Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,245
- 100,021
Ngoja na mimi nikopi format ya hii barua kuna wajinga flani wananisumbua hapa job
Deal na kutajirika haraka haraka...halafu wenye mali waliamua vingine tunawaona wanga. Kitu cha msingi ni kwa muajiri kufuata taratibu zote za kisheria...ila duka la mtu ni la kwake tu. Anaweza kuamua lolote analotaka.
Waajiriwa wa Tanzania ndiyo chanzo cha yote haya kwa uzembe na wizi wao wa muda mrefu ambao wewe unataka kutudanganya tukubaliane na wewe kwamba ni mafanikio.
Mafanikio ni pale unapokopa benki unaanzisha mradi na unafanikiwa huku ukilipa kodi. Ukifanikiwa hapo hata sisi tutajipendekeza kukujua si kuja kukuomba hela za mafanikio yako, bali tutakuja kukuomba ushauri na ikibidi utufundishe jinsi ya kufanikiwa kama wewe.
Mwenzetu kaeleza suala la wizi na ufisadi wa vijana wa kitanzania kwenye makampuni haya. Sasa huo wizi na ufisadi utauitaje kuwa ni mafanikio? Yaani tukija kukuomba ushauri utushauri jinsi ya kuiba na kufisadi!!!! Wewe mtu wa ajabu kabisa hata kama lengo lako ni kutetea watanzania.
Topic yako ingebaki bila kuwepo wanaujua kinachoendelea ndani ya Vodacom, basi wengine tulishadanganyika na kuanza kufikiri kuitetea.
Lakini naona topic ya wizi na ufisadi wa vijana wa Vodacom haipingiwi na inaelekea ina ukweli, basi inatuwia vigumu kulitetea jambo hili na kama ilivyowekkwa na wenzenu tunatakiwa kuufuatilia mjadala huu kwa makini ili tujue lengo lake ni nini hasa kulileta humu JF.
Kama hawa mabwana ni wezi kama inavyoelezwa na wewe hupingi basi unatakiwa ku-balance crimes zote yaani hii ya expatriates na huo wizi ili kimoja kisifunike kingine.
Vinginevyo, usipofanya hivyo uka-biase kumoja tu, basi na wewe una ajenda yako.
Mheshimiwa sifanyi kazi NSN wala VODACOM,sijawahi kufanya kazi kwenye makampuni hayo mawili,nimeandika kwa kutazama uhalisia wa tatizo na sio kwa kuegemea upande wowote.
Umeandika kama mtu mwenye hasira kali na wafanyakazi wa vodacom,kutokana na mafanikio ya muda mfupi waliyoyapata,kutokana na hilo itakuwa ngumu kuijadili mada hii kwa mtazamo huru.
Sijaandika matukio ya wizi yasifanyiwe kazi,nimeandika kuwa kama NSN wanavunja sheria za nchi suala hilo lishughuikiwe mara moja,kwani baada ya muda waajiri wa kigeni watajifunza kutokana na yanayotokea NSN na kuendelea kuwakandamiza waajiriwa watanzania.
Ndilo tatizo letu watanzania. Mali ya wizi tunaiita mafanikio!!! Nilikuwa na hamu ya kujadili lakini sijadili tena.
Waajiriwa wa Tanzania ndiyo chanzo cha yote haya kwa uzembe na wizi wao wa muda mrefu ambao wewe unataka kutudanganya tukubaliane na wewe kwamba ni mafanikio.
Mafanikio ni pale unapokopa benki unaanzisha mradi na unafanikiwa huku ukilipa kodi. Ukifanikiwa hapo hata sisi tutajipendekeza kukujua si kuja kukuomba hela za mafanikio yako, bali tutakuja kukuomba ushauri na ikibidi utufundishe jinsi ya kufanikiwa kama wewe.
Mwenzetu kaeleza suala la wizi na ufisadi wa vijana wa kitanzania kwenye makampuni haya. Sasa huo wizi na ufisadi utauitaje kuwa ni mafanikio? Yaani tukija kukuomba ushauri utushauri jinsi ya kuiba na kufisadi!!!! Wewe mtu wa ajabu kabisa hata kama lengo lako ni kutetea watanzania.
Topic yako ingebaki bila kuwepo wanaujua kinachoendelea ndani ya Vodacom, basi wengine tulishadanganyika na kuanza kufikiri kuitetea.
Lakini naona topic ya wizi na ufisadi wa vijana wa Vodacom haipingiwi na inaelekea ina ukweli, basi inatuwia vigumu kulitetea jambo hili na kama ilivyowekkwa na wenzenu tunatakiwa kuufuatilia mjadala huu kwa makini ili tujue lengo lake ni nini hasa kulileta humu JF.
Kama hawa mabwana ni wezi kama inavyoelezwa na wewe hupingi basi unatakiwa ku-balance crimes zote yaani hii ya expatriates na huo wizi ili kimoja kisifunike kingine.
Vinginevyo, usipofanya hivyo uka-biase kumoja tu, basi na wewe una ajenda yako.
Acha kuropoka vitu usivyovijua. NImesoma barua yenyewe hapo juu hawa foreigners hawazidi 15. Wafanyakazi wa Vodacom na NSN ni wangapi? Barua inaishia kutaja foreginers tu bila kutaja ni percent ngapi ya staff wote!
Hakuna mtambo unaotengenezwa hapa Tanzania. Hivyo huwezi kukwepa foreigners ambao ndiyo waliobuni mitambo hiyo.
Labda inawezekana hujui kwamba fundi wa Tanzania kazi yake ni kuiangalia mitambo ikiharibika anaishia kukimbizana huku na kule kuangalia kimeharibika nini na kama ni kikubwa kuzidi ujuzi wake anamtaarifu aliyekitengeneza. Sasa, utakwepaje kuwa na foreigner.
Kama unataka watanzania wawe expatriates waambie ndugu zako huko NSN na Vodacom watengeneze mitambo yao uone kama kuna mgeni atanusa pua yake hapa nchini.
Hivyo, tatizo ni hao vijana wako wa Tanzania. Tatizo ni elimu yako Tanzania haitoi ubunifu hata wa kutengeneza toothpick.
Utalaumu nini katika hali hii.
Wewe haya madai yako yana proof gani. Barua yenyewe kwanza haina proof na hata haijulikani imeandikwa na nani!!
Bwana Mkazi,
Nimeongelea kwa kirefu biashara ya hawa mabwana kuandikisha majina ya ndugu zao umiliki wa viwanja vyenye minara hiii ya Vodacom. Hutaki kabisa kuongelea hili, kwa lugha ya sasa tunasema unalipotezea. Kwa nini ulipotezee.
Nina uelea mzuri kuhusu mambo ya viwanja. NImekwambia nina uweo wa kutaja majina ya staff wengi tu humo NSN na Vodacom wanaomiliki viwanja viliposimamishwa minara hiyo na kodi inaenda kwao. Hili sihitaji kufundishwa au kushauriwa. Ninaheshimu tu maadili lakini karibu asilimia kubwa ya vijana hawa wametajirika kwa uhuni huu.
Ndiyo maana siwezi kuuita ni mafanikio. Ni wizi.
Minara inatakiwa ikae mahala ambapo inaweza kutoa mawasiliano. Wewe unapeleka mnara kwa mjomba wako. Mjomba na wewe mnafaidika. Mnatajirika. Mkazi anasema hayo ni mafanikio na sisi tukiyaongelea unataka itoke picha kwamba tunaona wivu!
Sasa kama tunawaonea wivu basi huo ni mtazamo wako ambao hautunyamazishi kuusema ukweli huu. Lakini wenye mamlaka ya kuwaondoa wameona hilo ni tatizo na wanaliondoa kwa njia waliyoamua.
Sasa wewe utawabana kwa sheria gani.
Nimeuliza na hutaki kujibu. Unazungumzia kutaja mambo ya kiufundi wakati barua imetaja hadi menejiment na administrative posts. Taja watanzania mle Vodacom au NSN ni wangapi ili tujue, maana barua haitaji.
Kama ni kweli wamepeleka malalamiko yao jinsi ilivyo mimi siwezi kuwazuia maana Serikali kama ni kweli imeyapokea itayashughulikia.
Lakini kupeleka malalamiko haya hakuwafanyi wanaojua kilicho behind the scenes kusema wanachokijua.
Kimsingi wengine hatupendi kuwa kama sehemu ya kutumika kutetea uovu unapoanza kushughulikiwa. Ushuhuda wa wizi ndani ya Vodacom na NSN hauhitaji ushahidi kama wewe umekuwa mfuatiliaji wa kampuni hizi.
Uko wazi na ule unaoripotiwa magazetini kama wizi wa MPESA ni cha mtoto.
Kama Serikali yako haifanyia uthibiti kujua iweje mtu wa miaka minane kazini ana majumba matatu ya shs. milioni 80 kila moja, serikali ikaacha kufuatilia kwa mshahara wa kija huyo kayapataje haya, basi wawekezaji hawana security intelligence kama serikali na hivyo watafanya kilicho ndani ya uwezo wao.
Kilichomo ndani ya uwezo wao ndicho hiki walichoamua kufanya. Hawajavunja sheria lakini wametumia technique ya kuweza kufanyika kazi popote duniani. Kitu ambacho ni kawaida kabisa na nimeshataja huko nyuma.
Tanzania Hatuna Taratibu za kufuatilia uhalali wa vipato vya watu,mamlaka yetu ya Mapato haina weledi na uwezo kama wa IRS ya marekani,hivyo ni vigumu sana kuweza kuthibitisha mali za wahusika.
Tumeanza kuchukua hatua kurekebisha mfumo ili kuweza kufikia sehemu ambayo mali za mtu zinaweza kufahamika kirahisi,Mfumo bora wa Kodi,Urajisi wa ardhi,urajisi wa ukazi,urajisi wa mapato ya watu n.kmifuko ikikaa vizuri tutaweza kupambana na mafisadi pamoja na wezi wanaohujumu sehemu zao za kazi n.k
sijakataa kuna wizi kwenye makampuni,upo,ingawa mimi simfahamu mtu anayefanya kazi VODACOM na NSN,lakini ninachofahamu ni kuwa vyombo vyetu vya dola havina uwezo wa kupambana na wizi wa kimfumo bado.
binafsi msimamo wangu ni kuwa,kama kuna wafanyakazi wezi,washtakiwe,kama wewe una taarifa hizo zifikishe kwa viongozi wao huko VODACOM/NSN hapo utakuwa umesaidia kuondoa tatizo.
lakini kwenye hili suala la hawa jamaa wa NSN kuziba ajira za ndani kwa sababu ya wafanayakazi wezi ni kosa na wanapaswa walirekebishe
Kama anauhuru huo mwambie mwenye duka achague nchi siyo Tanzania
Ninachokifahamu ni kwamba wafanyakazi wengi Tanzania huwa hawana habari na na hawataki kabisa kusikia neno "haki zao".
Pia hawana habari na sheria. Tena ukiwatajia sheria hata kama ni sheria ya kazi basi wanakimbia na kukuacha kwamba "umeanza kutuletea mambo yako". Kwamba unawachelewesha kazi zao na unaletea siasa!
Ukitizama kwa undani unagundua kwamba hawataki kutetea haki zao kwa sababu kuna jinsi wanafaidika na waajiri hawa na hivyo wewe na sheria zako unawapotezea muda.
Sasa hawa waajiri wanaijua hali hii. Wanawadekeza kama wanawapenda staff wasiojua sheria lakini wakijua kabisa si productive ni watu wa kujipendekeza tu au ni watu wa kufisadi tu. Kumbe waajiri kimyakimya wanakuwa wanabuni njia ya kitaalamu ya kuondokana nao.
Hivyo, ukiona mfanyakazi wa Tanzania analeta vitu mtandaoni hivi na anataja sheria au vyombo vya sheria basi hapo ujue maji yamemfika shingoni kwa maana ya kwamba ama amekaribia kufukuzwa au kupewa redundancy!
Kwa hali hii mimi naamini kwamba kuna redundancy imekaribia kuwapata baadhi ya staff wa NSN au Vodacom na hivyo wanatafuta huruma huku mitandaoni.
Mtu kama mimi ni lazima niwe muangalifu kutetea jambo kwenye hali kama hii.
hapo kwenye red hapo....hii hapa mkuu...
COMPLAINTS ON FOREIGN EXPATRIATES
Mr. Eric Shitindi
Permanent Secretary
Ministry of Labor and Employment (MLE)
The United Republic of Tanzania
P.O. Box 1422
DAR ES SALAAM, TANZANIA
cc. George M. Masaju
Deputy Attorney General
Attorney Generals Chambers
The United Republic of Tanzania
cc. Mr. Mbarak M. Abdulwakil
Permanent Secretary
Ministry of Home Affairs
Government of Tanzania
cc. Mr. Eliezer Feleshi
Director of Public Prosecution (DPP)
cc. Mr. Robert Manumba
Director of Criminal Investigation (DCI)
Department of Criminal Investigation
Ministry of Home Affairs
cc. Dr. Edward Hoseah
Director General
Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB)
P O Box 4865
Dar es salaam, Tanzania
cc. Dr. K. W. D. Khomano
Director
Immigration Services Department
Ministry of Home Affairs
Mr. Permanent Secretary
Greetings
Re: Foreign Expatriates in Nokia Siemens Network (NSN) TANZANIA
We would like to table our complaints regarding unacceptable foreign expatriates employment practices at
NSN for your attention and appropriate action.
We understand that one of the important reasons for encouraging investments in our country is to create
and increase employment opportunities for Tanzanians. However, it is increasingly becoming a tendency
for foreign workers to get employment opportunities and sometimes to be preferred employees in position,
professions and jobs that many Tanzanians are qualified for and can do, and one such a case is to be
found in NSN. We would like to present the following issues for your attention:
2
1. The following foreign employees are some of the expatriates working at NSN in positions, jobs and
with expertise abundantly available among local Tanzanians, and they therefore reduce the
chances and opportunities of Tanzanians to be employed.
2. We doubt whether some of these foreign employees have genuine work permits that actually
reflects what they are doing, because of their tendency to leave the country for a few days, often
when their visas are about to expire and re-enter, and therefore getting visas extension and
thereby abusing Tanzanians hospitality.
3. The above employees, are some of those who have had extended stay in the country, and are
different from many who come on short term basis for projects that can be done by Tanzanians
4. Several times we have witnessed officials from immigration services department coming and
leaving in questionable circumstances which leads to rife speculations that there are probably
dubious and unethical practices going on to maintain and protect the status quo.
5. Employed Tanzanians are increasingly subjected to difficult working conditions and frustrations as
a strategy towards forcing them to resign and find the working environment unbearable, to give
room to more foreign employees especially from India to get employment opportunities.
6. It would be best to scrutinize the legality and viability of the contract between Vodacom and NSN,
and whether it does not breach respective laws of the land. Moreover, the said contract had
contravened many rights of local employees, as your investigations would certainly and more
specifically reveal.
7. The adopted NSN strategy which seeks to centralize its services through a global services
delivery approach is being implemented and the looming transfer of Network Operations functions
and other strategic measures being rolled out is set to render many local employees unemployed
and even curtail the prospects of future employment opportunities. These measures apart from
affecting immediate employees, they also have a long-term implication to the nation.
We hope your esteemed offices will choose to take this matter seriously and out of patriotism endeavor to
ensure that profound screening is carried out and appropriate subsequent measures undertaken.
Thanking you,
Tanzanian Employees
NSN Tanzania
Hapo penye bld inabidi waTZ tubadilike kwani inatujengea sifa mbaya ya WIZI.Ni kweli tumekuwa tukiwapa ajira watu wa nje kuliko hapaa nchini hiki kitu hakifanyiki sehemu nyingine duniani ila Tanzania. Lakini wakati nawatetea watanzania wapewe kipaumbele kwenye ajira nao inabidi waache tamaa za kutajirika haraka haraka kwani sasa wengi wamekuwa wezi juzi juzi tumesikia walivyoiba pesa m pesa na kwenye mabenki hii inawajengea hoja wale wasiotaka kuajiri watanzania kwani takwimu za uhalifu ziko polisi