tanganyika waijenge tanganyika yao na wazanzibari waijenge zanzibar yao. Tutashirikiana kiuchumi, kijamii na kisiasa. Iwapo hili likitokea, basi utanzania umeisha na hakutokuwa na taifa la Tanzania. Sasa basi, kama hutakiwi kuwa mtanganyika au mzanzibari basi jiandae kuwa raia wa nchi nyingine tofauti na hizo mbili tajwa hapo juu. Sijui utasafiria passport gani, utakuwa na kitambulisho gani, nadhani unayasema haya kwa kuwa hayajatokea, ikitokea huna pa kwenda ndugu yangu. Tusingependa kuona hayo yote yakitokea kwa kuwa na mimi mwenyewe naupenda muungano wetu. Serikali 2 ni mzigo kwa raia wote, tujadili la serikali 3 au moja.
   
 18. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #18
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wakati wa shida walipenda muungano, sasa wamevimbiwa hewa inawatoka ovyo wanataka nafasi.... labda hewa inanuka sana yakhe!!!
  wapende wasipende wataendelea kuitegemea Tanganyika kwa kila kitu, jeuri yao mafirauni wa kiarabu? kwani Somalia, yemen inayopakana na Saudia au Uganda, wote hawa wako kwenye jumuiya ya nchi za kiislam na kiarab ligi, je wana nini kuliko sisi? sema jawako sawa kimentali hao jamaa zetu wazenji, sema kwa mademu si haba alhamdulillahi, japo mademu wenye mara wanagoma kutoa mpaka uzunguuke mlango wa uwani...
   
 19. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #19
  Apr 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  hicho ndicho kinacho nishangaza mimi hadi leo hii,huu muungano hauelewi,mala zanzibar sio nchi lakini ukiwa zenzi unakuta wanaendesha nchi yao kwa sheria,kanuni na taratibu zao kama ulivyo taja wanakila kitu cha kuitambulisha kuwa ni nchi sasa huu muungano ni nani na nani?
  kama vipi nasi tuwe na nyimbo yetu,bendera,nembo yetu,

  YAANI MUUNGANO HUU BADO SIUELEWI KABISAAAA
   
 20. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Na wala hutakaa uuelewe ng'o!!
   
Loading...