salimkabora
JF-Expert Member
- Nov 10, 2012
- 2,441
- 652
Jana nimenunua kifurushi cha vodacom internet kinachosomeka 9,000/= kwa mwezi; kabla sijaanza kusoma emails zangu umeme ukakatika na haukurudi hadi saa 12 jioni. Nilipowasha computer nilipokea ujumbe wa kifurushi kimeisha ili hali ni muda mfupi tu tangu nifungue internet hata nusu saa bado; sasa swali, hivi huu wizi wa aina hii ni nani anaudhibiti katika taifa hili? je hii fedha ya wizi wa jinsi hii toka kwa mteja maskini haiwezi kuibiwa fedha kubwa faidi kwenye kodi ya nchi? kwanini hivi vifurushi makampuni wanayojitangazia kitapeli havisajiliwi ili viweze kufatiliwa na mamlaka husika? elfu tisa kuunguzwa kwa nusu saa ni karibia laki tano kwa masaa 24; hivi kweli upo uhalali gani hapo? unaibiwa huku huwezi kujilinda?