Vodacom wamelipa kodi serikalini shs 700 billion?

Kuna kitu kimenistua sana kuhusu waandishi wa habari. Naweka habari yote toka mwananchi na Tanzania Daima. Habari zinafanana utadhani zimeandikwa na mtu mmoja. Nani ameendika hii habari? Na hakuna jina la mwandishi kwa magazeti yote mawali! Kuna nini hapa?


Gazeti la mwananchi
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania inatarajia kuchangia jumla ya Sh130 bilioni kama malipo ya kodi kwa katika mwaka wa fedha 2012/13.

Malipo hayo yataifanya Vodacom kufikisha zaidi ya Sh700 bilioni ilizokwishalipa kama kodi tangu mwaka 2001.

Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini hapa, baada ya kukutana na Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza alisema malipo ya kodi kwa serikali yamefikia zaidi ya asilimia 60 ya jumla ya uwekezaji wa Vodacom wa Sh 1.13 trilioni tangu mwaka 2001.

Meza alisema kampuni yak ina mipango wa kutumia zaidi ya Sh120 bilioni katika kuboresha mtandao, huduma na maendeleo ya uanzishwaji wa teknolojia mpya katika mwaka wa 2012.

Alisisitiza dhamira ya kampuni hiyo katika kuendelea kulipa kodi ipasavyo kwa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA)

“Hivi punde tumeboresha mtandao kwa zaidi ya Sh100 bilioni kufikia mwishoni mwa Machi 2012, na tunao mpango wa kuwekeza zaidi ya Sh120 bilioni ili kuendelea kuimarisha mtandao wetu nchi nzima.

‘Vodacom pia imetengeneza ajira 450,000 ikiwa ni pamoja na za mawakala wa M- Pesa, wauzaji wa jumla na wadogo pamoja na waajiriwa wengine 450 wa moja kwa moja katika kampuni,” alisema Meza.

Aliongeza kuwa kampuni pia imetoa zaidi ya Sh3.4 bilioni kwa serikali kama mchango katika Mfuko wa Maendeleo ya Huduma za Mawasiliano Vijijini, wa kuisaidia jamii kuwa na mipango ya uwekezaji katika katika nyanja ya mazingira na wanyama pori, elimu, afya na ustawi wa jamii.


Gazeti la Tanzania Daima

KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, inategemea kuchangia jumla ya sh bilioni 130 kama malipo ya kodi katika mwaka wa fedha wa 2012/13.

Malipo hayo yataifanya Vodacom kufikisha zaidi ya sh bilioni 700 ilizokwisha lipa kama kodi tangu mwaka 2001.

Akizungumza jana baada ya kukutana na Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, alisema kuwa malipo ya kodi kwa serikali yamefikia zaidi ya asilimia 60 ya jumla ya uwekezaji katika shughuli zake kuanzia mwaka 2001 ambayo inafikia jumla ya sh trilioni 1.13.

Aidha, Meza alisema kampuni ina mipango wa kutumia zaidi ya sh bilioni 120 katika kuboresha mtandao, huduma na maendeleo ya uanzishwaji wa teknolojia mpya katika mwaka wa 2012/13.

Meza alisisitiza dhamira ya kampuni hiyo katika kuendelea kulipa malipo yake ya kodi ipasavyo kwa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA).

“Hivi punde tumeboresha mtandao kwa zaidi ya sh bilioni 100 kufikia mwishoni mwa Machi mwaka huu, na tunao mpango wa kuwekeza zaidi ya sh bilioni 120 ili kuendelea kuimarisha mtandao wetu nchi nzima,” alisema Meza.

Aliongeza kuwa, Vodacom pia imetengeneza ajira 450,000 ikiwa ni pamoja na mawakala wa M-Pesa, wauzaji wa jumla na wadogo pamoja na waajiriwa 450 moja kwa moja na kampuni.

Kwamba kampuni pia imetoa zaidi ya sh bilioni 3.4 kwa serikali kama mchango katika Mfuko wa Maendeleo ya Huduma za Mawasiliano Vijijini, ikiwemo kuisaidia jamii na kuwa na mipango ya uwekezaji katika jamii kwenye nyanja ya mazingira, wanyama pori, elimu, afya na ustawi wa jamii.

Meza aliongeza kuwa, kupitia kampeni ya moyo ambayo ina lengo la kutokomeza fistula na uboreshaji wa huduma za afya kwa wajawazito nchini, Vodacom imewekeza zaidi ya sh bilioni 21 kutoka kampuni mama ya Vodafone na Vodacom duniani.

 
Madai yao Vodacom wamelipa hizo bilioni 700 toka mwaka 2001 hadi sasa...yaani ni kodi ya miaka 10 a

Kama ndivyo kwa nini jina la kampuni haliko kwenye orodha ya walipa kodi? Ofisi wa Waziri mkuu ilipata wapi taarifa iliyosomwa bungeni?
 
Kuna habari Michuzi blog inasema hivi:

"Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw Rene Meza akieleza jinsi Vodacom ilivyochangia zaidi ya
shilingi billion 700 katika malipo ya kodi ya serikali alipokutana na waandishi wa habari mjini Dodoma".

Tarehe 28/08/2011 Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisoma bungeni orodha ya makampuni 15 yanayoongoza kwa kulipa kodi;

1.TBL(Tsh bilioni 165.4)

2.NMB(Tsh bilioni 108.6)

3.TCC (Tsh bilioni 92.1)

4.NBC (Tsh bilioni 89.9)

5.CRDB Bank Ltd(Tsh bilioni 79.2)

6.Tanzani Ports Authority(Tsh bilioni 76.8)

7.Tanzania Portland Authority(Tsh 73.4 bilioni)

8.Airtel(T) Ltd(Tsh bilioni 63.6)

9.Tanga cement company Ltd(Tsh 43.6)

10.Standard chartered Bank Ltd(Tsh bilioni 40)

11.Citibank(T) Ltd(Tsh bilioni 35.7)

12.Resolute(T) Ltd(Tsh bilioni 32.1)

13.TICTS(Tsh bilioni 25.9)

14.Tanzania Distillers Ltd(Tsh bilioni 13.4)

15.Group five international(PTY) Ltd(Tsh bilioni 9.5)

Je, Inawezekana Waziri Mkuu alitumia wrong data? Maana kama Vodacom wamelipa kodi shs 700 billion walitakuwa wawe Number 1. Hapa kuna mkanganyiko.

Ni kuanzia mwaka 2001 to date ila nataka kujua kwani mwaka jana walilipa kiasi gani mpaka wasiwemo kwenye top 10 na mwaka huu wanapanga kulipa 130bil
 
da huu ufisadi bwana unaweza kucheka...sasa Kampuni mmoja wa big share holders ni Rosti Tamu alafu unategemea taarifa zitatolewa zilizo sawa bila kuchakachuliwa
 
Pius Msekwa ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Vodacom
Rostamu ni Shareholder...
Lowasa ni moja ya wadau wakubwa wa Vodacom maana ni mmliki wa Shivacom
sasa hapo wadau mnategemea kutakua na la maana zaidi ya ufisadi na uchakachuaji?
 
hahahaa, voda wazushi...! labda toka imeanzishwa, pia ieleweke kuwa wanaotoa hizo hela ni WATANZANIA watumiaji wa huduma za simu, na viongozi wanaona raaha kusikia hivyo wakati watu tupo over charged hizo rates za simu. Upuuzi mtupu
 
Ni tangu waanze kutoa huduma, lakini wenzao safaricom nchini kesho hicho ni kiasi wanachokusanya kwa mwaka mmoja

market share ya safaricom ni more than 80% kenya while vodacom ni 37% kama sikosei, huwezi fananisha revenue kwa hizo company 2
 
serikali siku zote hawana takwimu sahihi, ndo maana vodacom wameamua kuweka ukweli nje.on top of that exemption za kijinga jinga ndo zinawabeba hawa,!
 
VODACOM acheni wizi kama mwaka huu mtatoa 130 Bill mbona mwaka jana mlishindwa kutoa ata 9.4billion ili mshike angalau nafasi ya 16?
Ni vyema mtuambie mwaka jana mlichangia kiasi gani!
Otherwise kuna haja ya kuachana na huu mtandao usioleta tija kwenye uchumi wetu
 
Kuna habari Michuzi blog inasema hivi:

"Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw Rene Meza akieleza jinsi Vodacom ilivyochangia zaidi ya
shilingi billion 700 katika malipo ya kodi ya serikali alipokutana na waandishi wa habari mjini Dodoma".

Tarehe 28/08/2011 Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisoma bungeni orodha ya makampuni 15 yanayoongoza kwa kulipa kodi;

1.TBL(Tsh bilioni 165.4)

2.NMB(Tsh bilioni 108.6)

3.TCC (Tsh bilioni 92.1)

4.NBC (Tsh bilioni 89.9)

5.CRDB Bank Ltd(Tsh bilioni 79.2)

6.Tanzani Ports Authority(Tsh bilioni 76.8)

7.Tanzania Portland Authority(Tsh 73.4 bilioni)

8.Airtel(T) Ltd(Tsh bilioni 63.6)

9.Tanga cement company Ltd(Tsh 43.6)

10.Standard chartered Bank Ltd(Tsh bilioni 40)

11.Citibank(T) Ltd(Tsh bilioni 35.7)

12.Resolute(T) Ltd(Tsh bilioni 32.1)

13.TICTS(Tsh bilioni 25.9)

14.Tanzania Distillers Ltd(Tsh bilioni 13.4)

15.Group five international(PTY) Ltd(Tsh bilioni 9.5)

Je, Inawezekana Waziri Mkuu alitumia wrong data? Maana kama Vodacom wamelipa kodi shs 700 billion walitakuwa wawe Number 1. Hapa kuna mkanganyiko.

Mbona hata kampuni ya Geita Gold Mine inalalamika kodi iliyorekodiwa na Serikali inatofautiana na malipo waliyolipa wao?
 
Labda wamechangia Billioni 700 toka ilipoanzishwa , waandishi wetu maana huwa wanakurupuka tu kazi ku concentrate kwenye soda na biskuti za NICE za dezo.
 
We look like headless chicken kwa kweli kuna kiasi kampuni za madini wamelipa kama kodi but hakiko featured kwenye vitabu vya serikali.
Si uhuni huu jamani tena wa wazi wazi tena kama sikosei ni kama 300billion
 
Voda wamefanya press conference huko Dodoma baada ya kumaliza kikao na kamati ya mawasiliano! Tufuatilie mjadala wa bungeni tutajua ni kitu gani kimewapeleka wakubwa wa Voda bungeni!

Mbona nasikia haya makampuni ya simu hayalipi kodi inavotakiwa? au ndio maana mtoto wa makamba amewekwa pale ili kodi isilipwe vema? jamani tufike mahali tuwe wazalendo tuipende nchi yetu ili tusonge mbele, tuwaangalie wenzetu wa hali ya chini mahospitali vijijini, mashule jamani tuwe na moyo wa kizalendo tufikirie kuwa leo tupo juu kesho Mwenye ez Mungu anaweza kutuangusha wakati wowote ule !
 
Mbona kampuni za madini hazipo? na wale SONGAS?

Tusibiri pengine nao watafanya press conference na kutupa kiasi walicholipa! Hii nchi ni kama kichwa cha mwendawazimu na waandhishi wa habari hawatusaidii kabisa. Hapa watu wanauliza maswali very basic kwa sababu taarifa waliyandika hawa waandishi wa habari haitoi majibu zaidi ya kuweka kile walichopewa na Vodacom. Wangeuliza kwa mfano 'breakdown' ya hizo shs 700 billion kwamba kila mwaka walilipa kiasi gani tungepata mwanga.
 
Nadhani hiyo figure kwa vodacom ni kutoka imeanza kutoa huduma nchini

Moja; sio tu kutoka imeanza kutoa huduma ila ni kuanzia walipoanza kutoa huduma hadi mwisho wa mwaka 2013, yaani humo ndani wameweka hadi makadirio ya kodi watazolipa kwa mwaka 2012/2013 ambazo wanasema ni 120 bn.

Pili; sio tu kodi ila kila kitu walichowahi kutoa vodacoma (including zile pesa tulizochangia sisi wenyewe za fistula) zimejumlishwa humo, kama umewahi kumuona mwanvita anatoa magodor wakati wa mafuriko basi ujue nayo yamejumlishwa humu;

kwa hiyo walizotoa toka wameanza operations hadi sasa ni 700 - 120 = 580b

hawa ni wahuni tu!

hebu soma hii extract from corruption tracker, hii ilikua 2011

It is important to note that Airtel, which also leads in changing ownerships (another area that raises many questions), is the second largest in the country (with 5.9m subscribers).
Interestingly, a leading mobile phone company, Vodacom Tanzania Limited (with 10m subscribers), does not appear anywhere in the prime minister's list!

Commonsense shows that if Airtel with 5.9m subscribers can cough up 63.6bn/- in taxes, then Vodacom which has almost double the number of subscribers should be able to cough 127.2bn/- in taxes.
The question is why was Vodacom omitted from the prime minister's list? Or is it a question of the mobile phone company being a bad tax payer?

Surely, if Vodacom Tanzania Limited can readily give out its number of subscribers, in the same vein the government through the TRA should be able to tell the public how much the company coughed up in terms of taxes.

Even if the prime minister's list was intended to give the names of only big companies that were in the forefront in paying their taxes, there is no way Vodacom Tanzania Limited would have missed the boat.
 
Labda wamechangia Billioni 700 toka ilipoanzishwa , waandishi wetu maana huwa wanakurupuka tu kazi ku concentrate kwenye soda na biskuti za NICE za dezo.

hata kama ni toka wameanza bado wanapaswa kuona aibu, January makamba anasema mwaka 2010 peke yake hizi kampuni (kwa ujumla wake) zilitengeneza faida ya dola billioni moja, kwa hesabu hizo hizi kampuni zingehitaji kulipa USD300 million kwa huo mwaka ambayo ni around 450 billion TZS, sasa hizi ni jumla kwa makumpuni yote ya simu na kwa hesabu hizi na kuangalia market share ya voda unaweza kuona ni kiasi gani hawa jamaa wanatuzunguka

 
  • Thanks
Reactions: FJM

Similar Discussions

Back
Top Bottom