VodaFasta wamegeuka Matapeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VodaFasta wamegeuka Matapeli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndallo, May 23, 2011.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,133
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  WanaJF nawaomba mjihadhari na baadhi ya hawa wanaojiita VodaFast nikimaanisha hawa jamaa wanaokurushia muda wa maongezi barabarani! natoa ushauri huu kwakua yamenikuta na hii ni mara ya pili kwa mimi kufanyiwa utapeli huu.

  Hawa jamaa unapokutana nao na kumpatia kiasi cha hela ili akurushie muda wa maongezi wanakuambia salio linaingia kimyakimya lakini baada ya kuachana nao unapokujakutaka kupiga simu unakuta hakuna salio lililoingia na ukisema umtafute kwa muda huo unakuta kapotea machoni mwako sijui wanatoweka vipi! kweli yamenikuta na pia natoa ushauri wangu kwenu wanaJF kujihadhari na utapeli huu unaoendelea mjini.

  Watu hawa huwezi kuwategemea kabisa kama wanaweza kufanya utapeli huu mimi mara ya kwanza nilitapeliwa na mwanamume na mara ya pili huyu alikua ni mwanamke tena kwakumkumbuka machoni mwangu ni mtu wa heshima tu tafadhali wanaJF kaeni chonjo na utapeli huu.

  Ushauri wangu kuanzia leo mwambie huyo VodaFasta akurushie muda wa maongezi hakikisha salio lako limeingia halafu toa pesa, kwangu mimi sikufuata ushauri huu kwakua machoni mwangu hawa jamaa wanaonekana ni watu wastaarabu machoni lakini kumbe ni chui waliovaa ngozi ya Kondoo. Please wach out!
   
Loading...