Vodacom wawaombe radhi wateja wake

May 24, 2012
54
10
Katika hali ya kushangaza zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuzimwa kwa simu zisizosajiliwa(01/06/2013) imeonekana simu nyingi sana zimesajiliwa usajili wa awal,i na wateja wanatakiwa kwenda kupanga foleni tena ili kukamilisha usajili.

SIMU YANGU NILIISAJILI TANGU MWAKA 2010, LAKINI NIMEANGALIA LEO NAONA NAAMBIWA SIKUKAMILISHA USAJILI.
Je! huu siyo uzembe wao na kutusababishia usumbufu? Na wengi hawajui hili, HEBU NA WEWE MWANA JAMVI ANGALIA SIMU YAKO KWA KUPIGA *106# UONE KAMA UMESAJILIWA AU LA. Ni wengi sana wamekutanana kadhia hii. Kwahili VODACOM mnapaswa kutuomba radhi kwa usumbufu.
 
Nimesajiriwa!!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
aseee ebu ngoja nicheki,hasa sie tulisajiliwa kwa kufatwa
asante
 
Wananiambia sijasajiliwa, ngoja nikatoe mshiko wangu kwenye M-Pesa wakinifungia basi wamenipoteza kama Mteja wao.
 
Najiuliza sijui jina langu linatokea kwenye mpesa walilitoa wapi maana wananiambia sijasajili laini yangu.
 
Katika hali ya kushangaza zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuzimwa kwa simu zisizosajiliwa(01/06/2013) imeonekana simu nyingi sana zimesajiliwa usajili wa awal,i na wateja wanatakiwa kwenda kupanga foleni tena ili kukamilisha usajili.

SIMU YANGU NILIISAJILI TANGU MWAKA 2010, LAKINI NIMEANGALIA LEO NAONA NAAMBIWA SIKUKAMILISHA USAJILI.
Je! huu siyo uzembe wao na kutusababishia usumbufu? Na wengi hawajui hili, HEBU NA WEWE MWANA JAMVI ANGALIA SIMU YAKO KWA KUPIGA *106# UONE KAMA UMESAJILIWA AU LA. Ni wengi sana wamekutanana kadhia hii. Kwahili VODACOM mnapaswa kutuomba radhi kwa usumbufu.

kwakwel wadau mimi niliivunja laini yangu ya voda baada ya kuambiwa kuwa lain yangu haijasajiliwa,maana nimeisajili by miaka mitatu nyuma nakumbuka hiyo laini niliinunua maeneo ya ubungo kwa sh 100 kisha nikaisajili mwananyamala,,,,,sitatumia tena voda wapuuz hao,hawawez kunipanga foleni kwa tukio lilelile
 
Siyo voda peke yake wakuu, hata tigo na Airtel nao ukiangalia wanakwambia usajili wako haujakamilika, utakamilika fomu yako itakapo2fikia
 
Tatizo wale watu wanaowaweka kwa ajili ya usajili hawapeleki zile taarifa zetu...zile copy za vitambulisho na nini huwa hawazitumi/ au hawazitunzi..
 
You are fully registered as BELINDA JACOB. Thank you.
Pheeeew! Afadhali maana ingekuwa usumbufu mwingine.
 
Back
Top Bottom