tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,854
- 1,145
Form 4 masalia...wakikufungulia kesi uthibitishe wizi huo utapona wewe,kati ya mia 9 na elf tatu 500 ipi ya kumtoa mwenzake.
Mimi ni wakala wa Mpesa.
Leo kuna mteja kaja kutoa pesa, kabla ya kutoa pesa salio lilikuwa ni 1,183,900.
Baada ya mteja kutoa 3500 salio likawa ni 1,183,000.
Hapo kuna pungufu ya 900+3500=4400.
Nimejarbu kuwapigia simu. Wamenijibu kuwa hawaoni tatizo lolote.
Acheni wizi. Nirudishieni pesa zangu.
Hata mimi sijamuelewa huyu bwana. Alichoibiwa ni nini?
Kidato cha nne? Au kuna tatizo mahali?:help:
mbona mnakuwa na dharau kwa vitu msivyovijua?
Kwa kweli nadhani mwizi ni wewe myoa mada
Haya mahesabu yako kiboko. Hiyo mpesa unauza mwenyewe ama wewe ndo tajiri? Manake kama wewe uko hivi sijui huyo anaesimamia biashara ana akili gani! Go home, you are drunk!
Mteja akitoa pesa salio la wakala linatakiwa kuongezeka sio kupungua kama anayetoaHata mimi sijamuelewa huyu bwana. Alichoibiwa ni nini?
Mkuu,
Watu wasichojua ni kua Mteja akitoa hela kwenye M-Pesa, basi kwa wakala salio linaongezeka. Maana ni sawa na Mteja anamuuzia wakala salio lake.
Sasa kwa kutokuelewa huko wanafikia kumshambulia mleta mada bure. Pole Mkuu Mzee.
Meanwhile umeadimika sana kule siasani kaka (Out of Topic & Joke)
Mbona anaeleweka tu vizuri, ni kwamba kabla mteja hajaja, alikuwa na float ya TZS 1,183,900 ambayo yeye anaita salio, kwa kawaida mteja anapotoa float inatakiwa iongezeka kwa kiasi mteja alichotoa, mteja wake alitoa TZS 3,500, hivyo float ilitakiwa kuwa TZS 1,183,900+TZS 3,500=TZS 1,187,400, sasa badala ya float kuongezeka kwake ilipungua as if mteja wake alikuja kuweka hela. Inavyotakiwa ni hivi: akiweka float inapungua na cash inaongezeka na akitoa float inaongezeka na cash inapungua.Kidato cha nne? Au kuna tatizo mahali?:help:
Biashara hizi za uwakala ni Chuma Ulete Advanced ya Mzungu,,,haya makampuni ya Simu huwaga wanaiba kwenye ile miamala pindi pale mteja anapokuja kutoa hela na wewe wakala unaweza ukaiona hela ndogo tu lakini ukiangalia ni hasira yako we chukulia kwenye biashara yako kwa siku unafanya Transaction za wateja 60 kila mteja wanakuibia tsh150( Anaetoa 40000 kushuka chini,,ikipanda wanazidi kukuibia) zidisha hiyo kwa mwezi halafu angalia kuna Mawakala wangapi nchini.
I hope everything is okay as of now.Mimi ni wakala wa Mpesa.
Leo kuna mteja kaja kutoa pesa, kabla ya kutoa pesa salio lilikuwa ni 1,183,900.
Baada ya mteja kutoa 3500 salio likawa ni 1,183,000.
Hapo kuna pungufu ya 900+3500=4400.
Nimejarbu kuwapigia simu. Wamenijibu kuwa hawaoni tatizo lolote.
Acheni wizi. Nirudishieni pesa zangu.
====_==================
Mteja wake ndiye aliyetoa hicho kiasi; ili muamala ukamilike unahusisha watu wawili, mwenye kibanda cha mpesa ambaye ndo huyu anayelalamika na mteja wake ambaye alitoa hicho kiasi, kama mtoa mada anasema ukweli kuna tatizo ambalo halijulikani; lakini kwa ufahamu wangu inawezekana kabisa mtoa mada kuna kiasi alichokuwa anadaiwa. hii hutokea mara nyingi sana unakuta mteja anatoa hela halafu anakosea namba ya wakala badala ya kuingiza namba ya wakala alipo anajikuta anaingiza namba ya wakala mwingine, sasa aliyekosea akilalamika lazima hicho kiasi kivutwe kutoka kwa wakala ambako kimeingia kwa makosa kurudishwa kwa mteja aliyekosea. nadhani inawezekana kimetokea kitu kama hicho kwa mdau lakini si kweli kwamba Vodacom wamwibie kwa jinsi hiyo, kama ni kweli afuatilie maana system zinaonyesha kila kitu ikiwezekana wamprintie aangalie tatizo liko wapi asione kwamba ni hela ndogo sio ujinga kuuza mbuzi kwa kesi ya kuku kama unachotafuta ni haki.Masuke, kwa nini atoe Tsh.3,500 kwa mteja wakati float inaonyesha vituko?