Vodacom acheni Upumbavu!

M-pesa leo mmeniumbua mbele ya baba mkwe na mama mkwe.Pesa unahamisha ila msg ya kuthibitisha kuwa umehamisha pesa hazirudi na account inaonyesha pesa imetoka.Tatizo hili limekuwa likilalamikiwa kwa wiki tatu sasa. Custumer care(tena wa kike) ananigombeza kama mtoto,ananikatia simu niliyopiga kama customer wa VODACOM kuomba msaada('15366' kupitia namba hii ambayo nachajiwa navyoipiga) ananipelekesha na kujifanya yeye ndo fundi mitambo eti pesa imeshatoka iko hewani ila napaswa nitume tena(jibu hili nimeshapewa zaidi ya mara tano kwa siku tofauti ninazo muamishia mtu pesa kwa M-PESA). Lile tangazo lenu la M-pesa la yule mjomba anayepaa ni zuri sana na linaonekana mmelitengeneza kwa pesa nyingi ila huduma mnayoitoa kwa wateja wenu haifanani na maudhui ya tangazo hilo.
Matatizo ni kitu cha kawaida, ila tatizo hili limekaa zaidi kwa takribani siku ishirini naa.. Nadhani mmeingiza siasa kwenye HUDUMA YA VODACOM.
Kuna kitu tutafanya kama wateja then mtafrahiii!!!
 
Fungua kesi ya madai juu ya kampuni hii, kwani ukiwashinda utapata pesa nyingi sana na pia watanzania tuanze kususia Vodacom na tigo na wote tujiunge Zantel kwani ndio mtandao wenye kujali wateja
 
Hivi hakuna mwakilishi wa Vodacom au TCRA humu barazani?
Au japo mfanyakazi tu wao afikishe malalamiko yanayotolewaga hapa?
Mbona tunaibiana mchana kweupe?
TCRA mko wapi lakini?
Mmehongwa Tshs ngapi kiasi cha kutoelewa?
Tusemeje Voda muelewe?
Au ndio mnarudisha hela mliokodia Chopa ya Igunga?
Nimwekeka alfu ili niongee na mtu juu ya kumtumia M-Pesa, kushtuka 550/ ishakatwa eti kwa ajili ya kuambiwa "sishikiki", ni nini hiki?
Karibia kila siku naandika msg ya kuitoa kwenye hii promo feki, mbona hamnielewi?
Nishapiga mara kibao customer care kuwafamisha kua sitaki hii huduma, mbona hawanitoi?
Potelea mbali, huu sasa ni Usenge uliopitiliza huu!!!

Yaehhh, Umejiingiza au Umeingizwa?
Bora ungekuwa umebandikwa/kubandikwa ningekusaidia KUKUBANDUA!
Pole sana!!!!!!
 
M-pesa leo mmeniumbua mbele ya baba mkwe na mama mkwe.Pesa unahamisha ila msg ya kuthibitisha kuwa umehamisha pesa hazirudi na account inaonyesha pesa imetoka.Tatizo hili limekuwa likilalamikiwa kwa wiki tatu sasa. Custumer care(tena wa kike) ananigombeza kama mtoto,ananikatia simu niliyopiga kama customer wa VODACOM kuomba msaada('15366' kupitia namba hii ambayo nachajiwa navyoipiga) ananipelekesha na kujifanya yeye ndo fundi mitambo eti pesa imeshatoka iko hewani ila napaswa nitume tena(jibu hili nimeshapewa zaidi ya mara tano kwa siku tofauti ninazo muamishia mtu pesa kwa M-PESA). Lile tangazo lenu la M-pesa la yule mjomba anayepaa ni zuri sana na linaonekana mmelitengeneza kwa pesa nyingi ila huduma mnayoitoa kwa wateja wenu haifanani na maudhui ya tangazo hilo.
Matatizo ni kitu cha kawaida, ila tatizo hili limekaa zaidi kwa takribani siku ishirini naa.. Nadhani mmeingiza siasa kwenye HUDUMA YA VODACOM.
Kuna kitu tutafanya kama wateja then mtafrahiii!!!

Dah! Ni wewe au?
 
Vodacom mapimbi sana hii bahati nasibu yao eti ukiingia mara1 huruhusiwi kujitoa!Majambazi wanakugeuza mradi,wezi wakubwa wangekuwa wanatoa tahadhari kuwa ukishajiunga ni forever basi mtu ungeamua mwenyewe lkn wapi!nimetuma msg kuomba nijitoe hakuna jibu!Nimeitupa line hii ni wk ya pili.Mijitu yenyewe hailipi kodi,afadhali airtel kidogo nawaheshimu mana wako kwenye topten.
 
Mim voda wananiboa pind unaponunua bundle kwajil ya internet services. Ukinunua leo saa 6 mchana watakuambia itaisha muda wake wa matumiz kesho yake mchana saa 6 mchana wakimaanisha after 24 hrs lakin ajab ikifika saa 6 usiku ukiulizia salio wanakuambia hauna data bundle. Mbona kampuni nyingine ni waaminifu ktk hili? Acheni wizi Voda mnatuboa sana sio siri.
 
Fungua kesi ya madai juu ya kampuni hii, kwani ukiwashinda utapata pesa nyingi sana na pia watanzania tuanze kususia Vodacom na tigo na wote tujiunge Zantel kwani ndio mtandao wenye kujali wateja

Yani Watanzania wangejiunga na Zantel yani wangekuwa tumenusuru pesa ze2. Voda Mi nitaihama penda wasipende. Wezi wakubwa hawa.
 
Naona Zantel wameamu kuwanunua watu JF ili wawatangaze!!
Good work bro..yaelekea unapata commission kubwa sana!
 
pole hii ndo mitandao yetu mkuu wanatafuta pesa kinguvu huu ni sawa na wizi tu
 
pole ;hii ndo mitandao yetu mkuu wanatafuta pesa kinguvu huu ni sawa na wizi tu
 
Pole sana Shark kwa kukatwa senti zako.Nakushauri uende duka lolote lililo jirani na ww wataitoa hiyo huduma usiyoitaka na maisha yatasonga kama kawa.
Nashauri pia uwe na ukomavu wa fikra kuliko kukurupuka na kutukana kampuni nzima.zile promo huwa zinarushwa redioni kwenye tv na mwishoni huwa wanasema masharti na vigezo kuzingatiwa.
Hausomi hayo masharti wala kujiuliza mara mbili kabla hujashiriki.Umaskini wako unakusukuma kushiriki promo ili upate hela za bure.
Mwisho;jaribu kuacha fikra za kimaskini za kuweka vocha za buku buku...umakaa dar tangu 1985 hadi leo,una internet kwenye cm lkn bado una fikra za kimaskini.
Ukue
 
Hamia Airtel,wewe ndugu jamaa na marafiki zako wote. Atlist serikali inamiliki asilimia 49 kwenye Airtel. Hiyo mitandao mingine ni full ukoloni
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hivi hakuna mwakilishi wa Vodacom au TCRA humu barazani?
Au japo mfanyakazi tu wao afikishe malalamiko yanayotolewaga hapa?
Mbona tunaibiana mchana kweupe?
TCRA mko wapi lakini?
Mmehongwa Tshs ngapi kiasi cha kutoelewa?
Tusemeje Voda muelewe?
Au ndio mnarudisha hela mliokodia Chopa ya Igunga?
Nimwekeka alfu ili niongee na mtu juu ya kumtumia M-Pesa, kushtuka 550/ ishakatwa eti kwa ajili ya kuambiwa "sishikiki", ni nini hiki?
Karibia kila siku naandika msg ya kuitoa kwenye hii promo feki, mbona hamnielewi?
Nishapiga mara kibao customer care kuwafamisha kua sitaki hii huduma, mbona hawanitoi?
Potelea mbali, huu sasa ni Usenge uliopitiliza huu!!!
Inawezekana ni kweli eee!
 
Pole sana Shark kwa kukatwa senti zako.Nakushauri uende duka lolote lililo jirani na ww wataitoa hiyo huduma usiyoitaka na maisha yatasonga kama kawa.
Nashauri pia uwe na ukomavu wa fikra kuliko kukurupuka na kutukana kampuni nzima.zile promo huwa zinarushwa redioni kwenye tv na mwishoni huwa wanasema masharti na vigezo kuzingatiwa.
Hausomi hayo masharti wala kujiuliza mara mbili kabla hujashiriki.Umaskini wako unakusukuma kushiriki promo ili upate hela za bure.
Mwisho;jaribu kuacha fikra za kimaskini za kuweka vocha za buku buku...umakaa dar tangu 1985 hadi leo,una internet kwenye cm lkn bado una fikra za kimaskini.
Ukue

Eh!!,
Yamekua hayo tena mkuu wangu?
Yaani pole na masimango juu yake.
Anyway, mi sipo sana voda,
Ni vile tu kuna kamradi nakaendeleza kijijini ambako hawana tigo-pesa.
So buku ni kwa ajili ya kipiga na kuwauliza kama wameshapata pesa kama nikituma!!!
But otherwise punguza masimango kaka, niko kwenye matatizo namna hiyo ni kikatishana tamaa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom