SoC02 Namna viwanja vya wazi vinatumika kuongeza watumiaji wengi wa madawa ya kulevya Dar es salaam

Stories of Change - 2022 Competition

Hamisi Twanje

New Member
Aug 26, 2022
2
0
Serikali ilikua na lengo zuri sana kutenga maeneo ya wazi kwaajili ya matukio ya kijamii kama vile walsha, michezo, matamasha na vinginevyo vifananavyo na hivyo.

Kama ilivyo adha kwamba kila kizuri kina kasoro basi, kwa utafiti wangu nilioufanya kulizunguka jiji la dar es salaam nimegundua viwanja vya mpira au maeneo ya wazi ndio masoko yakuuzia madawa ya kulevya. Ukizuru maeneo hayo utakuta wapo kimakundi huku wakitumia madawa.

Madhara:
ni kwamba wakishavuta huunda vikundi vya kiharifu kama panya road na kushambulia watu.
Pili, hupelekea uraibu yaani (addiction) ambayo huharibu ubongo hivyo vijana wengi kupoteza mwelekeo.
Tatu, tunapoteza nguvu kazi ya taifa, kijana badala ya kuwaza kujiinua kiuchumi anawaza wizi, na uharifu.

Nini kifanyike:

Kuwepo na doria za askari wanao vaa kiraia katika maeneo ya wazi ili kubaini wauzaji wakuu wa hayo madawa na kuwachukulia hatua.
Viongozi wa serikali za mitaaa washirikishwe ili kuwabaini na kupambana na hii kadhia kwani wanawajua waharifu hao na wanaishi nao mitaaani.
serikali ianzishe sober house nyingi kuwasaidia waathirika na wakipona wapewe elimu ya ujasiliamali pamoja na mitaji ya kufanyia biashara sio kuwarudisha mitaani mikono mitupu, ikiwa hivyo watarudi kwenye uraibu.
Mwisho serikali ianzishe utaratibu wa kufundisha au kutoa semina kwa wanafunzi juu ya madhara ya dawa za kurevya.

Kwa ujenzi wa taifa bora la kesho jamii lazima ichukue hatua kupambana na hili janga linaloitesa dunia kwa sasa.
 
Back
Top Bottom