Vodacom ni majambazi sugu yasiyotumia silaha,yakamatwe haraka.

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
1,583
2,697
Ndugu zangu nimevumilia sasa nimechoka huu si wizi tena bali ni ujambazi' live '.
Hii kampuni nikipiga hesabu za haraka haraka tangu nijiunge nayo zaidi ya miaka 10 iliyopita wameshaniibia zaidi ya sh 600,000 tena wizi wa wazi kabisa bila hata ya aibu kila ukiweka vocha ukasema kuwa utajiunga siku nyingine hutakuta salio lolote, ukiwapigia simu na kuwauliza imekuwaje wamekula salio wanaanza kurushiana mpira, majuzi wakanitumia sms kuwa nimepata ofa ya kununua muda wa maongezi kwa sh 2,000 nipate dk 90 kwa wiki nzima, wakati huo nilikuwa tayari na muda mwingine wa maongezi wa wiki nzima na haukuwa umeisha, nikaona hili ni zali nikinunua tena dk 90 na hizi nilizonazo dk 35 nitakuwa na dk 125 tena, mwanaume nikajipinda buku mbili nzima na kujiunga dk 90,duuh kumbe nilikuwa naibiwa.
Mara baada ya kujiunga tu na kuanza kupiga zile dk 35 wakazipora na kuniunganisha na zile dk 90,hawa jamaa ni majambazi sugu wakamatwe haraka, kwani mamlaka ya wasiliano Tanzania wana kazi gani? wasipowachukulia hatua hawa jamaa kwa ujambazi huu sisi tuta assume wanakula nao maana si bure.
 
Mimi kinachonisikitisha niliingiza pesa kwenye akaunti ya benki ya UBA tangu December 16 na mpaka sasa hivi hiyo pesa haijaingia kwenye akaunti ya benki. Kila wakati wananiambia wanashughulikia.
 
Back
Top Bottom