Vodacom Premier League VPL | Ruvu Shooting Vs Simba SC | Uwanja wa CCM Kirumba

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Juni 3, 2021 ambapo Ruvu Shooting wanawakabili na Simba SC kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Simba SC anaingia kwenye dimba akiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza kwa bao moja kwa bila dhidi ya Ruvu Shooting.

Je, Maafande wa Ruvu Shooting wataendelea ubabe au Mnyama Mkali Simba SC atalipa kisasi kwenye mchezo huu wa VPL?

Usikose Ukasimuliwa..Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10: 00 Jioni.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.


===========

Wakati wowote mpira utaanza Uwanja wa CCM Kirumba

00' Naaaam mpira umeanza ni vita vya VPL | Ruvu Shooting 0-0 Simba SC.

10' Mchezo umeanza kwa kasi huku kila timu ikijaribu kusogelea lango la timu pinzani.

Shutiiiiii kali la Miquissone linapanguliwa na golikipa wa Ruvu na mabeki kusaidia kuokoa hatari ile.

17' Bocco Goooooooooooooaaal Goooooooooaaal

John Bocco anahesabu bao la kwanza akipokea pasi kutoka kwa Miquissone | Ruvu Shooting 0-1 Simba SC.

Difenda Juma Nyosso anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kucheza madhambi.

25' Ruvu wanamjaribu golikipa Aishi, kwa shutiiiiii mbaliiiii lakini anadaka bila wasiwasi na kuanzisha mashambulizi

32' Almanusura Ponera ajifunge baada ya krosiiiiiiii ya Kapombe kupiga kichwa katika harakati za kuokoa na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Mugalu anaonyeshwa Kadi ya Njano baada kumchezea faulo mchezaji wa Ruvu.

45+1' Kuelekea kuwa mapumziko Uwanja wa Kirumba, Nyoni kwake Manula, Simba wanawavuta Ruvu wasogee lakini Ruvu wanasoma mchezo

Naaaam mpira ni mapumziko Uwanja wa CCM Kirumba ambapo Simba SC wapo mbele kwa bao moja kwa bila

HT, VPL: Ruvu Shooting 0-1 Simba SC

45' Kipindi cha pili kimeanza CCM Kirumba huku Simba wakifanya mabadiliko | Ametoka Dilunga na ameingia Bernard Morrison.

55' Zuberi Dabi wa Ruvu Shooting anaonyeshwa Kadi ya Njano baada ya kumshika Mugalu.

Matumizi ya nguvu yanaongezeka. Shaban anaonyeshwa Kadi ya Njano baada kumkwatua Morrison.

61' Morrison anapiga krosiiiiiiii kwake Mugaluuuuuu Goooooooooaaal Goooooooaaal

Kope Mutshimba Mugalu anaipatia Simba SC bao la pili akipokea pasi murua ya Morrison. | Ruvu Shooting 0-2 Simba SC.

72' Juma Nyosso anaonyeshwa Kadi Nyekundu. Baada ya kuchezea madhambi Kapombe.

78' Ametoka Mussa na ameingia Santos upande wa Ruvu Shooting.. mpira unaendelea Simba wakitaka kuongeza mabao na Ruvu wakitafuta walau la kufutia machozi.

85' Anakwendaa Morrisooooon lakini golikipa Abdallah anamshika na kumwangusha eneo la 18. Ni Penatiiiii kuelekea Ruvu Shooting

Anakwendaa kupiga John Bocco Goooooooooooooaaal Goooooooooaaal

John Bocco anaipatia Simba SC bao la tatu kwa mkwaju wa Penati | Ruvu Shooting 0-3 Simba SC.

90+4' Kuelekea kumalizika kwa mchezo wa VPL

Naaaam mpira umekwishaaa ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya Ruvu Shooting.

FT, VPL: Ruvu Shooting 0-3 Simba SC

Ghazwat
 
Game ya Kwanza Clatous Chama hakuwepo Ruvu wakashinda, Leo pia Chama hayupo.

Tukumbuke kuwa mchezaji na Katibu wa zamani wa Yanga ndio Kocha wa Ruvu hivyo Simba leo inacheza na Timu mbili.

Kikosi Cha Simba vs RUVU.jpg
 
kikosi kitakachoanza leo Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Taddeo Lwanga (4), Hassan Dilunga (24), Rally Bwalya (8), John Bocco (22), Chris Mugalu (7), Luis Miquissone (11).


Wachezaji wa Akiba – Beno Kakolanya (30), Said Ndemla (13), Bernard Morrison (3), Mzamiru Yassin (19), Medie Kagere (14), Miraji Athumani (21) David Kameta (27).
 
Back
Top Bottom