Viwanja vya madini ya dhahabu handeni.

Viwanja vya madini ya dhahabu handeni.

Alex777

Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
30
Reaction score
4
Habari Kaka/Dada zangu wa JF,


Mimi ni kijana wa kitanzania, mwenye umri wa miaka ishirini (20).

Nikijana mpenda maendeleo na kupenda kusaidia vijana na taifa zima kwa ujumla.

Namshukuru Mwenyezi MUNGU ameniwezesha kupata leseni (Hati miliki) ya viwanja zaidi ya viwili Handeni kwenye maeneo ya KILINDI, KOMKONGA NA PANGASARU.

DHUMUNI YA POST HII;
Nia na dhumuni ya post hii kwa wanajamii forum ni kuwa, ninaahitaji mtu/watu wakuweza kushirikiana nao katika uwezeshaji ilikuweza kuweka wachimbaji wadogo wadogo watakao saidia kuchimba ilikupatikana kwa dhahabu.
KAMA UPO/MPO INTERESTED MNAWEZA NI PM KWA MASWALI NA MAELEZO ZAIDI.
NAPIA USISITE/MSISITE KUNIPA MAONI AMA USHAURI KATIKA KAZI HII

Ahsanteni.


 
Good and kila kheri.
Uchimbaji wa gold nao unachangamoto sana na shida upatikanaji wake ni tofauti na madini mengine kama almasi na tanzanite.
 
Hii habari ya handeni kuna dhahabu nyingi ilimsababisha jamaa yangu kuuza nyumba yake dar!
Kaenda handeni kachimba mpaka makucha yamemalizika! Mpaka leo wizauti!
Kila la kheri mkuu!
Lkn usije kula mpaka mtaji! Chimba kwa machale machale tu!
Ukiona vipi we tafuta mwenye mahela ya ziada umpe za juu! Unamwagia mwagia ile ming'ao ng'ao pembeni ya huo mgodi halafu Kiwanja million 100!
Teh teh teh teh!
 
Hongera mkuu kwa juhudi uonyeshazo. Kwa kilindi naweza pata madini gani ya vito?
Salaam
 
Ahsante sana, panapo nihusu mimi ni dhahabu tu aisee.
 
Mkuu mie pia mzee wangu anaviwanja huko,ni PM tuwasiliane zaidi namna ya kufanya.
 
mdogo wangu uchimbaji wa dhahabu unahitaji akili na si fedha kwakifupi unatakiwa ujue
- aina ya mwamba (kama ni milimani utachemka katikati kupasua mawe)
- umbali ulipo mwamba
- ppm za gold zinasoma ngapi, ppm za sulpur, copper zinasomaje
- changamoto ya maji
- utatumia vifaa gani kuchimba
Taarifa hizi utazipata kwa jirani zako na baada ya hapo utaamua kuchimba au kuacha

Uwezeshaji: watembelee bank ya TIB wanatoa mikopo kwa wachimbaji wadogo japo muda wa kurudisha ni kama miezi 12
 
chimba kitaalamu usije ng'ooka kucha bure organise gold detector machine ufanye survey all the best
 
Back
Top Bottom