Vodacom kukubali kutoa ushahidi dhidi ya Lema ni dharau kubwa kwa watanzania

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,419
Tumepata taarifa vodacom watatoa siri za mteja wake mbunge wa Arusha Mjini.
Wakithubutu kufanya hivyo watakuwa wameshidwa kumlinda mteja wao na itakuwa wanafanya kwa shinikizo,

Watanzania wenzangu iwapo wataendelea na nia yao ya kutoa siri za mteja wao yapasa sisis watanzania tulio wateja wao tuwawajibishe kwa kujitoa kutumia mtandao wao

Kumbukeni hii ni kampuni ya kigeni na iwapo watafanya hivyo ina maana wameshatudharau sana sisi wazawa kiasi cha kuingilia mambo yetu ya ndani
 
Hili la staff kwenda makamani kwa kesi ya mtu binafsi kutoa ushahidi ni kama kuna tatizo..........

Vodacom wanachotakiwa kufanya ni kuwapa mahakama taarifa walizoomba kama zina maslahi kwa taifa........

Kama mambo ya kuingilia mawasiliano ya serikali, uharifu na ujambazi mwisho uhaini..........

Lakini kampuni kubwa ya waingereza kama vodacom kwenda kusimama mahakamani kwa ajiri ya kumtetea mtu binafsi baada ya kuwapa polisi hizo taarifa wao ndio wafanyie Kazi.....

Kama vodacom wamefanya hivyo au watafanya basi kuna haja ya Takukuru kuingia vodacom Arusha kuchunguza Rushwa kwa maafisa Wa vodacom........
Tumepata taarifa vodacom watatoa siri za mteja wake mbunge wa Arusha Mjini.
Wakithubutu kufanya hivyo watakuwa wameshidwa kumlinda mteja wao na itakuwa wanafanya kwa shinikizo,
Watanzania wenzangu iwapo wataendelea na nia yao ya kutoa siri za mteja wao yapasa sisis watanzania tulio wateja wao tuwawajibishe kwa kujitoa kutumia mtandao wao
Kumbukeni hii ni kampuni ya kigeni na iwapo watafanya hivyo ina maana wameshatudharau sana sisi wazawa kiasi cha kuingilia mambo yetu ya ndani
 
hv ingekua kinyume kwamba ushahidi unaotolewa na vodacom ndio utaomtoa hatiani ingekua pia ni makosa??? ukiambiwa line yako ya simu imetumika kwenye uhalifu na ushahidi ndio utakutoa hatiani utakataa usitumike?? ukiwa na kesi ya kutukwanwa kwa njia ya mtandao na ushahidi wa msg alizokutumia na zimefutika kwenye simu yako ndio utakaomtia hatiani aliyekutukana utaukataa ushahidi??... elewa kuna sheria zinawabana wao kutoa taarifa hizo pale ushahidi unapohitajika na mahakama kinyume na hapo ni kuzuia sheria isifate mkondo wake... kwa uwelewa wangu!!!

sio bongo tu... na wala sio dharau kama ni muelewa.. hata ungekua marekani ushahidi ungefuatwa tu...swala hizo evidence zote zipatikane kihalali na kisheria ikiwemo kibali cha kutoa info hizo
 
kwani tatizo ni nini?

Hata kama wakitoa ushahidi kama Lema hajafanya kosa haitasaidia labda uniambie kama kweli Lema amefanya kosa na kwa maana hiyo hutaki kosa liwekwe wazi.

Huoni kuwa Vodacom ndio watamsafisha Lema kwa sababu ushahidi wao utakuwa ni kweli.

Kumbuka pia wanachofanya Vodacom ni takwa la kisheria ambalo linapatikana katika sheria inayoitwa The Electronic and Postal Communications Act, 2010.
 
Tumepata taarifa vodacom watatoa siri za mteja wake mbunge wa Arusha Mjini.
Wakithubutu kufanya hivyo watakuwa wameshidwa kumlinda mteja wao na itakuwa wanafanya kwa shinikizo,
Watanzania wenzangu iwapo wataendelea na nia yao ya kutoa siri za mteja wao yapasa sisis watanzania tulio wateja wao tuwawajibishe kwa kujitoa kutumia mtandao wao
Kumbukeni hii ni kampuni ya kigeni na iwapo watafanya hivyo ina maana wameshatudharau sana sisi wazawa kiasi cha kuingilia mambo yetu ya ndani

Sheria za kumlinda mteja huwa zina mipaka! Linapotokea jambo la Uharifu au Kesi za mahakamani or otherwise, mtandao ya simu huwa inatumika kutoa ushahidi, na hilo sio jambo geni.

Suala la kuhamasisha watu kutotumia mtandao kisa ulitumika kutoa ushahidi wa mtuhumiwa, ni jambo la kufikirika.

Kuwa kampuni ya kigeni, sio sababu ya msingi ya kwamba isitumike katika ushahidi mahakamani.
 
Tuwaonesheni dawa kwa kupunguza biashara nao, cut down vouchers and money transfers... Watajishtukia tu....
 
Hapo ndipo inabidi umkubali Maxence kwa ujasiri wake wa kukataa kutoa taarifa za wachangiaji wake na kuingia gharama ya kufungua kesi ya kikatiba kuhusu faragha za wachangiaji. Kimsingi mtoa huduma yoyote analazimika kutoa taarifa za wateja wake kama kuna sheria imevunjwa-analazimika kisheria.

Unaweza usiwalaumu Vodacom kwa kutoa taarifa maana huwa wanatoa kwa polisi karibu kila siku mawasiliano ya watu wanaoshikiwa kwa uhalifu. Labda hili la kwenda kusimama mahakamani kama shahidi ndiyo lenye walakini.
 
Tumepata taarifa vodacom watatoa siri za mteja wake mbunge wa Arusha Mjini.
Wakithubutu kufanya hivyo watakuwa wameshidwa kumlinda mteja wao na itakuwa wanafanya kwa shinikizo,
Watanzania wenzangu iwapo wataendelea na nia yao ya kutoa siri za mteja wao yapasa sisis watanzania tulio wateja wao tuwawajibishe kwa kujitoa kutumia mtandao wao
Kumbukeni hii ni kampuni ya kigeni na iwapo watafanya hivyo ina maana wameshatudharau sana sisi wazawa kiasi cha kuingilia mambo yetu ya ndani
Kwenye tuhuma za uhalifu hiyo kinga ya siri ya mteja inawezaondolewa kwa mujibu WA Sheria.Alafu ni Siri gani IPO hapo na kwanini una hofu isifahamike?
 
Habari wakuu.

Mwenzako akinyolewa wewe kazi tia maji kwani zamu yako yaja, vodacom wamekubali kutoa siri za mteja wao, leo limemkuta Lema, kesho hatufahamu itakuwa zamu ya nani.

Kwa maana hiyo ni dhahiri Vodacom wameshapoteza uaminifu kwa wateja wao, kilichobakia ni sisi kuanza kuwakataa wao mapema kabisa kabla hatujaadhirika, mitandao ya simu ipo mingi mizuri na huduma nzuri tu zinatoa, kuanzia leo tuanze kuikataa vodacom na tutafanya hivyo kwa kuacha kutumia line zao, wajulishe ndugu na jamaa na wazalendo wote tuihame vodacom tuende kwenye mitandao inayowajali wateja wao na kuwasitiri. Ipo mingi sana.

Kuna Halotel, Tigo, Zantel, Ttcl n.k

Sema hapana vodacom.........

Say NO to vodacom Tanzania.........

Renew line yako ile ile kwa mtandao mwingine...

[HASHTAG]#KampeniKataaVodacomTanzania[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom