Vodacom Tanzania kama mpo humu naomba hizi habari ziwafikie. Mimi ni mteja wenu mkubwa sana. Tena mteja kindaki ndaki. Sina line ya mtandao mwingine wa simu zaidi ya line hii moja iliyonayo. Ndugu zangu wengi wapo mitandao mingine, najitahidi kumudu gharama kuwasiliana nao ili tu nisiachana na nyie.
Sasa nasema basi. Huduma yenu ya #songesha imenifanya niwachukie sana. Haiwezekani niwalipe deni lenu lote alafu mshindwe kunipa mkopo mwingine. Hilo nimelikubali na nikaamua kuachana na huo mkopo. Leo nimetumiwa hela kwaajili ya mahitaji muhimu, mmekata tena hela yote wakati sina deni na nyie.
Hakika hapa nilipo nimekasirika hakuna mfano. Maana nimewasiliana na watoa huduma wenu, wananiambia changamoto itatatuliwa ndani ya masaa 96. Hii sio haki. Hata kama ni utaratibu mliojiwekea, lakini hii haikubaliki. Hela tunazotumiana kwenye mitandao hii ya simu ni hela za mahitaji ya haraka. Leo mnaweza sababisha mtu akafatiki kwa kuikosa hiyo hela yangu ambayo ilitakiwa ikafanye mahitaji ya muhimu.
Japa nilipo mpaka naogopa kuomba hela sehemu nyingine maana inaweza ikatumwa halafu ikakatwa nikaendelea kusubilishwa masaa 96.
Hili nalo neno aisee. Maana hii ni kero sana. Wanafanya kazi kwa mazoea na kuchukulia kama kawaida tu linapotokea tatizo bila kujali athari upande wa mtejaTumia formula ya KILL ME BEFORE I KILL YOU wacha kulalamika wewe kila siku unawalipa kabla hujatumia Ila wewe ukitaka kutumia kabla hujalipa wanakutoza zaidi.
Fanya changamoto kuwa fursa Kama maandishi ulioandika n fursa huwezi kosa hata ka 20m kutoka kwao Kama ukiamua Sheria ifate mkondo wake Mana wewe mtumiaji ukimkosea ndo imekula kwako Ila wao wakikosea unataka kuwaomba samahani.
#NoRoomForExcuse
halotel mwendo wa konokono hamna kitu muleWanasema ni mtandao wa matajiri.....voda nawatumia zaidi kwenye M-PESA, kwenye internet halotel ni baba la mji, TTCL kwenye kupiga...
Duh! sijui itakuwa tatizo la location ulipo au device unayotumia......mimi nikinunua kile cha 5000 GB 7 kwa wiki, yaani natiririka wiki nzima kwa kasi ya 4G na hadi wiki inaisha najikuta nimemaliza kama GB 4 tu....halotel ni baba la mji kwenye internet aisee..halotel mwendo wa konokono hamna kitu mule
Mi nlishaachana na vodacom nna miaka sita sasaVodacom Tanzania kama mpo humu naomba hizi habari ziwafikie. Mimi ni mteja wenu mkubwa sana. Tena mteja kindaki ndaki. Sina line ya mtandao mwingine wa simu zaidi ya line hii moja iliyonayo. Ndugu zangu wengi wapo mitandao mingine, najitahidi kumudu gharama kuwasiliana nao ili tu nisiachana na nyie.