Vladimir Putin

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,778
Vladimir Vladimirovich Putin alizaliwa Saint Petersburg wakati huo ikijulikana kama Leningrad, October 7, 1952. Ni rais wa Urusi kwa sasa tangia May 7, 2012. Alikuwa waziri mkuu kuanzia 1999 mpaka 2000, raisi kuanzia 2000 mpaka 2008, na tena kushika nafasi ya uwaziri mkuu kutoka 2008 mpaka 2012. Katika kipindi chake cha pili cha uwaziri mkuu pia alikuwa mwenyekiti wa chama cha Umoja wa Urusi.



Vladimir ni mtoto wa tatu na wa mwisho kuzaliwa katika familia ya Vladimir Spiridonichich Putin na Maria Ivanova Putin. Vladimir alitanguliwa kuzaliwa na kaka zake wawili, Viktor na Albert. Bahati mbaya Albert alifariki akiwa mtoto mchanga kutokana na ugonjwa wa polio, katika kipindi cha mateko ya Lenigrad. Mama yake Vladimir alikuwa mfanya kazi wa kiwandani, baba alikuwa mwandishi katika kikosi cha majini kwenye jeshi la Soviet. Katika kipindi cha Vita Kuu ya II ya Dunia, baba yake Vladimir alitumikia akiwa kwenye submarine. Hii likuwa mwanzoni mwa 1930, baadae alihamishiwa katika jeshi la kawaida ambako alipata majeraha makubwa sana mwaka 1942.

September1, 1960, Vladimir alianza shule Baskove Lane, karibu na nyumbani kwao. Alikuwa ni mmoja katika vijana wachache ambao hawakuwa kwenye Young Pioneer Organisation (mfano wa vijana wa chipukizi). Alijiunga na umoja huo akiwa na miaka 12 na alianza kujifunza sambo na judo. Alitamani kujifunza mbinu alizokuwa anacheza officer wa usalama katika cinema za ki-Soviet. Vladimir alisoma ki-Jerumani Saint Petersburg High School na anaongea lugha hiyo bila matatizo.

Vladimir alisoma sheria katika Chuo Kikuu cha Leningrad 1970 na kuhitimu 1975, thesis yake ikiwa "The Favored Nation Trading Principle in International Law". Akiwa chuoni hapo alitakiwa kujiunga na chama Cha Ujamaa cha Umoja wa Soviet, aliendelea kuwa mwanachama mpaka 1991 alipokutana na Anatoly Sobchak professor msaidizi ambae alitia chachu katika safari ya maendeleo ya Vladimir.

Mnamo 1975 Vladimir alijiunga na KGB ambako alipata mafunzo katika shule yao ya Okhta, Lenigrad. Baada ya mafunzo hayo alifanya kazi kama afisa wa juu kabla ya kuhamishwa kuwa First Chief Director na kazi yake kubwa ilikuwa kuchunguza wageni wakiwemo maofisa wa ubalozi mjini Lenigrad. Kati ya mwaka 1985-1990 alihamishiwa Dresden, Ujerumani Mashariki kwa kofia ya mkalimani. Inasadikika wakati ukuta wa uliogawa Ujerumani Mashariki na Magharibi unaanguka, Vladimir aliwahi kuchoma majalada yote ya KGB kuokoa yasiangukie mikoni mwa adui.

Baada ya anguko la Ujamaa, Ujerumani Mashariki, Vladimir alirudishwa Saint Petersburg ambako June 1991 alianza kazi katika Idara ya Mambo ya nje chuo kikuu cha Saint Ptersburg. Kazi yake kubwa hapa ilikuwa kuchunguza na kuchuja vijana wa kujiunga na KGB.

1980 Vladimir Putin akiwa kwenye uniform za KGB.

Wakati huo rafiki wa Vladimir Anatoly Sobchak akiwa meya wa Saint Petersburg, Mnamo August 1991 Vladimir aliacha kazi akiwa na cheo cha Leutani Kanali. Siku mbili tu baadae jaribio la kumpindua rais wa wakati huo wa Urusi Michael Gorbachev lilitoke. Vladimir aliwahi kusikika akisema kuwa tangia wakati mapinduzi hayo yanaanza, alishajua ni upande gani atakuwepo.

Baada ya hapo Vladimir aliteuliwa kuwa mshauri wa meya Sobchak katika maswala ya nje na alikuwa mkuu wa kitengo cha maswala ya nje katika ofisi ya meya ndani ya Saint Petersburg. Jukumu lake kubwa lilikuwa kuendeleza uwekezaji wa kimataifa na kuandikisha biashara za kimataifa. Ndani ya mwaka mmoja tu Vladimir alikuwa kwenye uchunguzi na mamlaka ya mji, uchunguzi huu uliongozwa na Marina Saliye, katika uchunguzi huu iligundiulika kuwa; Vladimir alifanya mapungufu ya bei katika vyuma vilivyouza nje vyenye thamani ya $million 93 na mauzo hayo yalibadilishwa kwa chakula kutoka nje ambacho hakikuwahi kuwasili. Pamoja na ripoti ya uchunguzi kupendekeza Vladimir afukuzwe kazi, aliendelea kuwa mkuu wa kitengo hicho mpaka 1996. Kati ya mwaka 1994-1996 alishika nafasi nyingine nyingi za siasa na serikali ndani ya Saint Petersburg.


source; The New Tsar, Rise and Reign of Putin.
 
Alizaliwa Saint Petersburg wakati huo ikijulikana kama Leningrad, October 7, 1952. Ni rais wa Urusi kwa sasa tangia May 7, 2012. Alikuwa waziri mkuu kuanzia 1999 mpaka 2000, raisi kuanzia 2000 mpaka 2008, na tena kushika nafasi ya uwaziri mkuu kutoka 2008 mpaka 2012. Katika kipindi chake cha pili cha uwaziri mkuu pia alikuwa mwenyekiti wa chama cha Umoja wa Urusi.


Umeweka maelezo na picha yake Mkuu je unataka tuchangie nini tena hapo?
 
Vladimir Vladimirovich Putin alizaliwa Saint Petersburg wakati huo ikijulikana kama Leningrad, October 7, 1952. Ni rais wa Urusi kwa sasa tangia May 7, 2012. Alikuwa waziri mkuu kuanzia 1999 mpaka 2000, raisi kuanzia 2000 mpaka 2008, na tena kushika nafasi ya uwaziri mkuu kutoka 2008 mpaka 2012. Katika kipindi chake cha pili cha uwaziri mkuu pia alikuwa mwenyekiti wa chama cha Umoja wa Urusi.



Vladimir ni mtoto wa tatu na wa mwisho kuzaliwa katika familia ya Vladimir Spiridonichich Putin na Maria Ivanova Putin. Vladimir alitanguliwa kuzaliwa na kaka zake wawili, Viktor na Albert. Bahati mbaya Albert alifariki akiwa mtoto mchanga kutokana na ugonjwa wa polio.

Habari njema .
Unataka kutuambia jambo,
Funguka....
 
The strong man Putin

Hicho kitabu kina onyesha jinsi gani kiongozi yeyote shupavu anavyotakiwa awe.

Huyu mchizi ana akili sana mara 100000000000 ya baba jeska.
 
Haujatiririka vya kutosha..nadhani ongezea kwamba ni Kiongozi pekee mwenye ushawishi mkubwa Duniani kwasasa, na pia ana nguvu kubwa sana ...
 
Back
Top Bottom