Vodacom waondoa bundle za siku na wiki?

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,741
6,432
Kila nikiingia #149*01# spati menu ya bundle ya wiki au siku kwa option ya voda to voda au voda to others.matokeo yake naona monthly bundles.je wamekuwa wanasiasa
 
Voda ni ovyo tu kwasasa, kuna ndugu yangu jana kahangaika kutoa pesa M_pesa wala hajafanikiwa hadi leo. Yaani voda ni Jipu ndg yangu!
 
Dah!!! Ngoja nichungulie maana hiyo ya mwezi wanaiba sana data na kuisha hata wakati mwingine wiki 3 hazifiki. Ila ya wiki mtu unaifatilia vizuri so hawachakachui kivile...wanaogopa utawajua haraka.

Mie naweka limit ya data usage kwa simu kila napojazia inasaidia kujua mambo yapo poa.
 
Ukiondoa tanesco, dude lingne linalokamua watanzania ni mitandao ya simu ikifuatiwa na mabenki
 
Teh! Kwani mlivyoambiwa mtaisoma namba mlikuwa wapi? Teh! Huku tunapoelekea naona mfumo wa barua unarudi taratibu! He he he!
 
Voda ni ovyo tu kwasasa, kuna ndugu yangu jana kahangaika kutoa pesa M_pesa wala hajafanikiwa hadi leo. Yaani voda ni Jipu ndg yangu!
Mimi mmoja wapo, nimeweka hela kwa wakala kwa wakala hela imekuja kwangu, kwangu haijafika, tumepiga simu ili kujua nini tatizo wanasema hela iko hewani, watairudisha kwa wakala aitume upya, utafikiri mimi na wakala tunakaa pamoja
 
Ipo mkuu, maybe hujaguswa Voda muda mrefu, sema unataka kifurushi gani nikuelekeze.
 
Na nanyi tumeshawachoka na mavodacom yenu humu ndani,.Mliambiwa ukiona mtandao mmoja haukufai tafute mtandao mwingine wenye naafu hao sio mama yako wala mke waki.

HAMIA HALOTEL MB 600 SH 500 KWA WIKI.
 
Back
Top Bottom