Viwanja vyetu vya ndege vimeanza tena kuwa uchochoro wa kusafirisha na kuingiza madawa ya kulevya!!!

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,137
7,711
Kumeibuka wimbi la usafirishaji na uingizaji wa madawa ya kulevya kupita uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Jana wamekamatwa watu kadhaa katika nyakati tofauti wakisafirisha madawa ya kulevya kwenda Dubai.

Kwa wimbi hili ni wazi kabisa biashara imenoga!! sasa watu wanateleza tu!!!

Pamoja na pongezi kwa viongozi wa usalama katika uwanja huo lakini bado tunaomba ukinzi mkali uendelee bila kuzembea.

Viwanja vyote vya ndege, vyote viwe na ulinzi madhubuti, tuweke watu weledi na waaminifu.

Taarifa ya kukamatwa wahalifu hao imetolewa na kituo Cha chanel ten habari tarehe 18/4/2023.
 
Nenda pale kisutu mahakamani au kinondoni Fika milango wa MAHABUSU angalia MAHABUSU wapya wanaotokea Polisi wanapochanganywa na wanaotokea jela ili kusiliza kesi zao ndiyo utajua Jela ni noma.
Ndege ikitoka Brazil ikitua Tz. Nchi imefunguliwa
 
Kama yamekamatwa kwenye Uwanja wetu wa Ndege wa JKIA inaonesha yaliingizwa na Sasa yanatoka.

Ulinzi ni vyema uimarishwe
 
Kwa sasa kila mtu atakula panapo mshibisha, wange waacha tu wameshindwa kamata mafisadi wanakamata wasaka tonge
 
Back
Top Bottom