Vunjeni Muungano lkn mimi nitabaki Mtanzania

utaifa ulioporwa ni utaifa gani?
baada ya kuporwa huo utaifa wako ulioasisiwa na wakoloni waliotwala Tanganyika, unajutia uhuru wako uliokukirimu utaifa mpya?
wewe huna utaifa?
unayo passport?
umeishawahi kusafiri nje na kuchanganyikana na watu wa mataifa mengine ukakosa kutambuliwa?
utaifa uliopachikwa na wakoloni wako ndio bora kuliko utaifa tunaouchukua vifuani mwetu na ulioasisiswa na watanzania wenzako wanamapinduzi?

Tuambie umuhimu wa huu Muungano na tusipokuwa kuwa na huo Muungano tunapoteza nini?

Unaona Tanganyika ni ukoloni? au utawala ndio ulikuwa wa kikoloni? kwani Zanzibaar kabla ya mapinduzi ilikuwa inaitwaje? mbona baada ya mapinduzi na hata muungano zanzibar imebaki kuitwa zanzibar? mataifa mangapi yamebadili majina ya utaifa wao eti kwa kisingizio kama hicho kuwa hayo majina yameletwa na wakoloni?

Mbona mipaka ya tanganika iliwekwa na wakoloni lakini baada ya uhuru hatujaibadilisha? au wewe kinachokukera ni jina tanganyika? Wewe unajua jina Tanzania mwalimu alilitoa wapi na lina maana gani?

Kama Muungano umekuwa ndio chanzo cha Zanzibar kudidimia kiuchumi kwanini waung'anga'anie the same kwa watanganyika.

Tueleze sababu za msingi za kwanini tuendelee kuamini kwenye Muungano huu wa vitu. maana ki uhalisia muungano huu sio wa watu bali wa vitu.
 
haya ndiyo majibu ya maswali niliyouliza?

kama unataka tujadilianie, nijibu kwanza maswali yale yanayotokana na hoja yako ya utaifa. kisha ongeza na hizi hoja zako mpya, kisha tuendelee

kubishana sipendi na kwa kweli siwezi
 
naombeni wale wote ambao wanasema muungano uvunjike wataje hasara mbili 2. mimi nimeshataja faida ninazoziona
1: elimu - wazanzibari wanfaidaka ktk elimu ya juu wakija kusoma tanganyika wankopeshwa sawa na wanalip[a ada sawa kama watanganyika na watanganyika wakienda zanzibar hivyohivyo wanapata fursa hiyo.
2; kuna free trade btn zanzibar na tanganyika. mzanzibar hapati aina yyte ya kikwazo akitaka kufanya biashara tanganyika kwa sababu ya uzanzibar wake na mtanganyika hivyohivyo hapati vikwazo akitaka kufanya biashara zanzibar.

sasa nyinyi munaouona hauna faida tajeni hasara mbili mnazozipta kwa ajili ya huu muungano wetu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU UBARIKI MUUNGANO WETU.

Wazanzibari wanasoma Tanganyika na sehemu nyingi za Africa, Ulaya, Asia, Australia US n.k na kote huko wanalipa ada kama wengine. Kama ni mikopo, wanasumbuliwa kisawasawa, mpaka Zanzibar imeamua kuunda Bodi yake ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Hivyo kusoma na ada hakuhitaji kuungana, Wazanzibari na Watanganyika wamekuwa wakisoma kabla ya huo unaouita wewe muungano na hata kabla ya uhuru.

Hakuna free trade yoyote ile LAKINI pengine hujawahi kufika Zanzibar. Ukileta chochote kutoka Zanzibar unalipishwa kile kinachoitwa "surcharge" ndani ya muungano wenye mamlaka moja ya kodi TRA

Hasara mimi nitakutajia moja tu na ni kwa upande wa Zanzibar:

Ni ile hali ya kupoteza utaifa wetu na nchi nyengine kutuamulia mambo yetu.

Huu muungano ni kwa faida ya watu wachache tu na kila siku itakuwa tunatatua kero, wakati muungano wenyewe ndio kero.

Daini Tanganyika yenu, iko siku utaamka hamtakuwa na Tanganyika wala Tanzania.
 
utaifa ulioporwa ni utaifa gani?
baada ya kuporwa huo utaifa wako ulioasisiwa na wakoloni walioitawala Tanganyika, unajutia uhuru wako uliokukirimu utaifa mpya?
wewe huna utaifa?
unayo passport?
umeishawahi kusafiri nje na kuchanganyikana na watu wa mataifa mengine ukakosa kutambuliwa?
utaifa uliopachikwa na wakoloni wako ndio bora kuliko utaifa tunaouchukua vifuani mwetu na ulioasisiswa na watanzania wenzako wanamapinduzi?
je, mwalimu nyerere, karume na wanamapinduzi wengine walaaniwe kwa kuwa tu waliasisi utaifa mpya wenye heshima kwa mwafrika na usioakisi ubeberu wa magharibi uliozaa ukoloni wa mataifa ya kiafrika?
kwako utaifa wa kutuniukiwa na mkoloni ni bora kuliko utaifa wa kizalendo?

Utaifa tulioporwa ni wa Tanganyika yetu. Tanganyika ilikuwepo kabla na baada ya uhuru. Hivi sasa tuna utaifa bandia wa Bara. Nyerere aliuzika utaifa wetu kwa kisingizio cha Muungano wa kiini macho.

Tunautaka utaifa wetu wa asili. Kuwa na Tanganyika haimaanishi kurudi yuma bali kuweka mambo sawa. Kuirudisha Tanganyika hakumaanishi kuvunjika muungano bali kuuimarisha zaidi.

Nitafurahi sana ukinijuza maana ya jina Tanzania
 
Sijui mawazo kama haya kwa mtu wa JF huanzia wapi?
Nini unachofaidi kwa kuitwa m-Tanzania? nini utapoteza kwa kuitwa m-Tanganyika? Ni matokeo ya kudanyanywa muda mrefu na hatimaye unang'aka kana kwamba umefikiria kwa makini.

Hata hivyo nani kasema Muungano ufe? Wengi wanadai serikali ya Tanganyika. Serikali hii ikiwepo bado uraia wetu unaweza kubaki ni Tanzania. Kwani Nigeria kuna uraia upi tofauti na Nigeria pamoja na kuwa na serikali zao za majimbo?

Naona tunaendelea kuchanganya mambo tuuu! Mbona kulikuwa na Congo, Ikaja Zaire, ikarudi tena Congo! kipindi chote hicho nini kilileta neena au taabu kwa maisha ya mtu kama wewe!
 
mkuu uyasemayo ni ya kweli kabisa.

Kuna watu humu sijui wanafaidishwa nini na huu utawala wa sasa. wanavyoupigia chapuo.

lakini ipo siku tu haya yote yatafika mwisho Tanganyika itarudi, maendeleo tutayaona na hawa wapinzani wa sasa ndio watakuwa wa kwanza kupongeza.
 
Hivii, naweza kuruhusiwa kugombea uwakilishi au ubunge huko Zenji bila kikwazo?

Gad Oneya, mbona ndugu zako wakina Nzori, Mapuri na N'gumbi wamegombea ubunge na kuchaguliwa kule bila ya matatizo?

Lakini na mimi nikuulize, hivi naweza kwenda maeneo kama Shinyanga vijijini, Bukoba, Same, Rombo na kadhalika kugombea huo ubunge unaosema bila ya kikwazo? Kwa maoni yangu mimi nyinyi wa bara ndiyo wabaguzi zaidi kuliko hata sisi. Majimbo ambayo kabila lo lote linaweza kugombea ni yale ya Dar tu, mengine bila ya kujua lugha yao ya kijijini huoni ndani.

Au mkuki kwa nguruwe kwa binaadamu mchungu?
 
Hatuwezi kujuta, muungano sio lazima, viinchi vingapi vidogo kama karanga vina nguvu kuliko Tanzania na li muungano lake?

Swaziland, Lesotho, Botswana, wameungana na nani?

Hatujaenda Ulaya, viinchi kama Belgium, Luxembourg, Uswizi wameungana na nani?

Kill the Muungano!
KILL, KILL KIIILL wasiotaka uTANGANYIKA WAO waungane na SOMALI au SUDAN si mnapenda kuungana! Mnawaonea wa Zenj tu. Na ukoloni wenu enh!
 
mkuu uyasemayo ni ya kweli kabisa.

Kuna watu humu sijui wanafaidishwa nini na huu utawala wa sasa. wanavyoupigia chapuo.

lakini ipo siku tu haya yote yatafika mwisho Tanganyika itarudi, maendeleo tutayaona na hawa wapinzani wa sasa ndio watakuwa wa kwanza kupongeza.

Hisia yangu ni ile hotuba ya Msekwa. Nadhani kwa kutoweza kuwatafuta wale wanaodhani wako kinyume na CCM ndani ya JF, Sasa CCM inanyaka watu fulani nje ya JF wanaodhani wana uelewa wa kusema saaaana! ili wajaribu kuleta hoja za aina hii. Haya ndo matokeo yake.

Si unaona mtu anakurupuka na kuweka thrd ya aina hii, ambayo haina ushawishi, haina maelezo ya kushawishi. Yaani ni kama hotuba ya Makamba tu!

Tushawishi ili tuone sababu ya uamuzi wako wa kufa na Tanzania.
 
kila siku itakuwa tunatatua kero, wakati muungano wenyewe ndio kero.
Wazanzibar mnajua sana Kiswahili, labda utanielewa kwa hili: Inzi akikuzunguka zunguka usoni ndio kero. Mbu akikuuma, au nyoka, ni tatizo, anaweza kukuua. Muungano sio kero, ni matatizo. Kwa nini hatutumii Kiswahili fasaha kuelezea matatizo yetu?

Mtanganyika nikilipishwa ushuru wa mamilioni kwa kuingiza gari Tanganyika kutokea Zanzibar, hayo mamilioni ni kero au tatizo?

Ninapoona nyumba za ibada za dini isiyokuwa popular Zanzibar zinachomwa moto wakati wao wamejaa Bara huku wanafanya shughuli zao hakuna anaewabughudhi hiyo ni kero au kutafutana vita?

Ninapoona Bunge limejaa wawakilishi kutoka Zanzibar tofauti na uwiano wao, hayo mabilioni ya kugharimia hawa wabunge wa kigeni ni kero au balaa?

Ninapoona waziri wa Zanzibar anatangaza hadharani kimabavu kwamba hatalipia Umeme wakati mimi Mtanganyika sithubutu kuikoromea TANESCO, hiyo ni kero au uonevu?

Ninapoona nusu ya mabalozi, mawaziri wa Muungano, viongozi wa vyama, wanatoka sehemu moja ndoooogo ya nchi, hiyo ni kero au upendeleo?

Ninapoona kura yangu haina nguvu ikilinganishwa na Mzanzibar kwa sababu ya uwakilishi mkubwa wa Wazanzibar kwenye vyombo vya maamuzi, Bunge na Baraza la Wawakilishi, hiyo ni kero au nimebakwa kidemokrasia?

Ninapoona Mtanganyika hawezi kununua kiwanja kirahisi Zanzibar, kujenga, kuendesha biashara, hiyo ni kero au ubaguzi dhalimu?

Ninapoona Zanzibar inaandika Katiba inayokinzana na Katiba ya Muungano na kutangaza unilaterally kufuta kitu fulani katika orodha ya mambo ya Muungano, hiyo ni kero au jinai ya dharau?

Ndio maana wengine tunasema to hell with the Muungano!
 
Taso, Umesema vema. Mimi kama mtanganyika ninauona muungano huu kuwa wa kinyonyaji ambao sehemu ndogo na yenye watu wachache kuliko Wilaya ya Kahama ikiunganishwa na Bukombe ikiinyonya sehemu kubwa ya bara kwa namna nyingi- Kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kinachonisikitisha ni watu hawa wachache kuendelea kulalamika kama ndio wanaokandamizwa na Muungano. Ninaiona hii ni janja ya wazanzibari kutuumiza wabara halafu anayeumizwa amuonee huruma muumizaji silielewi hili.

Hata katika mjadala wa katiba ni muhimu kuwa na katiba ya Tanganyika kwanza ndipo tuzungumze katiba ya muungano. Hili likifanikiwa huenda ikawa mwanzo wa kutibu majeraha tuliyo nayo juu ya muungano wetu.
 
Najua wengi wenu mtahisi au mtaniona kama mropokaji lkn kamwe damu ya kitanzania na kamwe haitakuwa ya tanganyika wala ya kizanzibari. kwangu hupatwa na mfadhaiko nikimsikia mtu anajitambulisha yy ni mzanzibari au yy ni mtanganyika. uchezeeni muungano leo lkn kesho mutajuta. tunachotakiwa ni kuurekebisha mfumo wa muungano wa si kutengana haswa ktk wakati huu ambao tuhitaji kuujenga uchumi wetu. lkn mkiamua kamwe sitokuwa mtanganyika wala mzanzibari.

nakuunga mkono mkuu,

hata mimi nitabaki mtanzania daima.

Tanganyika siijui,
sikuzaliwa Tanganyika,
wakoloni ndio wanaoijua Tanganyika,
hii Tanganyika ilikuwa shamba la bibi kwa wakoloni,
ha wao wanjua kuwa hawatathubutu kuigeuza Tanzania koloni lao, haiwezekani
Tanzania ni huru na haijawahi kutawaliwa
Tanganyika na Zanzibar yote ni makoloni na hayajawahi kuwa huru
muungano ndio uliokamilisha uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Tanzania ni jina la kizalendo
tena linaakisi uhuru na azma ya kujitawala
tanganyika inaakisi utumwa, ukoloni, na unyonyaji

siipendi Tanganyika,
siipendi Zanzibar
napenda Tanzania
daima nitaililia Tanzania
Mungu ibariki Tanzania!!!

Angalizo kwenu wapendwa, Mwanaone na Miss Judith.

Jitayarisheni na heart attack!
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulizaa Tanzania baada ya miezi sita tokea kuundwa kwa Muungano. Kabla ya hapo mnajua jina la Muungano liliitwaje?
Baada ya Muungano ,Jina Tanganyika limeyeyushwa kinyemela!

Sasa vipi mnatarajia jina Tanzania litabaki na utanzania utabaki baada ya operation "East African Federation"?
Kama tutafuata utaratibu wa kubadilisha jina kama tulivyofanya kwa Muungano huu tulionao, basi Tanzania, itapata jina jipya la Afrikamashariki baravisiwani na uraia utakuwa Uafrikamashariki.

Kama hamtaki Tanganyika na Utanganyika, wala Zanzibar na uzanzibari... basi na Tanzania na utanzania utabaki kwenye historia tu kama ilivyo kwa jina Tanganyika leo.

Au hamfuatilii mwenendo na hatua za Muungano wa EAC?
 
kheri kuwa mwanafrica mashariki kuliko kuvunjika kwa muungano nicholilia mimi ndugu zangu ni umoja na si chingine.narudia tena kusema tutibu kasoro za muungano ili tuwe na muungano imara badala ya kuuvunja muungano . TUKIANZA KUSEMA SISI NI WATANGANYIKA KESHO TUTASEMA SI NI WAKSAKAZINI TUJIAMULIE NA WENGINE WATASEMA SISI WA KUSINI NA WAZANZIBAR NAO MWISHO WATASEMA SISI WAPEMBA NA HAWA NAO WATASEMA SISI WAUNGUJA. NA SIKU ZOTE UMOJA NI NGUVU UTENGANO DHAIFU. MIMI NAHISI TUWE NA BUNGE LA TANGANYIKA, TUWE NA BUNGE LA ZANZIBAR KAMA ILIVYO SASA NA TUWE NA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA. TUWE NA WIZARA MOJA YA MAMBO YA NJE, MAMBO YA NDANI , ULINZI. HIZI WIZARA TAU ZISITENGANISHWE. YAANI KWA UFUPI UPANDE WA TANGANYIKA WAWE NA MAMBO AMBAYO WATAJIAMULIA WENYWE NA ZANZIBAR WAWE NA MAMBO AMBAYO WATAJIAMULIA WENYWE LKN KUNA MAMBO NI LAZIMA YAWE NA MAAMUZI YA PAMOJA HUSUSANI KTK WIZARA HIZO TATU NILIZOZISEMA.
 
Muungano sio kero, ni matatizo. Kwa nini hatutumii Kiswahili fasaha kuelezea matatizo yetu?

Ninapoona Bunge limejaa wawakilishi kutoka Zanzibar tofauti na uwiano wao, hayo mabilioni ya kugharimia hawa wabunge wa kigeni ni kero au balaa?

Ninapoona waziri wa Zanzibar anatangaza hadharani kimabavu kwamba hatalipia Umeme wakati mimi Mtanganyika sithubutu kuikoromea TANESCO, hiyo ni kero au uonevu?

Ninapoona nusu ya mabalozi, mawaziri wa Muungano, viongozi wa vyama, wanatoka sehemu moja ndoooogo ya nchi, hiyo ni kero au upendeleo?

Ninapoona Zanzibar inaandika Katiba inayokinzana na Katiba ya Muungano na kutangaza unilaterally kufuta kitu fulani katika orodha ya mambo ya Muungano, hiyo ni kero au jinai ya dharau?

Ndio maana wengine tunasema to hell with the Muungano!

Taso.
Wewe na mimi tunaweza kusema "to hell with the Muungano!

Lakini huu muungano sio wetu. Ni Muungano wa Chama cha magamba na wenyewe hawataki ujadiliwe, bali uimarishwe tu.
Wameapa kuulinda Muungano na mapinduzi kwa vyovyote iwavyo!

We have to do more than saying "to hell with the Muungano!"

Mkuu.,
Sisi tunataka nchi moja na serikali moja....kwa maana nyengine tunataka kuifuta Zanzibar..huoni hii kuwalipa wabunge wa zanzibar na viongozi wao ni sawa tu ili lengo hili la nchi moja na serikali moja litimie?

Likishatimia, tutaanza kuhesabu faida tu...nchi kama Zanzibar ukiitia thamani utainunua kwa shillingi ngapi? So we buy it very cheap! Au tunaposema Zanzibar ni sehemu ya Tanzania maana yake nini?

Au msemo wa serikali mbili kuelekea moja umefutwa?
Tumeungana mambo kumi na moja, tunasema nchi moja...
baada ya kasheshe ya G-55 tumeambiwa sera ni kutoka serikali mbili kwenda moja...au?

Ni lazima kuingia gharama katika katika project hii ya nchi moja serikali moja , au vipi mkuu?
Au inawezekana kukamilisha project kubwa kama hii bila ya kuingia gharama?
Tatizo ni kuwa "viongozi wetu" wanafanya kila kitu ni siri, ni nyeti za serikali!

Na ndio unaona hawataki muungano uguswe au ujadiliwe!

Baada ya kusoma mchango huu, bado tutasema, "to hell with the Muungano?"
 
kheri kuwa mwanafrica mashariki kuliko kuvunjika kwa muungano nicholilia mimi ndugu zangu ni umoja na si chingine.narudia tena kusema tutibu kasoro za muungano ili tuwe na muungano imara badala ya kuuvunja muungano . TUKIANZA KUSEMA SISI NI WATANGANYIKA KESHO TUTASEMA SI NI WAKSAKAZINI TUJIAMULIE NA WENGINE WATASEMA SISI WA KUSINI NA WAZANZIBAR NAO MWISHO WATASEMA SISI WAPEMBA NA HAWA NAO WATASEMA SISI WAUNGUJA. NA SIKU ZOTE UMOJA NI NGUVU UTENGANO DHAIFU. MIMI NAHISI TUWE NA BUNGE LA TANGANYIKA, TUWE NA BUNGE LA ZANZIBAR KAMA ILIVYO SASA NA TUWE NA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA. TUWE NA WIZARA MOJA YA MAMBO YA NJE, MAMBO YA NDANI , ULINZI. HIZI WIZARA TAU ZISITENGANISHWE. YAANI KWA UFUPI UPANDE WA TANGANYIKA WAWE NA MAMBO AMBAYO WATAJIAMULIA WENYWE NA ZANZIBAR WAWE NA MAMBO AMBAYO WATAJIAMULIA WENYWE LKN KUNA MAMBO NI LAZIMA YAWE NA MAAMUZI YA PAMOJA HUSUSANI KTK WIZARA HIZO TATU NILIZOZISEMA.
Mkuu.
Una mawazo mazuri kama ya kwangu.
Mkuu.
Watanganyika wanautaka Muungano na wazanzibari wanautaka muungano. Hii ni kutokana na maoni ninayosoma juu ya mijadala ya Muungano huu.

Ambacho watanganyika na wazanzibari hawataki ni muungano usioeleweka. Muungano wa mazingaombwe, changa la macho au usanii.

Lakini njia nzuri ya kuthibitisha kauli yako ni kwa kuwepo mjadala wa wazi wa kitaifa juu ya muungano na muundo wake na pia kuitisha kura ya maoni.

kwa kuanzia, ule mkataba halisi wa muungano inapasa kutolewa hadharani ili wananchi washuhudie ni nini hasa kilikubaliwa kwa kuanzia.

Lakini mimi baada ya kuisoma hii makala
https://www.jamiiforums.com/tanzani...ibar-kuchoshwa-na-muungano-7.html#post1891556

Na kuona idadi ya tume na kamati na kwamba hakuna kinachofanyiwa kazi katika mapendekezo yao ili kutatua matatizo ya Muungano...Ni wazi kuwa VIONGOZI ndio tatizo letu kuu!
 
Hata mimi nitabaki mtz, tz inaweza kubaki hata bila ya znz kwa kuwa hilo ni jina tu ndio maana kuna neno "nia" ambalo liliwekwa kukamilisha jina.

Huyo anayesema znz kwa kuwa inabendera,bunge,mahakama nk basi znz ni nchi ni mvivu wa kufikiri na hajui ni vigezo vipi vinatakiwa ili kuifanya znz nchi ktk masuala ya kimataifa.

Kwa taarifa yake znz kimataifa sio nchi na wala hakuna anayeijua znz ni nchi huko nje,na kama anabisha asafiri nje ya nchi kama ataiona bendera ya znz nchi za nje zaidi ya bendera ya tz, kama atasikia wimbo wa nchi ya zanzibar ukipigwa zaidi ya wimbo wa taifa la tz, kama ataona ubalozi wa znz zaidi ya ubalozi wa tz, kama ataona passport ya znz zaidi ya passport na visa ya tz, kama atakutana na mtu anayejitambulisha mznz zaidi ya mtu anayejitambulisha kama mtz nk.Kwa hiyo znz kuwa na bendera,wimbo wa znz maana sio wa taifa,mahakama na bunge nk hauifanyi znz kuwa na hadhi ya nchi kimataifa, hayo ni mambo madogo sana ambayo siyo sifa ya kuwa nchi.

USA na Canada imeundwa na states na provinces ambazo zinabendera ,mahakama, bunge, nyimbo nk lakini hazina hadhi ya nchi , nchi ni USA na Canada.
 
Hata mimi nitabaki mtz, tz inaweza kubaki hata bila ya znz kwa kuwa hilo ni jina tu ndio maana kuna neno "nia" ambalo liliwekwa kukamilisha jina.Huyo anayesema znz kwa kuwa inabendera,bunge,mahakama nk basi znz ni nchi ni mvivu wa kufikiri na hajui ni vigezo vipi vinatakiwa ili kuifanya znz nchi ktk masuala ya kimataifa.Kwa taarifa yake znz kimataifa sio nchi na wala hakuna anayeijua znz ni nchi huko nje,na kama anabisha asafiri nje ya nchi kama ataiona bendera ya znz nchi za nje zaidi ya bendera ya tz, kama atasikia wimbo wa nchi ya zanzibar ukipigwa zaidi ya wimbo wa taifa la tz, kama ataona ubalozi wa znz zaidi ya ubalozi wa tz, kama ataona passport ya znz zaidi ya passport na visa ya tz, kama atakutana na mtu anayejitambulisha mznz zaidi ya mtu anayejitambulisha kama mtz nk.Kwa hiyo znz kuwa na bendera,wimbo wa znz maana sio wa taifa,mahakama na bunge nk hauifanyi znz kuwa na hadhi ya nchi kimataifa, hayo ni mambo madogo sana ambayo siyo sifa ya kuwa nchi.USA na Canada imeundwa na states na provinces ambazo zinabendera ,mahakama, bunge, nyimbo nk lakini hazina hadhi ya nchi , nchi ni USA na Canada.
Mkuu.
Hapa umetoa maelezo mazuri sana na mifano mizuri sana wakati huo huo ulichokisema ndio penye matatizo.
Sasa huyu Zanzibar yupo, je mbia mwenzake yuko wapi?
Kama tutachukulia kuwa State of Zanzibar na state of Tanzania bara(Tanganyika)?
Hii iko wapi? Umewahi kuisikia hata hapa TZ wacha nje... kama hatuna haki ya kuwa na state of Tanganyika basi hata jina pia hatuna haki ya kubaki nalo?

Hata kwa wale wanaotoa mfano wa UK, kusema kuna serikali ya Muungano ambayo pia ni ya England...lakini England ipo, hapa TZ, Tanganyika imeyeyushwa!

Lakini pia kuna habari hii,
Hata hivyo, mwaka 1964 makubaliano ya kimyakimya yalifikiwa kati ya nchi nne - ambazo ni Kenya, Tanganyika, Uganda na Zanzibar – kuungana chini ya uongozi wa Kenyatta. Kama ilivyoelezwa, Nairobi watu walikwenda kulala wakitegemea kuwa siku ya pili Kenyatta atatangaza shirikisho. Hili halikutokea. Wengi wakikisia kuwa walikuwa Charles Njonjo na Bruce Mckenzie waliomwelekeza Kenyatta asiendelee na shirikisho. Kwa hiyo ilikuwa katika wakati huo ambao Nyerere – aliyependelea Zanzibar iingie katia Shirikisho la Afrika Mashariki, akihisi kuwa chaguo ambalo lingeliuzika zaidi Umoja wa Mataifa – ni kukubalina na Karume, kuunda Muungano. Ni katika dhana hii ndiyo Muungano unaweza ukasemekana kuwa ni matokeo ya jaribio lililoshindwa la kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki.

Hili lilithibitishwa na maelezo mingine kuwa, kabla ya mapinduzi ya Zanzibar, Muungano ulizungumzwa kwa namna ya shirikisho tu. Ni kweli kuwa mara baada ya Zanzibar kupata uhuru wake mwaka 1963, Tom Mboya alitembelea Zanzibar ambayo iliunga mkono shirikisho kwa maneno matupu bila ya kuupinga kwa nguvu kama ilivyofanya Uganda.

Kwa majaribio ya shirikisho lililoshindikana, pamoja na wasiwasi wa nchi za Afrika Mashariki ambazo zote zilikwisha jadiliana juu ya uhuru wao, matokeo mabaya ya mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na uasi wa majeshi katika nchi tatu za Afrika Mashariki mwaka huo huo, mtu anaweza kuelewa kuhusu uhusiano kati ya shirikisho lililoshindikana na Muungano wa nchi mbili, na kwa nini Muungano haukuhojiwa katika Afrika Mashariki ambayo imelikataa shirikisho, kwa upande mwingine.

Katika muktadha huu, ilielezwa waziwazi kuwa nchi za Afrika Mashariki zina wasiwasi kuwa Zanzibar inaweza kutumiwa na madola ya nje kuiyumbisha kanda yote. Shirikisho ndani ya shirikisho Ukurasa 92-94
 
Tanzania haiwezi kukwepa historia! Miungano yote ya kulazimisha inapata kifo cha asili. Iangalie USSR Kuanzia vita vikuu vya 2 Hadi 1990 au Yugoslavia chink ya Tito iliyogeuka kuwa nchi Saba za eneo la Baltic. Kwa hapa Africa angalia iliyokuwa Senegambia sasa hivi kuna Senegal na Gambia. Mambo ya muungano hayapaswi kulazimishwa bali watu waingie kwanhiari baada ya referandum.

USA ina muungano wa tofauti ambapo zile states ziliunganishwa kwenye umoja kwa civil wars zilizodumu kuanzia 1776 mpaka mwamzoni mwankarne ya 18. Lakini zile states Zina autonomy kubwa kisiasa na kiuchumi. Status ya Gavana wa California Schwazznegger yaweza kuwa kubwa kuliko hata PM wa Uingereza

Rekebisha kumbukumbu zako Arnold Schwatenegger ni Governor wa California kwa sasa.

Pili umeizalilisha Uingereza kuandika Governor wa state ya US ni mkubwa kuliko Primier wa Great Britain, hujui madaraka ya Primier, kama ungejua the Monarch is just a celemonial post na mtendaji mkuu wa serikali ni PM wala usingeandika hivyo. PM anaweza akainitiate na kuenfluence UK ikaenda vitani na huteuwa mawaziri nyeti kama foreign minister na finance minister wa UK na wala si huyo Governor unayemwandika ambaye hana influence yoyote ya foreign policy wala hata influence katika State nyingine ya Marekani.

Vilevile wakati wa Uhuru wa Marekani kuna state ambazo zilitaka kuwa na Uhuru wa kwao kama vile Texas lakini zililazimishwa kuwa ndani ya US, so ubavu pia ulitumika kuunda Taifa la Marekani kama wazanzibar wanavyodai na wala si kweli muungano wa state za marekani ulikuwa kwa hiari ya State zote.

Wakati mwingine part moja ya nchi inaweza ikawa inagoma kuwa ndani ya muungano kama wazanzibar wanavyogoma kwa sasa lakini zikalazimishwa kufuatana na masilahi flanflan, kama wazanzibar kwa sasa. Nakutolea mifano:-

Finland mpaka imeunganishwa na Kisiwa cha Aland ambacho wakazi wake karibu wote wanaongea Kisweedish, wakati majority ya raia wa Finland wanaongea Finnish. Katika kuwaaccomodate wakazi wa kisiwa cha Aland, Finland iliamua kuweka Kisweedish na Kifinnish kuwa lugha zote za Taifa, wakazi wa Aland walipenda zaidi wawe raia wa Sweden kwani ndio asili yao na lugha yao inazingumzwa sana huko lakini uamuzi haukukubalika.

Pia eneo la Alsace and Lorraine nchini Ufaransa wakazi wake wanaongea kijerumani na wana asili ya Ujerumani na wangependa wawe raia wa Ujerumani lakini kufuatana na historia ya vita vya dunia wala hiyo hawana hio uwezo na Ujerumani inamezea mate hilo eneo bila mafanikio hata Hitler alijaribu kulirudisha alishindwa

Eneo na Tirol nchini Italia wakazi wake wengi wanaongea kijerumani na wangependa wawe raia wa Austria kwa kutangaza eneo nao kuwa si mali ya Italy lakini imeshindikana. Mifano ni mingi pamoja na nchi kama Hispania kumiliki visiwa vya Canary na Puetro Rico kuwa chini ya Marekani.

Ni vizuri kuona wachangiaji wengi wa maada ya Muungano especially Wazanzabar wanakiri kuwa huu muungano wa Tanzania haukuwa wa hiari, kama Mh Makaimati na wengine kuwa kilikuwa kitendo cha nchi moja kubwa, i.e Tanganyika kuivamia na kuiteka Zanzibar. Kama ndio hivyo basi basi huu muungano wala hauwezi kufa kwani hiyo nchi ndogo kujitoa ni vigumu kama mifano iliyotolewa hapa juu. Na kwa misingi hiyo ya uvamizi wala huwezi linganisha muungano wa Senegar na Gambia kwani inaonekana wazi nchi zote mbili wadau wa ule muungano walikuwa na nguvu sawa ndio maana walijitoa kirahisi.

Siwezi kuanza kulingalisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar kama ule wa Yugoslavia ya zamani hata Urusi kwani baada ya kufa comminism sioni tofauti yoyote ya wakati wa ukominist na sasa.

Mwisho hii kwa wanzanzibar waelewe kwamba muungano hauwezi kufa kirahisi kama mnavyodhani, miaka 47 baada ya muungano kuna wazanzibara (Wazanzi-tanganyika) wengi wamezaliwa na wapo huko Unguja kuna sheria za kimataifa ambazo mtalazimishwa mzifuate ili kuwalinda hao watu, kwani ni wazanzibar kama ninyi (hao watakuwa Wazanzibar but with Tanganyika as their kin-state). Na hao pia wataendeleza influence za Tanganyika huko kwani wanaweza wakapewa hata uraia wa Tanganyika pale ambapo kutakuwa na duo-Nationality upande wa Tanganyika.

Ukifuata hiyo philosophy ili kurespond hiyo hali ni either mtaruhusu raia wa nchi zingine kama Oman kwani huko ndiko kuna ndugu zenu wengi muwape uraia na matokea yake mtakuwa wasaidizi kwenye nchi yenu wala hiyo soreignity mhayoitafuta mtaisikia ndotoni. Tanzania ni signatory wa UN and AU charter for minority rights na wakati mwingine ni bora tu kuuwa muungano kama wenzetu mnavyotaka, Tanganyika itabaki na influence yake Zanzibar kwa kupitia hao wanzanzibara watakaolindwa na hizo sheria za kimataifa kama bado inaihitaji Zanzibar na pia Zanzibar itawakilishwa Wazanzibar wataobaki bara kama itakuwa na uwezo wa kufanya hivyo
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom