Wizi unaondoa uhalali wa kila kitu. Dawa ya mwizi ni kurudisha kile alichoiba bila kujali ana madai gani mengine halali.
Kupitia mpangaji wangu nilikuwa nasikia mengi ndani ya Vodacom. Kuna mwaka mfanyakazi wa Vodacom alitekwa na gari huko Shinyanga na kidogo auawe. Watekaji naambiwa wakamwacha wakaenda na gari.
Kuna namna minara yenu ilikuwa inamulika gari hilo lilivyokuwa linakata mbuga kati ya Shinyanga na Mwanza na hatimaye kwa kutumia usalama wa Taifa mkalipata gari na watekaji. Kiongozi wa watekaji alikuwa anaitwa somebody Kisusi. Huyu Kisusi namfahamau wakati nimeishi Shinyanga na alikuwa ni mwanajamii mzuri pale Shinyanga na mchangiaji namba moja wa CCM. Tena si CCM tu, bali alikuw amchangiaji mzuri wa Kanisani.
Kumbe hela ile alikuwa anipata kwa biashara ile. Mbona Vodacom mlikasirika na mlitaka apewe adhabu ya kutosha bila kujali mchango wake katika jamii.
Wezi wa EPA hadi leo tanang'ang'ania wakamatwe waswekwe ndani. Hatusemi eti kwamba wezi wale tuwatetee madai yao mengine na tunajua wengine kama KAGODA tunasikia ni ma-shareholders wenu huko. Mwizi akishatoka gerezani ndipo na yeye afuatilie madai yake wengine.
Hivyo, huwezi kusema eti sasa kampuni inawashughulikia Vodacom na NSN kwa wizi wenu wa muda mrefu mtutake tuwatee wakati tukijua mnatuletea hoja mitandaoni ili kututumia tu ili muendelee kujineemesha na utajiri wa wizi mnaoufanya hapo Vodacom.
Wala msitudanganye mnatetea ajira za watanzania bali mnatetea ajira zenu tu. Hebu nikumbusheni. Ni lini ajira za Vodacom zilitangazwa magazetini? Maana yake inawezekana ajira zipo lakini nyinyi mliomo kwa ujanja hamtaki zitangazwe na mnachukuana ndugu zenu watakaowasaidia kufanikisha huo wizi wenu wa kuandikisha majina ya ndugu zenu kama wamiliki wa minara na kuiba mafuta ya magari ya kampuni hadi nasikia kwamba mnanyang'anywa magari yaliyokuwa yamejaa kama utitiri, bila kusahau wizi mwingi tele mnaoufanya hapo Vodacom.
Wanafiki wakubwa nyinyi? Ni lini Vodacom mmeshiriki katika mitando ya jamii katika masuala ya nchi? Kampuni yenu inapandisha gharama za simu kila leo lakini hatuwaoni wafanyakazi wa Vodacom mkijitokea kuetetea. Mko kimya ili muendelee kujenga majumba Mbezi Beach, mfungue shule za sekondari na hata chekechea.
Kama ninabisha basi tuleteeni list ya wenye viwanja vya minara ya Vodacom halafu tutaweka list ya wafanyakazi wa Vodacom wa zamani na waliomo sasa hivi halafu uone majina yanavyofanana baadhi.
Hivyo kinachofanyika ni kuondokana na uvivu na wizi wenu na wala si kuwaonea kwamba hakuna ajira. Kuna hotel hapa nchini zimeandikwa mlangoni kwamba BEWARE NOW YOUR IN AFRICA KEEP THE DOOR LOCKED. Maana yake ni kwamba ukiwa hapa Tanzania jiahadhari na ni kweli mnaonyesha.
Hebu semeni nyie wenyewe ni wangapi hapo wanatimuliwa kwa wizi wa mabilioni hapo Vodacom. Acheni za kuleta kujifanya mnatetea ajira za watanzania bali mnatetea ajira zenu.
Tena mnavyoodoka hapo kama mnavyoondolewa sasa basi kila mwajiri hapa nchini anatakiwa kuwa macho na wafanyakazi waliopitia Vodacom na hasa waliopitia ngazi za juu. Ni vijana wa juzijuzi tu, wamejifunza kuendesha gari juzijuzi tu ajabu haijapita miaka 10 lakini wana utajiri kuliko wa Lowasa. Wameupata wapi?
Si ni afadhali kuliko hata Lowasa ambaye hata alipokuwa hapa Wizarani hakuna rekodi inayoonyesha alifukuzwa au kuiba hata senti.
Keep it up NSN and Vodacom. FUkuza hawa mafisadi wadogo ili serikali ijifunze kufukuza mafisadi wakubwa.