Lakini wanajitahidi kudhamini ligi yetu
Mkuu, jibu hilo lisms lao la "hushikiki" kwa ju-reply TOA uataondokana na hilo CHUMA ULETE.
Mimi walinitesaga sana, sina hamu kabisa!
Hivi hakuna mwakilishi wa Vodacom au TCRA humu barazani?
Au japo mfanyakazi tu wao afikishe malalamiko yanayotolewaga hapa?
Mbona tunaibiana mchana kweupe?
TCRA mko wapi lakini?
Mmehongwa Tshs ngapi kiasi cha kutoelewa?
Tusemeje Voda muelewe?
Au ndio mnarudisha hela mliokodia Chopa ya Igunga?
Nimwekeka alfu ili niongee na mtu juu ya kumtumia M-Pesa, kushtuka 550/ ishakatwa eti kwa ajili ya kuambiwa "sishikiki", ni nini hiki?
Karibia kila siku naandika msg ya kuitoa kwenye hii promo feki, mbona hamnielewi?
Nishapiga mara kibao customer care kuwafamisha kua sitaki hii huduma, mbona hawanitoi?
Potelea mbali, huu sasa ni Usenge uliopitiliza huu!!!
Kudhamini Ligi kwa kuwaibia wateja?
Hii ni mara ya pili nalalamika hapa, hivi hakuna mwakilishi wao?
Kila nikipiga customer care wananijibu watanitoa, mbona bado natumiwa?
Wadau nisaidieni nini natakiwa nifanye,
Maana naona hasira zinaanza ku-control ubongo ambapo si sahihi!!
Mkuu,
Nishatuma TOA,
ONDOA,
ONDOKA,
CANCEL,
TOKA,
STOP n.k.
Mpaka matusi nishatuma ili wanipigie wao niwape ukweli lakini wapi!!
Juzi kulikuwa na thread ya Tigo, leo Voda keshokutwa labda Airtel. Something must be wrong somewhere. Sijaelewa inakuwaje mtu anakuwa subscribed automatically kwneye kitu ambacho hakitaki. Or are we pressing the wrong bottons?