Vodacom mobile partner---ni mimi tu au?

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
24,891
11,288
Wadau, nashukuru mungu nimerudi mjini baada ya katripu kafupi... nimeimiss sana JF hasa kwa kukosa habari nzito na nyepesi na pia hoja nzito na nyepesi na vimbwanga vyote kwenye majukwaa mbalimbali

Nina tatizo moja, yaani haka ka-mobile partner tangu nikaingize kwenye ile MYMEG kamekuwa slow na ni siku tatu sasa sijapata access kabisa; sasa maswali yangu. Je, hiki kimobile partner ina maana coverage yake ni tofauti na simu za kawaida?

Je nikiweka MYMEG ndio inakuwa slow au kuna tatizo jingine?

Ninajua kuna wataalam humu na walinisaidia kuondoa virusi, naombeni msaada maana namiss JF tena sasa niko likizo itakuwa mateso makubwa

Wakatabahu...
 
Wakatabahu??????

Huu ni msemo wa kidini au kikabila au kiswahili fasaha?
 
Labda upige vidacom huduma kwa mteja utasaidiwa....kumbuka kuna gprs na 3G...speed huwa tofauti kidogo...uko eneo gani na lina nini kati ya hizo??piga huduma kwa mteja...no 100 nafikiri utasaidiwa.
 
Labda upige vidacom huduma kwa mteja utasaidiwa....kumbuka kuna gprs na 3G...speed huwa tofauti kidogo...uko eneo gani na lina nini kati ya hizo??piga huduma kwa mteja...no 100 nafikiri utasaidiwa.

Mkuu nashukuru sana kwa idea, niko mbali kidogo ya Dar [Pwani] na nikipiga kule majibu yao ni kama ya wabunge wetu... na kwasababu kuna wakti nilipata msaada humu ndio maana ninakimbilia huku... mimi natumia 3G na kinachonisumbua ni ile kubadili tu mfumo mambo yakawa slow
 
Wazushi sana wale, niliface the same problem nikawakal wakaniambia watanitumia log number alafu watu wa data watanicall, lakini hawakufanya hivyo. Mi nakaa karibu kabisa na mnara wao cha ajabu huo mnara una 3g lakini cha ajabu zaidi it was too slow, bytes zinaenda tu....
 
Mimi mara nyingine Mobile Partner 3G huwa naiona kuwa ni fast na mara nyingine slow! Nadhani suala ni wakati gani uko kwenye mtandao au idadi ya watumiaji kuwa ndogo au kubwa!

Nyakati za usiku (kuanzia saa 4:30) huwa naona iko fast sometimes na mara nyingine slow! Mara nyingine mchana na fast, mara nyingine slow! Kwa ujumla nimeshindwa kupata formula nzuri ya hii kitu! Hawa customer care huwa nawaonea uvivu sana maana mara nyingine huwa ni weupe!
 
tumia zantel-mobile partner,halafu kuna kitu huwa kina counterfeit window,kinaitwa window-genuine microsoft.unahitaji crack-file ya kuzuia hiyo genuine huwa ina slow down computer internet
 
ila jamaani hizi customer care za mitandao zote ni booom sana hawajui kitu uzushi mtupu wanachojua wao ni washa simu yako na uzime basi kazi kubana pua zao tu ukiongea nao wamekaliaa kutongozwa kwa mademu na mamen kuuza sura tu hawana lolote.
 
uwezo mdogo sana...wanachojua ni kuzima na kuwasaha simu. tigo waliliona hilo ikabidi wa outsource call center yao....angalau kuna heshima siku hizi...wabongo wavivu sana, nenda kwa wakenya uone....
 
Back
Top Bottom