Vodacom Premier League 'VPL' KMC FC dhidi ya Simba SC, Kazi Ipo Uwanja wa Uhuru

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League VPL, kuendelea kutimua vumbi leo December 28, 2019 ambapo KMC FC Kino Boys, kukinukisha na Mabingwa wa Nchi, Simba SC, Mnyama Mkali Mwituni, kwenye dimba la Uwanja wa Uhuru.

KMC FC, ambao ndo wenyeji wa mchezo huo kwa upande wao wanaingia uwanjani wakiwa na maumivu ya kupoteza mchezo wao wa VPL uliopita baada ya kuchapwa na Polisi Tanzania kwa mabao 3-2 hivyo kwa mechi ya leo KMC FC imejipanga kuhakikisha wanarejesha hali ya furaha.

Akiingia kwa mara ya pili ndani ya kikosi cha Simba, akishinda mchezo wa FA, kwa kuichapa Arusha United 6-0 na kuirarua Lipuli FC 4-0 kwenye VPL, kocha mkuu Sven Vanderbroeck, ameweka wazi kabisa kuwa kikosi chake kipo tayari kusaka alama tatu muhimu huku akiongeza kwamba, anahitaji kuona timu yake inapata ushindi kwa idadi kubwa ya mabao katika kila mchezo utakaochezwa ili kuweza kutimiza malengo klabu.

Nani kuibuka na ushindi? Dakika 90 zitaamua, Kumbuka mechi ni kuanzia saa 10:00 Alasiri..Usikose Ukaambiwa
tapatalk_1577531398885.jpeg
IMG_20191228_140657_515.jpeg


•••••••••=========••••••

Klabu ya Simba SC, imeibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya KMC FC kwenye dimba la uhuru.

Ikicheza kandanda safi la kuvutia na pasi za hapa na pale, Simba walianza kuhesabu bao la kwanza dakika ya 46 lililofungwa na Deo Kanda

Wakati mechi ikikisiwa kuwa itakuwa 1-0, Greson Fraga alipigilia msumari wa mwisho kwa kuongeza bao la pili kunako sekunde za jioni kabisa 90+3..

Kwa matokeo hayo Simba SC imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa VPL kwa alama 31 kwa michezo 12

FT: KMC FC 0-2 Simba SC
 
05' mpira umeanza kwa kasi huku kila timu ikijaribu kusoma mchezo wa mpinzani wake

KMC wamejaribu kupenya ngome ya simba bila mafanikio, huku Simba SC wakipata kona mbili ambazo hazikuzaa matunda.
 
15' Deo kanda anaonyeshwa kadi ya njano baada kujaribu kuufinya mpira ndani ya eneo la hatari hatimaye kuangushwa, ambapo mwamuzi alitafsiri kuwa amejiangusha

KMC FC 0-0 Simba SC
 
18' KMC walipiga krosi iliyopanguliwa na Manula huku Simba wakijibu dk 20' kwa shambulizi kali kwa mpira kumbabadiza Wawa eneo la hatari na kutoka nje kuwa goal kick

KMC FC 0-0 Simba SC
 
Mlivyokuwa si wavumilivu ikitokea mmefungwa au Kutoa droo Leo Leo mtasema kakake Manara aondoke hajui kupanga timu
 
Back
Top Bottom