MotoYaMbongo
JF-Expert Member
- Jan 7, 2008
- 2,146
- 887
Naombeni ushauri jamani, Vodacom wamefunga laini yangu ina Pesa, nimewapigia customer care wakasema ilisajiliwa usajili wa muda, wakataka namba ya kitambulisho, Jina langu, Tarehe, Mwezi na Mwaka wa kuzaliwa nikawapa, wakasema ndani ya masaa 24 itakuwa tayari yakapita hamna kitu. Nimehangaika nao kwa siku 8 ikiwamo ya leo bado hamna kitu, kila siku naambiwa subiri ndani ya masaa 24, nimekwenda Voda shop Tabora mjini, nikatakiwa vielelezo nikawapa, wakasema tayari wamepeleka idara husika, nikaambiwa ndani ya masaa 24 yakapita hamna kitu. nikarudi tena hali ikawa ileile. Hadi nimechoka Voda wamenichosha kwa kweli. Jamani naombeni ushauri nifanyeje, Hela zangu zimo katika laini hiyo, shughuli zangu zimekwama.