Leo
nimejiunga na huduma ya vodacom ya cheka time ya Tsh 400 ambayo unapewa
dk 10 za vodacom kwenda vodacom na MB 25 na sms100 baada ya kujiunga
nilipiga sim nikaongea kwa dk 5.53 cha kushangaza muda huo huo nikatumiwa msg toka
voda kuwa kifurushi changu kimekwisha. Jamani voda huu sio wizi?
ni wezi sana.mie juzi niliweka cheka miatano nikapata dakika 20 na bado kwenye cm zikabaki fedha, nilipiga simu nikaongea dk 3 kidogo fedha ikaisha kwenye akaunti yote na hizo dk 20 niliongea dk 3 tu.najutia sana na wasiwaamini hawa wezi wengine wanaosimamiwa na kumilikiwa na mafisadi akina Rostam.
tangia juzi voda inasumbua maana mimi nilinunua cheka 500 juzi ilipofika jana nikanunua cheka 500 na leo nimenunua cheka 500, lakini nilipoangalia salio nimezikuta dakika zote za tangia juzi na sms lakini mb kwakuwa nazitumia nimebakiza mb 74
hamia huku kwetu, tangu 2004 hawa jamaa nawakubali sana, vijana walikuwa hawalali, paper ikivuja manasolve maswali kwa njia ya maongezi ya simu, ndiko wengi walikojifunzia kutongoza kwenye simu na kujenga makomfo
Hawa jamaa ni noma kwa kuibia wateja though kuna wakati 50MB zinakatika ndani ya dakika 20 wakati page unazopita ni hizi hizi za JF, ila kuna wakati 50mb unatumia mpaka basi na ukiangalia salio unakuta bado zipo 50mb, sijui hapa wataalamu watasemaje maana naweza ingia JF tu dakika 20 inakata lakini kuna kipindi kingine unaingia JF na mitandao mingine mara kibao lakini bundle yako bado inakuwa imeshiba
Hata mimi nilicheka nao voda kwenda mitandao yote shs 350 nilipopiga simu ya airtel nikagundua kuwa hela imeisha. Nikafifkiri kuwa mimeongea sana hivyo nikajirusha tena ya shs 500 dk 20 mitandao yote. Niliongea dak 8.21 kuulizia salio la cheka nao nikaambiwa zero na salio langu la kawaida limeliwa pia.Kwa kweli nawakubali airtel yatosha maana kila unapoongea ukimaliza wanakupa baki. Sasa sicheki tena kwenye voda hadi warudishe pesa zangu.
nilikuwa na salio la sek 3840, nikapiga simu baada ya dk 7 kupita nasiki beep kwenye simu kuashiria kwamba salio linakaribia kuisha. sijakaa vizuri simu ikakata. kucheck balance ni naona kuna sek 0 na mb20 zimeisha kwa dk 7 na bado wakakata kwenye balance yangu. huu ni wizi mkubwa
nini kimetokea voda? wiki mbili hawako vizuri ukijiunga hupewi dk,mb, wala sms na pesa inachukuliwa bt baada ya mda hiyo pesa huwa wanakurudishia kwene ac. hebu wachekin customer service wako vizuri tu.
Je mmepeleka malalamiko ofisini kwao? Ukilalamika hapa hutaweza kusaidika, una haki ya kupata huduma kwa kile ulicholipia. Nakushauri upige simu customer care ya voda au uwaandikie kwenye facebook page yao kwa msaada zaidi.
Frankly writting mimi tangu Airtel waje na huduma yao ya TOSHA, VodaCom nimebaki nayo ya kupokea tu, means siiweki tena airtime. Hata hawa Airtel nao tangu juzi nina mashaka nao kwani wanazidisha actual time uliyotumia.