Babu wa Loliondo
JF-Expert Member
- Jan 31, 2012
- 323
- 105
- Thread starter
- #61
Tena ukisoma vizuri hio tofaut ya faida ilisababishwa na hasara kwenye kampuni yake ya minara Helios Towers ambayo wameamua kuuza hisa zao na kuachana nayo,vinginevyo ni uwekezaji mzuri sana,tukizubaa tutakuja sikia baadae akina Manji ndio wana hisa za kutosha huko na kama kawaida yetu tutalalamika kana kwamba tulikatazwa kuwekeza wakati fursa tulipewa tukaipuuzia.Mkuu mimi binafsi naona ni opportunity nzuri sana kuwekeza kwenye Telecoms. nilitumiwa prospectus yao nikaisoma ipo vizuri wanatengeneza profit baada ya kodi ni bil. 29. ingawa imeshuka kutoka bil 32 mwaka 2015 na bil 128 mwaka 2014. hii inatokana na competition kuwa kubwa lkn wanaongoza kwenye market share. na pia ukiongelea Vodacom unaongelea global kila mtu anaitolea macho. Dividend ni 50% profit itakayopatikana kwa mwaka. Najua wengi wetu ni speculators na tunategemea price appreciation ili kufaidika. Vodacom haitofilisika leo wala kesho na kama opportunity kama hii ikipatikana ya ku participate katika IPO sio ya kuacha wakuu.