Vodacom Watoa Number ya Bure Kuwasilisha Kilio Cha Mazingira! Tutume Maoni Yetu!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vodacom Watoa Number ya Bure Kuwasilisha Kilio Cha Mazingira! Tutume Maoni Yetu!.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, Nov 7, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,217
  Trophy Points: 280
  Wanabodi ambao ni wakereketwa wa mazingira,

  Someni Hapa!.

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Novemba 2011

  Mabadiliko ya tabia nchi: Je nini maoni yako? Unafikiri yataiathiri vipi Tanzania? Na serikali ya Tanzania ifanyeje katika kukabiliana na tabia nchi?

  Hii ni nafasi yako kuongea moja kwa moja na serikali kuhusu mabadiliko ya tabianchi

  Chukua nafasi hii kuwasiliana kupitia ujumbe mfupi wa maandishi BURE na Idara ya Mazingira ya Ofisi ya Makamu wa Rais

  Kwa wateja wa VODACOM pekee

  Nini Mabadiliko ya Tabianchi?

  Mabadiliko ya tabianchi ni moja ya changamoto kubwa kwa dunia ya leo. Inaathiri kila mmoja, ikiwa ni pamoja na WEWE- ni tatizo la dunia lenye madhara hadi kwako.

  Je, mabadiliko ya tabianchi yana maana gani kwako? Katika Tanzania athari zionekanazo kwa haraka ni ongezeko la matukio ya hali mbaya ya majira, kama mafuriko na ukame. Pia ina maana ya hali ya majira zisizokuwa na uhakika zaidi, na hatutaweza kuwa na uwezo wa kutabiri kwa usahihi mvua au ukame, na joto litaongezeka. Kuna hatari ya kupanda kwa ujazo wa bahari ambayo inaweza kutishia maeneo ya pwani. Yote haya yatakuwa na madhara juu ya afya ya watu na vile vile katika kilimo na usalama wa chakula - kwa mfano kushindwa kwa mazao, kuenea kwa malaria, shinikizo juu ya usambazaji wa maji.

  Je, dunia inafanya nini kuhusu hili suala?

  Kila mwaka serikali za dunia hukutana kujadili mabadiliko ya tabianchi, matatizo na athari, na kujaribu kukubaliana juu ya njia bora ya kushughulikia changamoto hii na kutatua tatizo hili kwa haki. Mikutano hii hufanywa na UNFCCC (Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mfumo wa Mabadiliko ya Tabianchi) na huitwa Mkutano wa pande zinazohusika. Mkutano wa17 (COP17) utafanyika Durban, Afrika Kusini kuanzia tarehe 28 mwezi Novemba mwaka huu.

  Kuwa na mkutano wa COP17 katika ardhi ya Afrika ni nafasi kubwa ya kupata sauti ya Afrika katika mjadala wa kimataifa. Afrika imesababisha kidogo sana tatizo hili lakini itaathirika zaidi na mabadiliko ya tabianchi na ni muhimu kwa mataifa ya Afrika kupaza sauti zao wasikike. Tanzania na nchi nyingine za Afrika zina haja ya kufanya kazi kwa pamoja, pamoja na nchi nyingine kama vile Uingereza na nchi za Umoja wa Ulaya. kukubaliana njia ya kutatua tatizo hili na kuboresha maisha ya kila mtu

  Ninaweza kufanya nini kuhusu hili tatizo?

  Kuna mambo mengi tunaweza kufanya ili kusaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi - kubadilisha njia ya maisha yetu, jinsi tunavyofanya kazi, jinsi tunavyosafiri ... Tunahitaji kujifunza jinsi ya kukabiliana na hayo mabadiliko, jinsi ya kukabiliana na matukio hayo ya hali ya majira iliyo duni, jinsi ya kutekeleza mikakati shujaa kwa ajili ya kilimo, jinsi ya kuendeleza mawazo ya biashara kijani ... na mengi zaidi!

  Nini unataka kujua?

  Hii ni nafasi yako ya kuuliza serikali yako moja kwa moja! Matatizo gani mabadiliko ya tabianchi yamekusababishia? Je, umeathirika na mwelekeo wa hali ya hewa usiotabirika? Mazao ya jadi yameanza kushindwa? Je, unatafuta mawazo ya kuimarisha uwezo wa familia yako kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi? Ni nini unataka kujua kuhusu msimamo wa Tanzania katika mazungumzo ya kimataifa ya Mabadiliko ya tabianchi jijini Durban? Unafikiri nini serikali yako iseme kwa dunia kuhusu mabadiliko ya tabianchi? Ni nini Tanzania idai?

  Tuma neno “MT” na swali lako kwenda namba 15300 bure! Maswali yatakusanywa na
  Dk. Julius Ningu Mkurugenzi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais
  atajibu maswali YAKO!
  Imeungwa mkono na Vodacom Tanzania na ForumCC.org, na kufadhiliwa na UKAID

  Kama kuna yeyote mwenye maswali, maoni au mapendekezo,

  Wasiliana na Dr. Ningu bure kupitia sms ile.

  Pasco.
   
 2. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2013
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Kujibu maswali, mikutano makongamano nk havitasaidia kuokoa mazingira yetu, tunataka action on the ground ili kukomesha uchafuzi unasababishwa na viwanda, kilimo na magari. Sheria zipo, conventions treaty na declarations za kimataifa zipo mbona hazitumiki kuzuia uharibifu wa mazingira?!
   
 3. Wapoti

  Wapoti JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2013
  Joined: Aug 28, 2013
  Messages: 2,824
  Likes Received: 417
  Trophy Points: 180
  Voda waache ujinga wanajifanya kutoa number ya bure wakati ni makato wanayotuibia ndio yanalipia hiyo number
   
Loading...