Babu wa Loliondo
JF-Expert Member
- Jan 31, 2012
- 323
- 105
Kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) itaanza kuuza hisa zake milioni 560 kwa thamani ya Shilingi 850 kila hisa. Mauzo yataanza tarehe 09.03.2017 na kufungwa tarehe 19.04.2017.
======
YAWAPIGA MSASA MAWAKALA WATAKAOKUSANYA FEDHA ZA HISA
Mawakala wa kuuza hisa za Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom TanzaniaPLC, wamepatiwa mafunzo elekezi ya siku moja yaliyokuwa na lengo lakuwaelimisha jinsi ya kukusanya fedha wakati wa zoezi la kuuza hisa zakampuni hiyo litakapoanza hivi karibuni tukio ambalo limekuwa likisubiriwakwa hamu kubwa na watanzania walio wengi.
View attachment 477950
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao akifafanua jambo kwa mawakala (hawapo pichani )wakati alipokuwa akitoa mafunzo elekezi ya siku moja jijini Dar es Salaam leo juu ya ukusanyaji wa fedha wakati wa zoezi la kuuza hisa za kampuni hiyo litakaloanza hivi karibuni.
Semina hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mlimani City ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ian Ferrao alisema “Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu tangia tulipoanza mchakato wa maombi ya kuuza hisa kwa umma hadi kufkia sasa ambapo tayari tumepata kibali cha kutekeleza zoezi hili kutoka serikali kupitia Mamlaka ya Dhamana Masoko na Mitaji (CMSA) na mkiwa wabia wetu katika mchakato huu tumewaita kwa ajili ya kubadilishana mawazo jinsi tutakavyofanikisha matarajio yetu tuliyokusudia na kuwa tayari kwa kazi iliyosubiliwa kwa muda mrefu”.
Ferrao alieleza kuwa Vodacom inatarajia kuuza asilimia 25% ya hisa zake kwa umma zenye thamani ya shilingi Bilioni 476/-na kila hisa itauzwa kwa shilingi 850/-
Vodacom Tanzania PLC,imekuwa ya kwanza kutekeleza sheria ya Electroniki na Mawasiliano ya Posta (EPOCA) na sheria ya fedha ya mwaka 2016 inayoyataka makampuni kumilikisha asilimia 25% ya hisa zake kwa umma kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Ferrao, wananchi wataweza kununua hisa za zao katika matawi ya Benki ya NBC na mawakala wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) waliopo nchini kote.
Wakati zoezi la uuzaji hisa za Vodacom linatarajiwa kuanza rasmi hivi karibuni,wawekezaji na wananchi wamekuwa wakisubiri kwa shauku kubwa ambapo wamekuwa wakifuatilia kwa karibu jinsi zoezi hili linavyoendelea ili waweze kujipatia fursa ya kumiliki hisa katika kampuni kinara ya mawasiliano nchini.
View attachment 477951
View attachment 477952