Vodacom na wizi wa mchana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vodacom na wizi wa mchana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ngonani, Aug 29, 2012.

 1. n

  ngonani JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 27, 2012
  Messages: 1,371
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Nilivutiwa na tangazo la Vodacom kuwa ongeza salio la 7500 kabla ya 31st August nao watakuongezea mara mbili,nikapiga hesabu yangu nikaona nikiweka hiyo na kupata ofa angalau itanisukuma kwa siku kadhaa nikiwa na salio la elfu 22,500.Sasa cha ajabu nimeweka hela najibiwa nitaongezewa elfu 15 na nizitumie kwa siku mbili kupiga voda kwenda voda,huu si ndio wizi wa mchana,ilitakiwa kwenye ilo tangazo lao la ofa waseme kuwa hiyo nyongeza itatumika kwa siku mbil i tu na baada ya hapo haina kazi,pia wajulishe watu kuwa nyongeza hiyo ni voda kwenda voda tu,ningejua hivyo nisingepoteza hela yangu,ningeendelea na utaratibu wangu wa kununua dakika 100 kwa shilingi elfu mbili tu ambazo nazo ningetumia siku mbili hizo hizo. Acheni wizi kwenye matangazo yenu.
   
 2. bampami

  bampami JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 4,862
  Likes Received: 1,303
  Trophy Points: 280
  Minya *602#
  utachat bure siku nzima kwani lazima upige?
  V. Kazi ni kwako.
  Tigo ndiyo wezi.
   
 3. M

  Mpigaji JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watanzania mnapenda vya bure!Mpaka leo mnaibiwa kwa karata 3,weka elfu upate elfu 2!
   
 4. mjunguonline

  mjunguonline Member

  #4
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Njaa!Njaaa!Njaaa....Vya bure Ghali....
   
 5. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,695
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Masikini siku zote ndo huwa anakamuliwa zaidi
   
 6. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hakuna Bure dunia hii Arifu.. wenyewe wameshapiga mahesabu na wanajua fika hutoweza maliza hizo pesa.....
   
 7. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,115
  Likes Received: 24,203
  Trophy Points: 280
  Mkuu bampami ukiminya hiyo makitu wanakuchaji shingapi ili userebuke siku nzima?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...