Vodacom mnaniboa sana....!!!!

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Tangu juzi watu wanaonipigia simu yangu ya kiganjani wanakumbana na ring tone ya Mizengo Pinda akijitambulisha na kisha kunadai kuwa watu wapigie kura Mlima kilimanjaro eti uwe ni moja ya maajabu ya dunia sijui ulimwengu??!! Hivi hawajaona njia nyingine ya kutaka watu wapige hizo kura mpaka kuja kutupachikia hilo sauti la huyo bwana bila ridhaa za wateja? Habari ya mlima k'njaro tunaifahamu na kuna taarifa kibao zinazotuhamasisha watanzania kupiga kura sio hii mliyoiweka tena bila hata ku-consult clients wenu...kwa kweli imenikera sana nafikiria njia mbadala kuondokana na hii kitu!!....
 
Back
Top Bottom